Wanaume wa JF muwe mnatuma nauli mkitaka kuonana na warembo mwenzenu kanitia hasara!

Wanaume wa JF muwe mnatuma nauli mkitaka kuonana na warembo mwenzenu kanitia hasara!

Muzine

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2017
Posts
32,366
Reaction score
60,453
Bora tu niseme ukweli kuliko kudanganyanaa.

Kwanini nimesema mwanaume yeyote anaye hitaji kuonana na mimi lazima atume nauli.


MKASA
Kuna mkaka mmoja wa Jf ana I'd yake inaanzia kama ya kike alinifata pm anahitaji kuonana na mimi.
Mimi wala sikuwa na shobo naye akaniganda kama rubaa nakwambia ooh mara natoka Canada nitashuka kenyata airport mara sjui wapi nakuja Dodoma kikazi lazima nikuone Demiss.

Mimi kusikia hivyo nikaona huyu mtu wa maana bwanaa weee kumbe hamsini zangu zimefika chiii

Huyu mkaka baada ya kufika Dom tukawasiliana akasema niende town alafu si mnajua mm naishi huku Hombolo jamani.

Eeeh nikachukua bodaboda mpaka mjini gharama elf 20 nikalipa.
Kichwani nilivaa wigi limeshachambuka na upepo limekuwa kama vuzi la Escober.
Nikapitia saloon kwa Jesca mcharuko akanipaka make up mimi akanichana na wigi kwa sh elf 5. Jumla nimetumia elf 25 mpaka hapo.

Nikakaa hapo saloon nasubiria kuonana na Mwanajf asije akanikimbia nimeshajipodoa na kuupara mtoto nanukia marashi weee balaaa.

Wewe si akaingiza sababu kibaoo jaman nilikereka hapo alisema atarudisha nauli yangu ikabidi niende kulala kwenye geto la Jesca Maili mbili.

Kesho nikaamka nikaenda nane nane nikapanda Super baraka mpaka hombolo nikiwa na mawazo debee.
Jaman nilipata hasara yani hela yangu bado inaniuma mpaka leo.
Alafu huyo member alisema atanirudishia lakini wapi mpaka leo sijaona muamala ukisoma kiufupi hela yangu inaniuma yani ningenunua mchele si ningepata hata kilo kumi.

Kuanzia leo naomba mjue mimi naishi HOMBOLO village.

Mchanganuo wa nauli
Hombolo-Town Elfu 40,000 kwenda na kurudi.
Saloon - Elf10,000

Kama huna nauli basi uwe na gari ya kunifata nilipo sitaki usumbufu.

Onyo:
Sijalazimisha kuonana na mtu ila mkae mkijua habari ndo hiyooo.
Alafu mm sina kifua ukinifanyia kitu lazima niseme saivi kiufupi siwezi kuweka mambo rohoni nisije kufa na pressure.

Location: Ihumwa Machimboni.
 
Hahahahhahaha hata wewe sitaki hasara mimi loooh
Dada demiss hadi Mimi ndugu yako mdogo wako utanitoza na hela ya saloon?au hio sheria ni kwa Hawa Al watan mabazazi?
 
Back
Top Bottom