Wanaume tuwe wasafi jamani!

Wanaume tuwe wasafi jamani!

hapana, ukifika home kabla ya kulala brush basi. Kila siku mnalalamika wake zenu hawawapi cha alfajiri; sasa utamkiss vipi kwa domo lililochacha na mibeer na mikachumbari!

wanawake wako sensitive sana na harufu!

unaona ,mbali sana wewe.....................
 
Kuna Mambo sisi wanaume lazima tuyaache na tujue jinsi ya kuwa wasafi.

1. Mtu soksi zinanuka kwa sababu ya kuvaliwa kwa muda mrefu haoni kama ni tatizo

2. Hotelini mtu anasukutua na kutemea mate au kohozi kwenye sink linalotumiwa na watu wote. raha mustarehe

3. Una Soksi ina bonge la tobo kwenye kisigino na kwenye dole gumba lakini bila ya aibu unaivua mbele za watu.

4. Unaingiza dole lako kwenye pua na kutoa Kamasi au ugando wa kamasi bila ya wasiwasi mbele za watu

5. Unafanya kazi Gereji hufui nguo zako hadi tofauti kati yako na Grease za gereji inakuwa sawasawa na Ziro

6. Unajijua una kikwapa lakini kunyoa nywele zako za kwapani inakuwa ni mgogoro mkubwa.

7. Unakula kitimoto, unakunywa bia na vitu vingine kadha wa kadha,lakini mswaki kwako mwiko!

8. Huwezi kuoga mpaka ujue unakwenda kwenye kideti kipya.

9. Domo lako unajua kwamba linanuka lakini wewe ndiyo kinara wa kutaka kunong'oneza watu.

Hizi ni tabia ambazo baadhi yetu wanaume tunazo ila wengine wanazitetea eti ndiyo "udume" jamani tuwe wasafi kwani usafi nao ni sehemu inayochochea mapenzi.

hizi siyo sifa za mwanaume, usipotoshe watu wewe, kama we ndo ulivyo then don't generalize coz wengine tupo smart 24/7.
Usirudie kuandika uharo hapa!
 
dah sjui nikupe nini wewe??
ahh umeongea fresh jaman...lijitu linanuka kwapa utasema kaficha tope la choo

ahh kuna njemba moja iyo olevel ebwna ehh sjapata mfanoe yule bwana alikuwa anapenda kunihug kila akiniona na akishanihug anataka aninongoneze et ata masomo mema ye anataka anisemee kisikion sasa BALAA LAKE ILO KWAPA jaman ahh yaan akipanua mkono utasema kuna jalala limefunguliwa...na izo njino zinavyonuka jaman,...dahh afu anapenda kuzungumza chngereza mda wote bas watu wakawa WANAMPONDA AHH HAUNA LOLOTE MWINGEREZA GAN DOMO LINATEMA..raha ya chngereza domo livutie..

Ha! Ha! Ha! Ha!!...lol..
 
Lakini toothpick siyo dental floss!!!
NN huku nylon filaments au zile plastic ribbon zinazotumika kutoa masalia ya chakula na dental plaque kwenye meno sidhani kwanza kama watu wanazitumia au wanazijua kama wapo ni wachache, watu wamezoea toothpick kwa kwenda mbele lol!!
 
Wanatumia vijiti vya chelewa kaka!
 
Kuna Mambo sisi wanaume lazima tuyaache na tujue jinsi ya kuwa wasafi.

1. Mtu soksi zinanuka kwa sababu ya kuvaliwa kwa muda mrefu haoni kama ni tatizo

2. Hotelini mtu anasukutua na kutemea mate au kohozi kwenye sink linalotumiwa na watu wote. raha mustarehe

3. Una Soksi ina bonge la tobo kwenye kisigino na kwenye dole gumba lakini bila ya aibu unaivua mbele za watu.

4. Unaingiza dole lako kwenye pua na kutoa Kamasi au ugando wa kamasi bila ya wasiwasi mbele za watu

5. Unafanya kazi Gereji hufui nguo zako hadi tofauti kati yako na Grease za gereji inakuwa sawasawa na Ziro

6. Unajijua una kikwapa lakini kunyoa nywele zako za kwapani inakuwa ni mgogoro mkubwa.

7. Unakula kitimoto, unakunywa bia na vitu vingine kadha wa kadha,lakini mswaki kwako mwiko!

8. Huwezi kuoga mpaka ujue unakwenda kwenye kideti kipya.

9. Domo lako unajua kwamba linanuka lakini wewe ndiyo kinara wa kutaka kunong'oneza watu.

Hizi ni tabia ambazo baadhi yetu wanaume tunazo ila wengine wanazitetea eti ndiyo "udume" jamani tuwe wasafi kwani usafi nao ni sehemu inayochochea mapenzi.

Hili ni tatizo kubwa sana..si kwa wanaume tu hata kwa wanawake..
Wengi wa wenye tatizo hili hawajui namna ya kusafisha kinywa; wengi uwa wanakazana kusafisha meno tu huku wakiupa usafi wa ulimi muda mfupi. Ulimi ndio chanzo cha mdomo kunuka au kutonuka.
Ewe dada na kaka safisha ulimi wako angalau kwa dakika 5 asubuhi na jioni ili kuondoa harufu mbaya kinywani.
 
nimewahi kuambiwa na dokta mmoja kuwa naturally, kati ya watu 1000; ni watu wawili tu wasionuka mdomo.

Hili ni tatizo kubwa sana..si kwa wanaume tu hata kwa wanawake..
Wengi wa wenye tatizo hili hawajui namna ya kusafisha kinywa; wengi uwa wanakazana kusafisha meno tu huku wakiupa usafi wa ulimi muda mfupi. Ulimi ndio chanzo cha mdomo kunuka au kutonuka.
Ewe dada na kaka safisha ulimi wako angalau kwa dakika 5 asubuhi na jioni ili kuondoa harufu mbaya kinywani.
 
Waambie hao, ila kuna wanaume ni wasafi hadi raha.
 
mkuu uko juu sana. Hebu weka hii namba 10. kupendelea kuvaa chupi zaidi ya maramoja, hata siku 3.
 
Huu utata wa maharufu na mauoza mengine ni wanaume tu au na wanawake??nionavyo mimi wanawake pia pamoja na hayo yaliyotajwa, ongeza na yale mambo yetu yale.
 
Back
Top Bottom