RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
💼 MHADHARA WA 6.
Habari ya leo wanaJF...
Kwenye mhadhara huu naomba kuzungumzia tabia ya wanaume wengi (wazawa) wa mikoa ya DAR ES SALAAM, LINDI, MTWARA, TANGA, PWANI na hata kule ZANZIBAR ambao kutwa wanashinda vijiweni bila kufanya kazi.
Vijana wengi wa hiyo mikoa wanashinda vijiweni siku nzima (kila siku) bila kufanya kazi wala kutafuta kazi huku baadhi wakiwa wamevaa mataulo na misuli kiunoni mchana kweupe. Baadhi ya vijiwe wamevipa majina fulani fulani vikiambatana na neno CAMP; kwa mfano unaweza kukuta hapo kijiweni kumeandikwa WATOTO WA MJINI CAMP, utawakuta wamelala, wengine wanacheza bao huku wanapulizwa na upepo wa miti au bahari.
Kilichopo hapo ni uvivu, kwasababu vijana utakaowakuta hapo huwa wanaketi vijiweni siku nzima, na muda wa chakula ukifika wanakwenda kula chakula kwa wazazi au kwa ndugu zao kisha wanarudi vijiweni kuendelea kupiga stori. Stori zinazozungumzwa hapo ni za siasa, uchawi, mapenzi, na lawama mbalimbali.
Hakika mikoa hiyo ina idadi kubwa sana ya vijana wavivu (wasiopenda kusoma, kufanya kazi wala kutafuta kazi). Unakuta kijana wa miaka isiyopungua 30 anaishi maisha ya "KULA KULALA" kwa mume wa dada (shemeji), na akiamka asubuhi anasubiri breakfast kutoka kwa wazazi au shemeji; baada ya hapo anakwenda kijiweni kupiga stori. Asset pekee anayomiliki ni smartphone ambayo amepewa na dada yake aliyenunuliwa simu mpya.
Tabia hiyo ya kushinda vijiweni bila kufanya kazi ni tofauti na mikoa mingine. Mikoa mingine ukikuta vijana wameketi vijiweni ni bodaboda wanasubiri abiria, na ukihesabu idadi ya vijana waliopo kijiweni ni sawa na idadi ya pikipiki zilizoegeshwa pembeni. Mikoa mingine hukuti vijana wameketi kijiweni bila channels za hela, na ukikuta vijana wapo kijiweni wana maduka yao pembeni.
BY: RIGHT MARKER-TZ
Mbezi Louis, Dar es Salaam.