oooh Wait,
hii siwezi kuiacha ipite.........
Nimeishi Arusha Na moshi kwa muda mrefu sana ndo nilipozaliwa na kusomea.....ila kwa sasa naishi Dar,Tufahamu kabisa kuwa kila wanaume wa kila mkoa wana tofauti,hii inatokana na mila ,mazingira na hata malezi,pia na majirani,wakati nikiishi arusha na Moshi nilikua nikidharau sana wanaume wenzangu wa dar (na hii ni kila mtu anaeishi moshi na arusha anafanya) nilikua nawaona soft,wanajiremba,masharobaro na wako kama wanawake hv,hii inatokana na ubabe,ukorofi,majigambo na ukorofi niliokua nao (wengi wa moshi na arusha wapo hivyo) lakini pia nilikua najua watu wa dar hawana hela kama Arusha,ila nilijua matajiri wengi wa dar wameoriginate Arusha au moshi...
Then Nikahamia Dar,
Ilinibidi kubadilisha attitude yangu,watu wa Dar hawana ubabe na hasira za faster,wana connection na atleast kila kitu,cash ipo dar nyingi kuliko arusha,na pia watu wa hapa wako real kwenye biashara kama ni biashara hamna sound na longo longo kama arusha na Moshi,pia nilinote kuwa matajiri na wenye hela wapo dar,hapa dar ukileta ubabe wako wa arusha au moshi unaweza kufungwa hata maisha...ila arusha itakua ni kuchomana visu au visasi vya kuuana...
Mwisho,
Arusha kuna madini,Ardhi yenye rutuba,UN wapo pale,Mlima kilimanjaro then na biashara ya utalii,maisha yapo juu sana lakini mzunguko wake wa hela ni mkubwa si kama mbeya ,tabora na mikoa mingi ya tanzania lakini kiukweli Dar hailingani na arusha kwa chochote, Dar Hamna kitu zaidi ya bahari,watu hawalimi chochote lakini sijawahi kusikia Kuna njaa hapa dar,utaskia Sumbawanga,Rombo na kwingineko wakati huko ndo kuna mashamba ya vyakula.....
kwa Ushauri wa wanaume wa Moshi na Arusha,
Wajiulize kwa nini mtu wa arusha au Moshi au arusha Akijaribu biashara au maisha hapa dar huwa harudi huko tena anahamia moja kwa moja!
Najua PJ atakuja hapa ila wanaume wa Dar ni kiboko ya wale wa Arusha-Pls Note mi ni mwanaume wa Arusha.
Nawakilisha