Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
WANAUME WA DAR HUOGOPWA ZAIDI NA WANAUME WA MIKOANI!
Anaandika Robert Heriel
Ili uwe mwanaume wa Dar itakupasa uwe umeishi Dar kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo, wanaume wa Dar wanaogopwa Sana na wanaume wa mikoani tangu nchi hii ipate Uhuru. Zipo sababu nyingi za Jambo hili kuwa kama lilivyo,
Mbali na kuogopwa pia Wanachukiwa na baadhi ya wanaume wa mikoani hasa Mkoa WA Arusha. Chuki nyingi huwa zakijinga na zakishamba Fulani hivi.
Mwanaume WA Dar attitude yake Kwa mtu wa mkoani ni Sawa na Attitude ya Mzungu Kwa muafrika. Yaani Mwanaume WA Dar hujiona Bora na kamwe hamuhofii mwanaume wa mkoani.
Wanaume wa Dar hujikita zaidi kutatua mambo Yao kiakili kuliko nguvu ilhali wamikoani hujikita kutatua mambo Yao Kwa kutumia nguvu kuliko Akili.
Linapokuja suala la Wanawake na mahusiano,.wanaume wa Dar hupendwa zaidi na wanawake kuliko wanaume wa mikoani na hii huwafanya wanaume wa mikoani kuwa na wivu wa kijinga hata hivyo wanaume wa DAR hawanaga muda wa kujadili mambo na watu wanaowaona ni washamba, Kama nilivyosema Attitude ya Mwanaume wa Dar ni Sawa na Attitude ya Mzungu dhidi ya muafrika.
Ni rahisi mwanaume wa Dar kwenda Mkoa wowote akaopoa Demu ndani ya siku moja lakini ni ngumu Sana Kwa Mwanaume WA mkoani kuopoa Demu akija DAR hata akipewa wiki nzima, labda akanunue Dadapoa.
Wanaume wa Dar wakifika mkoani kwenye sherehe hupewa Huduma maalumu ya heshima ni Kama vile Mzungu atoke Ulaya aje Tanzania anavyopewa Care ya kutosha, lakini wanaume wa mikoani wakija DAR hawachukuliwi Sirius hupewa Majina Kama Mjomba wangu kutoka kijiji, Mlugaluga, na mtu Pori.
Wanaume wa Dar huwa Kama reference Kwa Vijana walioko shuleni huko mikoani, wazazi huwaambia watoto wasome ili waende DAR wakaishi Kama Fulani (ndugu Yao aliyehama miaka mingi iliyopita)
Ni nadra Sana wanaume wa Dar kutaka kuishi mikoani Ila ni kitu cha kawaida Wanaume WA mikoani kuhangaika walau waje kupaona DAR.
Kuishi DAR Kwa nchi ya Tanzania kuna MPA mtu fursa nyingi za kijamii, kiuchumi na Kisiasa, lakini kuishi mkoani kunam-limit mtu kifursa.
Ukienda mkoani mwanaume wa Dar hajielezi Sana Kwa Warembo, atasema anaishi DAR na amepanga yupo pekeake, huyo Demu akisikia hivyo anaweza vunja mahusiano na mchumba wake ili aje DAR na Mwanaume WA Dar.
Wanaume wa Dar wanjisifia akili wakati wanaume wa mikoani wanajisifia nguvu, hii ni kutokana na tofauti za kimaeneo. Majiji makubwa huhitaji akili zaidi ili uweze kuishi maisha mazuri kuliko nguvu, wakati mikoani hata ukitumia akili ya NG'OMBE unaweza kuishi.
Wazoefu wa DAR ni nadra sana kuwakuta wanafanya mambo ya ajabu Kama kuvaa nguo za uchi, Ila Watu WA mkoani wakija wengi wao ndio hufanya vitu vya ajabu kuonyesha ulimbukeni wao.
Viongozi na matajiri wote wakubwa wanapenda kuishi DAR hivyo wamegeuka Wanaume wa Dar Kwa sababu wanaona kuwa mtu wa mkoani hawastahili hadhi hiyo.
Wao mtazamo wao ni kuwa Majiji makubwa yapo Kwa ajili ya watu wakubwa Kama wao, mikoani au shambani wanapaona Kama Kwa Watu wasioweza mapambano, Wazee ndio maana wakizeeka huamua Kurudi mikoani ili kuepusha vurugu za Mjini.
Wanaume WA DAR wanaenjoi zaidi maisha kuliko wanaume wa Mikoani hasa kipindi cha ujana Mpaka utu uzima, wakati wanaume wa mikoani huyafurahia maisha zaidi ya wanaume wa mikoani nyakati za uzee kwani wengi huwa na angalau vijumba mshenzi vya kujistiri huku wanaume wa Dar wakiwa hawana lolote.
Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Moshi Mjini