Wanaume wa JF mnajishushia CV zenu kwa wadada. Kuweni real, acheni fake life

JF hapa ni mtandaoni; na mtandaoni (na pengine popote pale) akili za kuambiwa NI LAZIMA uchanganye na zako. Watu wengi waliofanikiwa (na wanaojielewa) mara nyingi huwa hawajitapi wala kujivuna. Nafahamu brothers na sisters wachache humu wako vizuri sana kimaisha lakini huwezi kuwasikia wakijinadi mafanikio yao popote pale. Ukiona mtu anajitapa hovyo chukulia hilo kama onyo kwako.

Naamini kuwa JF hapa kuna akina kaka na mabinti wanaojielewa sana kama utakuwa mvumilivu na wewe mwenyewe kuelewa unachotaka. Binafsi nimebahatika kupata binti wa pekee sana, msomi, mwenye pesa zake, rafiki na binadamu mwenye ubinadamu uliotukuka. Lakini imenichukua muda mrefu sana kuweza kumwelewa sawa sawa kwa sababu kama nilivyosema hapo juu, mtu mwenye uwezo na anayejielewa huwa hajitapi wala kujivuna. Mpaka siku naonana naye tulibaki tu tunatazamana na kushangaana. Na sasa tumekuwa marafiki wa kweli kabisa kabisa. Maajabu !!!

Jua kwanza unachokitafuta. Kisha uvumilie na usiwe na papara. Ikibidi mshirikishe Mungu kama uko siriazi. Lakini kama unatafuta mtu wa kugegedana naye basi uwe open kwa kila kiumbe utakachokikuta kwenye kokoro lako...na usilalamike !!!
 
Ila ni aibu sana mwanaume kujifanya una gari au nyumba while hauna.
Kukosa gari au nyumba sio uhalifu jamani tuweni real
 
Hahajaja
Kuna mganga yuko Msumbiji, anatibu kwa njia ya wasap.
Jamani waganga hawa wanaleta hekaheka mjini hapa
Huyo Jamaa wa arusha ulomsema mi namjua sana ana fix Hugo.aliniambia nimtumie account ya dola.daah nikamuambia me sitaki hela yako bna.
Tukakaa akajisahau akaniambia anaomba nimkopeshe elfu 50 nikamuambia anitumie account ya euro.
 
Samahani ndugu..ti wilayani mkalama, kwa m.k... singidani.
Ebu ngoja niishie hapa kwanza...
Naomba kujiwasilisha mimi mlume w.a.k.o. humu jf.....
 
Huyo Jamaa wa arusha ulomsema mi namjua sana ana fix Hugo.aliniambia nimtumie account ya dola.daah nikamuambia me sitaki hela yako bna.
Tukakaa akajisahau akaniambia anaomba nimkopeshe elfu 50 nikamuambia anitumie account ya euro.
Mkuu....
Kwahiyo umeamua kuja kunianika huku laivu...[emoji25] [emoji25] [emoji25] .
 
Mkuu umezungumza vyema sana,na ndio ukweli huo!
 
Kwanza kwa niaba ya wanaume wa JF tunashukuru kwa kuyaeleza haya yote!

Pili utuombe radhi kwa kutujumuisha na hao matapeli ulokutana nao

Tatu sio kila alieko JF anatafuta mahusiano ya kimapenzi na kingono awe me au ke

Mwisho mtu ametumia fake Id unawezaje kukurupuka na kuamini kila anachokuambia kuhusu yeye? Hapo wote mna matatizo yeye na ww pia!

Mahusiano ya kukutana mitandaoni sio ya kuamini sana but pia kuna watu wamekutana humu humu JF na wako vizuri mpka leo
 
Huyo Jamaa wa arusha ulomsema mi namjua sana ana fix Hugo.aliniambia nimtumie account ya dola.daah nikamuambia me sitaki hela yako bna.
Tukakaa akajisahau akaniambia anaomba nimkopeshe elfu 50 nikamuambia anitumie account ya euro.
Hahaaaaa usikute ni tapeli huyo. Mie Kuna wachuga Ana swagga hizo hizo. Eeeh
 
Wanaume ni vinara kwa umbeya had unashangaa walikosea jinsia, sijui mambo ya watu yanawahusu nini, girlfriend wake au mke atapata tabu sana
Afu unajua mwanaume kuwa mmbea ni kipaji kigumu sana.
Fake I'd ziko kibao na kila siku zinaibuka mpya.
Inabidi tuanze kukariri miandilo ya wanaotujia pm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…