Sidhani kama hoja ya umri ina matter sana. Tabia za mtu na kuwa na umri mdogo au mkubwa si hoja ya msingi. Maana tunajionea wazi, watoto wa miaka 18 ni watu wazima kuliko wazazi wao. Yaani mtu kapitia mambo ambayo hata mzazi wake hajapitia.
Dunia ya sasa imebadilika. Ukipata mtu mwenye tabia njema, akiwa na miaka 23 au 30, mshukuru Mungu sana.
Wenye miaka iliyoenda wengi wanaona upuuzi kupoteza muda kwa kufanya mambo ya kijinga wakati watoto wanaona bado wana muda mwingi wa kuchezea na vice versa.
Pia ndoa za siku hizi wadada wengi wamepoteza interest sana. Na hii ni baadhi ya wanaojielewa na wanatazama future.
Kiukweli kwa maisha ya sasa, 23 bado anasoma. Akiacha kazi akimbilie kuolewa, je wanaume mna ubavu wa kumkubali kumuhudumia kwa kila hitaji lake? Najua ni wachache sana.
Wengi watamuona binti hana akili, ni mtu asiye na future, hana msaada hata inapotokea tatizo na dharau nyingi tu.
Mwisho mdada ataona ndoa chungu. Ila hatokuwa na pa kukimbilia. Atakuwa mtumwa maisha yake yote.
Tuacheni tujijenge jamani. Ndoa kama ipo ipo tu. Ukiwa na 20 au 50, its does not matter. What matters ni kufika malengo yako uliyojiwekea.
Kama malengo ni ndoa, go for it, kama ni kutengeneza kampuni do it, kama ni kusoma fanya hivyo.