Godwin peter
JF-Expert Member
- May 12, 2019
- 360
- 608
Leo nimekutana na kituko cha mwaka aisee, nilikuwa maeneo ya Sinza napata chakula cha mchana ghafla jamaa akaja na mtu anakibeg mgongoni akakaa kwenye kitu huku wakiangaliana.
Baada ya muda akanyoosha mguu na kuweka kisturi kidogo kilichokuwa pale si akaanza kumkata kucha na kumsugua miguu. Dah yaani nimejiuliza maswali mengi sana ni kwamba yeye hawezi kukata kucha na kusugua miguu yake mpaka aje mtu tena mwanaume amsugue miguu, mimi najua hizo ni tabia za wanawake sasa mwanaume kusuguliwa miguu na kucha wapi na wapi au ndo staili mpya hapa mjini sisi hatujui?
Ila wanaume wa Daslam Sinza mmezidi kwa kweli.