Youngblood
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 19,433
- 56,810
- Thread starter
-
- #41
Hao ni ndugu zangu lazima niwaambie ukweli,na nyie watu wa mjini mnaogoza kuagiza batabna kuku kutoka huku vijijini,muache kutubebesha mizigo.Umecatch kabisa yani. [emoji2362] Let people do whatever sails their boat, as long as it doesn’t sink yours. Waache watu warushe vitambi vyao na wewe pambana na bata wako na mahindi yako mabichi [emoji2960]
Ona sasa ndio mana tunasema hamna uvumilivu na ujasiri wa kupambana na mambo vishawishi [emoji23]gm nikienda naishia kutamani mademu wamlendani tuu.mdawote mbooinadinda
Usitupigie keleleWanaume wa dar mnaitwa huku
😅😅😅Usitupigie kelele
Mi sio mwanaume wa dar ila mziki wa chatu naujua Kuna siku nlikuwa nawinda aiseee chatu akamdaka mbwa wangu ilibidi nipate kampan ya kumwokoa, tulimwokoa mbwa japo alivunjikaNilijua tu wanaume wa Daslam mtabisha mana hizo guts hamna
Huu ni umamaBasi bwana juzi baada ya kipindi kirefu kupita nikiwa nimejichimbia huko kijijini kwetu Ushongo pangani,nikaona isiwe tabu niende mjini kati Daslam kwaajili ya kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya pamoja na mambo ya shule januari.
Basi bwana nipo zangu ndani ya Tashreef chombo imeivaa full AC, tumefika tegeta nyuki kuna abiria alikuwa anashuka pale, jambo la kwanza baada ya kufunguliwa mlango ni harufu kali ya uozo na vinyesi baada ya watu kuzibua mitaro,unajua tena Dar kipindi cha mvua ndo wakati wake. Mji unanuka... basi nikaona isiwe tabu maadamu wenyewe wamezoea na supu ya pweza wanapiga bila kutapika sio mbaya.
Gari ikatembea mpaka stendi ya Magufuli pale wakashuka baadhi ya abiria wengine tukaanza safari kuelekea Magomeni mapipa,kufika pale sijui ni kimara au mbezi kwenye lile daraja la kuvuka kwa miguu naona wanaume kibao na vibukta vyao eti wanapanda ngazi na kushuka wanafanya mazoezi
Nikajisemea moyoni hawa kweli wanafanya mazoezi au show off tu....nikavunga zangu nikamwambia konda usisahau kunishusha shekilango mana nimebeba bata wangu wawili na mahindi mabichi nampelekea mjomba kama zawadi,mana nitapata nao shida kama nikipitishwa kituo.
Basi ile njia nzima kuanzia stendi ya magufuli ni wanaume tu na viboksa wanakimbia pembezoni mwa barabara na mbwembwe kibao za kupiga push up na kuruka ruka kamba huku wakipishana na magari na pikipiki....cha ajabu wengi wana vitambi vikubwa sana,ila viatu walivyovaa vimechakaa ikimaanisha hayo mazoezi wameanza siku nyingi lakini workdone inaonyesha kuwa ni zero bin sufuri ,mana hawafanyi mazoezi bali wanaturingishia vibukta na vi Nike na Adidas uchwara vya mlimani city.
Nikakumbuka kule kwetu pangani wanaume kijiji kizima hakuna ambaye hana six pack, wakati huko mjini Daslam nasikia kuna watu wanawekewa mapulizo tumboni ili wapungue uzito na vitambi,nikacheka sana....
......kule kwetu ushongo watu tunachana mbao za Minazi kwa kututumia ile misumeno ya juu- chini na kupalilia mkonge asubuhi,na mchana wa jua kali bila shida.
Nikapata wazo moja kichwani kwamba kinachowasumbua wanaume wa dar ni tamaa,majivuno na kupenda mteremko katika mambo yanayohitaji mabadiliko na juhudi,mwanaume wa kweli huwezi kutoka nyumbani ukaenda Mloganzila kuweka puto tumboni ili upungue uzito,inamaana umeshindwa kujizuia kula supu ya pweza na chips mayai rojorojo.
Nikajiuliza moyoni hivi hawa jamaa wanaoruka humu mitaroni wakijifanya wanafanya mazoezi wangekuwa na nia kweli si wangetafuta mashamba huko chanika ndani ndani au bagamoyo wakalime kila weekend waone kama vitambi vitabaki
Nikakumbuka wanaume wengi wa jiji la Daslam maneno mengi lakini uvumilivu na juhudi hawana, mana nimewahi kusikia panya road watatu walifunga mtaa mzima huko buza huku wanaume kwa wanawake wote wamejifungia ndani siku nzima,.....wakati nakumbuka kipindi hicho nina umri wa miaka kumi tu niliuwa chatu kule kijijini kwetu bila hata kuwa na kiwembe.
Kwaherini mpaka kipindi kingine tena nikija mjini tena,wapeni hai wale majamaa wavaa vibukta wakiwa na vi mackbook/laptop wanafanya kazi wakiwa night club, bado mpaka leo najiuliza huwa wanafanya kazi zipi nashindwa kupata majibu.
[emoji23][emoji23] inawezekanawee kuweza mkuu?
Unapajua pangani mkuu au umeishia barabarani huko Tanga mjiniKwani watu wa Tanga na Dar wana tofauti?
Me naonaga ni warembo wale wale.
Mwanaume halisi yupo kanda ya ziwa
Mi niliweza kuuwa chatu mwenyeweMi sio mwanaume wa dar ila mziki wa chatu naujua Kuna siku nlikuwa nawinda aiseee chatu akamdaka mbwa wangu ilibidi nipate kampan ya kumwokoa, tulimwokoa mbwa japo alivunjika
Punguza makasirikoHuu ni umama
Mkuu hujui kwamba kuna njia ya Wazo hillGari likafika Tegeta Nyuki, likaenda Stand ya Magufuli, halafu likaja kukushusha Shekilango!!?
Labda hakua mkubwa sanaMi niliweza kuuwa chatu mwenyewe
Mkuu tayari nimekimbia mji maisha ya kushindia slice mbili za mkate siwezikumbuka umekuja dar na wewe yatakukuta tu. huku asubuhi utalishwa mkate na asali, hujatulia hapo shekilango maeneo la legho mchana utapigwa kitimoto na ugali (kitam balaa)[emoji1787]
usiku hujapelekwa wavuvi camp ama M.burger ukale kisinia ukitamani kurudi kwenu niite mbwa. nawewe utajiunga nao tu.
Ila mkuu umewasiliba! Sasa na wewe six pack zina kazi gani? Hao hao wa Dar wanaotafuta 6 pack wameanza kulialia kwamba wanagongewa!Basi bwana juzi baada ya kipindi kirefu kupita nikiwa nimejichimbia huko kijijini kwetu Ushongo pangani,nikaona isiwe tabu niende mjini kati Daslam kwaajili ya kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya pamoja na mambo ya shule januari.
Basi bwana nipo zangu ndani ya Tashreef chombo imeivaa full AC, tumefika tegeta nyuki kuna abiria alikuwa anashuka pale, jambo la kwanza baada ya kufunguliwa mlango ni harufu kali ya uozo na vinyesi baada ya watu kuzibua mitaro,unajua tena Dar kipindi cha mvua ndo wakati wake. Mji unanuka... basi nikaona isiwe tabu maadamu wenyewe wamezoea na supu ya pweza wanapiga bila kutapika sio mbaya.
Gari ikatembea mpaka stendi ya Magufuli pale wakashuka baadhi ya abiria wengine tukaanza safari kuelekea Magomeni mapipa,kufika pale sijui ni kimara au mbezi kwenye lile daraja la kuvuka kwa miguu naona wanaume kibao na vibukta vyao eti wanapanda ngazi na kushuka wanafanya mazoezi
Nikajisemea moyoni hawa kweli wanafanya mazoezi au show off tu....nikavunga zangu nikamwambia konda usisahau kunishusha shekilango mana nimebeba bata wangu wawili na mahindi mabichi nampelekea mjomba kama zawadi,mana nitapata nao shida kama nikipitishwa kituo.
Basi ile njia nzima kuanzia stendi ya magufuli ni wanaume tu na viboksa wanakimbia pembezoni mwa barabara na mbwembwe kibao za kupiga push up na kuruka ruka kamba huku wakipishana na magari na pikipiki....cha ajabu wengi wana vitambi vikubwa sana,ila viatu walivyovaa vimechakaa ikimaanisha hayo mazoezi wameanza siku nyingi lakini workdone inaonyesha kuwa ni zero bin sufuri ,mana hawafanyi mazoezi bali wanaturingishia vibukta na vi Nike na Adidas uchwara vya mlimani city.
Nikakumbuka kule kwetu pangani wanaume kijiji kizima hakuna ambaye hana six pack, wakati huko mjini Daslam nasikia kuna watu wanawekewa mapulizo tumboni ili wapungue uzito na vitambi,nikacheka sana....
......kule kwetu ushongo watu tunachana mbao za Minazi kwa kututumia ile misumeno ya juu- chini na kupalilia mkonge asubuhi,na mchana wa jua kali bila shida.
Nikapata wazo moja kichwani kwamba kinachowasumbua wanaume wa dar ni tamaa,majivuno na kupenda mteremko katika mambo yanayohitaji mabadiliko na juhudi,mwanaume wa kweli huwezi kutoka nyumbani ukaenda Mloganzila kuweka puto tumboni ili upungue uzito,inamaana umeshindwa kujizuia kula supu ya pweza na chips mayai rojorojo.
Nikajiuliza moyoni hivi hawa jamaa wanaoruka humu mitaroni wakijifanya wanafanya mazoezi wangekuwa na nia kweli si wangetafuta mashamba huko chanika ndani ndani au bagamoyo wakalime kila weekend waone kama vitambi vitabaki
Nikakumbuka wanaume wengi wa jiji la Daslam maneno mengi lakini uvumilivu na juhudi hawana, mana nimewahi kusikia panya road watatu walifunga mtaa mzima huko buza huku wanaume kwa wanawake wote wamejifungia ndani siku nzima,.....wakati nakumbuka kipindi hicho nina umri wa miaka kumi tu niliuwa chatu kule kijijini kwetu bila hata kuwa na kiwembe.
Kwaherini mpaka kipindi kingine tena nikija mjini tena,wapeni hai wale majamaa wavaa vibukta wakiwa na vi mackbook/laptop wanafanya kazi wakiwa night club, bado mpaka leo najiuliza huwa wanafanya kazi zipi nashindwa kupata majibu.
Kanachonga kucha?😁😁😂😂 wanaume wa Dar hawako serious![emoji23][emoji23] mwanaume kama huyu hata kufukuza paka hawezi
Mtu akiwa hana hela anaweza akakuamini aisee!
Jiulize kwanini waheshimiwa wanaenda dodoma na kurudi Dar?