Wanaume wa Dar acheni ushamba kwani kipi cha ajabu hapa?

harder king

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
3,970
Reaction score
6,907
Wasalam wakuu!
Ni iv..baada ya kusikia misifa kibao kwa hawa watu Wa 'dar es salam' kuhusu uzuri Wa kijiji chao..tukaona isiwe tabu,tukazichanga Mimi na mwanangu kama mwezi iv..lengo kwenda kusafisha macho na kupunguza ushamba wa kurushwa roho na hawa watu kila wakija huku kijijini

Siku ikafika tukajiandaa na kitita chetu cha mkwanja kila MTU akiwa na burungutu la pesa kama laki na nusu 150000 nje na nauli ya kwenda na kurudi na malazi..

Baada ya kufika dar es salaam kweli kuna vingi vilituacha mdomo wazi..aisee asikuambie mtu..kwanza kuvuka tu barabara ilikua tatizo kwetu..yale magari yanayofanana cjui ndio mwendo kasi..sasa kuna mabasi mengine mareefu af linakatika katika kama mdudu flan yan..hapa nitoe ongera kwa wana daslam kwa ujasiri..,mimi hule mgari ata kuusogelea nliogopa eroo..! Japo mwanangu akua mgeni wa huu usafiri Wa uma,ilinitoa wasi wasi lakini sikumuelewa kabisa.. siwezi kufa kabla ya wakati arifu!

Sasa niliipo ona hawa wanaume wa dar hatuwaonei kwa kejeli tunazo watupia kutoka mikoani ni pale Mimi na mwanangu tukiwa maeneo ya kujidai ile mida ya kulala Kuku..

Kwanza tumefika sehemu tukaagiza kitimoto rost kilo na nusu ili kuweka tumbo sawa,mudumu Wa vinywaji tukamuagiza faru joni..tukiwa tunamshusha huyo faru ile rost ikawasili
Kabla mudumu hajaondoka tukamwambia atuandalie kilo na nusu nyingine ya kukausha,nikamuona muduma kama kashtu ila akapotezea kafuata maagizo..kumbe hakua mudumu tu ata wanaume waliokua meza za jirani walikua wakitutumbulia mimacho bila sisi kujua sababu..
Tulipo maliza rost na kumalizia na yule faru..tukamuita Dada Wa vinywaji akatuongezie jibapa jingine..limekaribia katikati ile kitimoto ya kukausha ikawasili..hapa ndio wale wanaume Wa meza jirani walipagawa na 'viserenget lite' vyao..tumemaliza tukaongeza jipaba la tatu..aisee wale wanaume Wa dar wakaanza kutuseme cjui walifikir konyagi ishatuziba masikio hatuwasikii..
Mara cjui hawa watatufia hapa..ooh wamelogewa pombe cjui hawataweza nyanyuka..sisi tunalishusha huku tunawasikiliza hawa 'wambea Wa dar' baada ya kumaliza tukaongeza kilo moja ya kurost na Mdogo wake fara joni(ml500)
Na kuwambia watuandalie bili..
Wale wanaume na kiserenget kimoja kinanywewa masaa matatu wameduaa tu ata umbea umewaishia wametulia tulii..! wanatuangalia tu..
Yule mudumu alipo leta bili akapayuka kwa nguvu HAWA NDIO WANAUME SASA..
tukalipa tukanyanyuka tukiwa wazima kama tulivyo kuja, tukawaacha wanaume Wa dar midomo wazi..sisi haoo mwendo mdundo kwenda kulala

Sasa nyie wanaume Wa dar es salaam kama mmezoe kiepe yai na vibia biwili mkizid vi3 tena lite msitake na sisi tufanane na nyie!!
Tena ile kwetu ni kama kupiga kiwe kiatu tu sababu ya uchumi sasa sijui mkitukuta tumeuza miogo mifuko imetuna si mtazimia nyie.
PUNGUZENI USHAMBA!!




young kilimanjaro
 
Kula uliwe .......[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4]

Fursa2017
 
Ha haa! Tofauti ya watu wa Dar na mikoani ni kuwa, watu wa Dar wanatumia akili nyingi hivyo hawahitaji misuli na watu wa mikoani wanatumia misuli hivyo hawahitaji akili nyingi na ndio maana wanakula sana.
 
Ha haa! Tofauti ya watu wa Dar na mikoani ni kuwa, watu wa Dar wanatumia akili nyingi hivyo hawahitaji misuli na watu wa mikoani wanatumia misuli hivyo hawahitaji akili nyingi na ndio maana wanakula sana.
Ad mnashindwa na wake zenu kula kisa akili?

young kilimanjaro
 
Umekosea njia, umeenda Gongo la Mboto , Uwanja wa Fisi au Manzese kwa mfuga Mbwa?
Hivyo si viwanja vya mtu wa hadhi ya JF!
Ole wako kama hutapata kipundupindu jijini hapa kwa kufamakia rosti za vibudu vya Vingunguti!!
 
Umekosea njia, umeenda Gongo la Mboto , Uwanja wa Fisi au Manzese kwa mfuga Mbwa?
Hivyo si viwanja vya mtu wa hadhi ya JF!
Ole wako kama hutapata kipundupindu jijini hapa kwa kufamakia rosti za vibudu vya Vingunguti!!
Sio gongo la mboto mkuu,
Ni sehemu kuna watu wazito na magari ya kifahari yamepaki

young kilimanjaro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…