Wanaume!!! Usahaulifu wenu unatuumiza....

Yaani wakati unaninunia najisemea huyu mwanamke kweli ananinunia jambo dogo hivi Mungu amsamehee tu.

miezi michache imepita nilinuniwa kisa nimesahau tarehe ya likizo....Vingine unafikiri tunajitakia kusahau sasa...
Usilete masihara, ukumbuke hadi size yake ya kiatu Kama sio kiuno.
 
Nilikua nashangaa uwezo wako wa kunivumilia. Asante kwa kuonesha kiasi gani unaumia. Nitajitahidi kukumbuka.

Hilo halipunguzi upendo wangu kwako. Ukishindwa kuniambia kule njoo huku ujumbe wangu nitaujua tu.
Pamoja na kuwa mmeumbwa kusahau, lakini wakati mwingine jitahidini kukumbuka.
Ni vitu vidogo sana ila vinatuumiza sana.

Hapa ni kwa ujumla, sio lazima uwe kwenye mahusiano, hata kaka, baba, mjomba nk.
 
ndio dada, mambo mengi kichwani...

nikumbuke meeting na minutes zake halafu bado nianze kukumbuka na siku ya kuzaliwa, anyway uzuri teknolojia inatusaidia
Mbona vingine hamvisahau?
Vile vinavyowahusu haswaaaa.....
 
Jana alikwambia mtoto bamkubwa leo anakwambia mke wa rafiki yake (shemela wake)
 
Vipi siku yako ya kuzaliwa imepita kavu bila kupata ujumbe wa kheri kutoka kwa Mr....

Wakati mwingine mtuhurumie aisee sasa hali imekuwa ngumu kwelikweli muda wowote unawaaza ada za watoto... kodi ya nyumba bado kuna madogo na ndugu pia wanakutegemea so tunajikuta tunasahau hivyo vitu vidogo [emoji45][emoji45][emoji45][emoji45][emoji45]
 
Wengine unakuta hata hawalipi hivyo wanamtegea mwanamke halafu wanasahau.
 
Yaani mimi hata hamnipi stress. Mtu asahau au akumbuke ni sawa tu maisha yanaenda. Hata usahau kitu gani nakuangalia tu as long as sio jambo linalosababisha mtu afe.

Unajifanya una moyo wa chuma
 
Yaani mimi hata hamnipi stress. Mtu asahau au akumbuke ni sawa tu maisha yanaenda. Hata usahau kitu gani nakuangalia tu as long as sio jambo linalosababisha mtu afe.
Eeehhh, unayaweza basi...
Yaani nikishakuweka kwa Moyo ujue hakuna kidogo wala kikubwa....maumivu yake yanafanana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…