Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 11,258
- 20,386
Ndugu mleta mada na wanajamiiforum wengine naomba niwaeleze haya:-
Kabila la wasukuma ni jamii kubwa yenye mkusanyiko wa desturi ndogo ndogo nyingi sana kuanzia salamu, mavazi, Ngoma za asili n.k
Hizo desturi zinachangiwa zaidi na maeneo husika kwani wasukuma ( bhasuguma) wamegawanyika katika Makundi karibia Makundi matano ( 5 ) au sita ( 6) kwa Sasa ambayo ni:-
1. Wasukuma wa Mwanza
- Hawa shughuli zao kubwa ni uvuvi na kilimo pia ufugaji wa wastani. Hawavai shanga na bangili au sketi kwa wanaume. Ngoma Yao kubwa ya asili ni Bugobogobo na beni
2. Wasukuma wa Mkoa wa Geita, na maeneo ya Kahama.
_ Hawa hujulikana kama BHANANG'WERI ( watu wa magharibi). Ni wakulima na wavuvi pia wafugaji. Ni hodari kwa ushirikina na dawa za asili. Hawavai hereni, sketi, bangili au kusuka ( wanaume).
3. Wasukuma wa Mkoa wa Simiyu ( wilaya ya Bariadi, Itilima na maeneo ya wilaya ya Meatu) na maeneo ya wilaya za Bunda na Serengeti huko Mara.
Hawa hujulikana kama WANYANTUZU. Ni jamii jeuri sana ya kisukuma inayojidhatiti kwenye kilimo, biashara, uchimbaji madini. Ni jamii ya matajiri wengi na wanasiasa maarufu kama John Chenge, John Momose Cheyo, Kamani, Charles Kitwanga n.k
Hawavai bangili, hereni, sketi kwa wanaume.
4. Wasukuma wa Meatu ( Meyadu) hujulikana kama BHANAKIYA.
Ni jamii ya watu wapole kama wale wa Mwanza.
Baadhi huvaa hereni, sketi, bagili na shanga ( makoja na bhudodi) hasa wanaoishi maeneo ya Bukundi.
5. Wasukuma wa Kusini. hupatikana mkoa wa Tabora( BHADAKAMA). Hawa ni wasukuma wenye mchanganyiko wa jamii za Wanyamwezi, wasumbwa, watutsi, wakonongo n.k
- Hawa ni wafugaji na wakulima.
Wengi walihamia kutoka mikoa ya shinyanga, na Mwanza.
6. Wasukuma jamii ya kifugaji ( BHADIMI).
HITIMISHO
Mimi ni msukuma wa jamii ya wanyantuzu na wanakiya ( meyadu). Utamaduni wa kuvaa sketi, hereni, bangili n.k si wa jamii nzima ya wasukuma, ni sehemu tu ya baadhi ya desturi za jamii za kifugaji.
Atakeyesoma andiko hili ataelewa kwa undani. Hata Mimi nikiwaona hao wanaovaa vile nashangaa kama wewe ufanyavyo.

- Hawa ni wasukuma waishio mpakani mwa wilaya ya Meatu na wilaya za Hanang ( Manyara) ziwa Eyasi, Wilaya ya Iramba.
- Wana mwingiliano mkubwa na makabila ya Wataturu, Wanyiramba ( wajakazi wa wasukuma), Wahadzabe ( Bhahi) na Wadatooga.
Ni jamii ya watu wapole kama wale wa Mwanza.
Baadhi huvaa hereni, sketi, bagili na shanga ( makoja na bhudodi) hasa wanaoishi maeneo ya Bukundi.
5. Wasukuma wa Kusini. hupatikana mkoa wa Tabora( BHADAKAMA). Hawa ni wasukuma wenye mchanganyiko wa jamii za Wanyamwezi, wasumbwa, watutsi, wakonongo n.k
- Hawa ni wafugaji na wakulima.
Wengi walihamia kutoka mikoa ya shinyanga, na Mwanza.
6. Wasukuma jamii ya kifugaji ( BHADIMI).
- Hawa ndiyo jamii inayohama hama na kusambaa kwa Kasi kwenda mikoa ya Kusini mwa Tanzania na hata nchi jirani za Msumbiji na Zambia.
- Shughuli yao kubwa ni ufugaji wa ng'ombe.
- ni jamii jeuri na haribifu katika mazingira.
- Hawa ndiyo huvaa Sketi, hereni, bangili, mashuka na aghalabu Huwa na fimbo mkononi.
- Ni maarufu kwa desturi ya CHAGULAGA ( kupata mke kwa kuzidiana mwonekano na ujasiri).
- wanaishi Mikoa ya Tabora ( Nh'obhola), Dodoma ( wilaya za Bahi, Chemba, na Chamwino), Katavi, Singida ( Manyoni), Morogoro, Mbeya ( Usangu), Songwe, Pwani, Lindi na mkoa wa Ruvuma.
- Hawa ni wahamiaji katika mikoa hii.