Wakati naandika hii comment nipo bar ya jirani na home nacheki game ya aseno dhidi ya liver. Mbele yangu kuna serengeti lite baridiiii. Watoto n wife wapo home wanacheki tamthilia zao wanazozipenda wakisubiri mshua mimalize kucheki game na wana then niwabebe kitimoto wakale na chips atakazokaanga mama yao home.
Sasa ni hivi wewe wakupita njia. Hapa mjini kuishi ili kumaliza siku kwa mafanikio inahitajika akili ichangamke kweli kweli na iwe sober kwa muda wote. Hizi pombe tunazokunywa sisi sio kwa ajili ya kuikomoa akili na mwili. Hatunywi tu ili mradi tilewe no, bali ili tuinjoi huku akili na mwili bado vikiendelea kuwa fiti ili kesho tuamke tukiwa fresh kimwili, kiakili na hata kiroho kwa ajili y kuendelea na mishe za town..
Kwanini unywe pombe huku unakunja sura? Kwa nini unywe pombe ambazo zinachosha mwili na akili, kesho utapigaje mishe? Halafu hizi pombe ili ulewe unahitajo unywe nyingi, so ni mtindo tu wa maisha kuonyesha mjini pesa sio ishu, ishu ni kuwa na akili za kuipata hiyo pesa. Shibaaamit