Wanaume wa hii mikoa sita (6) acheni kukaa vijiweni bila kufanya kazi.

Nimemchukua rafiki yangu nikamtembeza karibia mji mzima wa Tanga , aone kama kuna waliokaa vijiwezi au wacheza bao .

Kazunguka mpaka kasema hamna kweli nimeamini ....Kila kijiwe basi kuna bodaboda wamepaki mpaka baiskeli ....Tumerudi jioni baada ya kutoka Raskazoni yaani inaenda usiku ndio unakuta vijiwe vina watu wanakunywa kahawa ni usiku tena .


Nimekaa nae Deepsea pale forodhani anaona watu wengi ndio wanaingiza mzigoni kuvua , namwambia huu ndio mda wavuvi kuingia kazi ndio kumekucha kwao 😀 😀
 
Wanaita ''ruza'' nimecheza sana , tena ujinga huo nimetemana nao hata kubet sitaki kujaribu ....Ukitoka hapo usiku aidha umepiga pesa au umepigwa .

Ugomvi kila siku , siku moja jamaa aliuliwa kisa sh. 50 mwaka 2000 .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…