Habarini,
Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wanaume tuliowengi juu ya tabia ya wanawake walio wengi kupenda kuomba hela kutoka kwa wanaume.
Lakini cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu kipenzi ambaye ana Girlfriend wake ambaye amefikia hatua ya kutomthamini wala kumpenda kabisa sio labda kwa sababu anatabia mbaya au laa ila ni kwa sababu rafiki yake wa kike sio mpenda pesa
Yani tangu wawe katika mahusiano wana muda kama miezi 6 inakaribia ila huyu msichana hajawahi kumuomba pesa kwa shida yeyote ile. Yani hata wakitoka mwanamke huwa mambo karibu mengi anagharamia.
Kuna muda jamaa anajisikia weak saana eti kwa sababu tuu hajawahi kumgharamia wakiwa pamoja au katika mahitaji yake mfano kusuka n.k
Akimletea zawadi za gharama binti huwa anashukuru ila huwa anamhurumia kwa kumwambia hupaswi kufanya hivyo. Wala sipendi wewe kuingia gharama kwa sababu yangu.
Kuna kipindi huwa anamlazimishia kumpa pesa, binti wa watu huwa anakataa kabisa. Jamaa anachojaribu huwa ni kumpa kwa lazima na pia huwa anampa kwa njia ya kumuachia bila ya yeye kujua.
Ila pamoja na binti huyu kutokuwa na tabia ya kupenda pesa kutoka kwa boyfriend wake yupo loyal kwa mpenzi wake na nlipomuuliza rafiki yangu huyu iether kama anadharau au kutokumheshimu binti wa watu hana hayo yote ni mskivu mno.
Paka maamuzi ya mwisho jamaa anaamua kumpotezea binti huyu na kutomjali.
Kitu ambacho nimejiuliza bila kupata majibu kwa sisi wanaume hivi tunatatizo gani!?
Kumpa hela mwanamke ndio sababu ya kuwa confident kwa mwanamke? Kama huyu jamaa anavyodai
Kwanini wanaume tunashindwa kuthamini wanawake wa aina hii!?
Wabarikiwe wanawake wa aina hii kwakweli maana ni wachache mno.
Pia wale wapenda pesa salam kwenu, maana mnaweza achwa kama huyu binti kisa tuu hamuombi pesa.