Nakapanya
JF-Expert Member
- May 22, 2012
- 2,096
- 709
Inatokea kuna mdada umempenda sana,unachukua uamuzi wa kumtongoza na yeye bila hiyana anakukubalia,mnaingia kwenye mahusiano,inapita kama miezi 3 bila kukutana kimwili tangu muanze uhusiano maana kila ukimuomba penzi anakuzungusha kwa sababu mbalimbali na ahadi zisizotimilika.Unaamua kutulia tu;siku moja unapokea sms yake inasema hivi,"HONEY NAKUPENDA SANA,NAPENDA KUWA NAWE ILA KABLA SIJALALA NAWE/KUFANYA MAPENZI NAOMBA UNILIPIE PANGO LA NYUMBA MIEZI 6(72000) COZ KWASASA SINA KAMAPANI NA NIMEFULIA,JE UPO TAYARI?".sasa kama ungekuwa wewe ungefanyaje?