Wanaume wa mkoani wanapoingia jijini

Wanaume wa mkoani wanapoingia jijini

Nikiwa mitaa Fulani hapa katika jiji linalotamaniwa na wengi hapa Tz.
Nikawasikia kinadada wakipiga story.

Dada wa kwanza;
Hii mvua jamani haitupi nafasi hata ya kupumua.!

Dada wa pili;
Shoga iache tu inyeshe, inaleta mishahara kutoka mikoani hiyo.!!

Dada wa kwanza;
Kwanini shosti?

Dada wa pili;
Shosti na we unakuwa kama shamba, hiyo inaleta pesa za mavuno kutoka mkoani.
Hao washamba wakishauza mazao yao huko wanajileta wenyewe.!

Dada wa kwanza;
Heheee, umeona eee!! Unamfungia ndani kumlea babu wee.!! Simbakizii hata nauli ya kwendea kwa bibikizee lake huko lisojua kuhendo.!

Dada wa pili;
Heheee, tena mletee na zawadi ya boxer, hapo ndo umemaliza kabisa hata iliyobaki m-pesa atakurushia.!!

Sasa hapo ndio nikapata kuelewa kumbe hiki ndo wanachofanyiwa wanaume wa mkoani wajapo hapa jinini.

Punguzeni ushamba hii ni Dsm, mtaua watoto wenu bure kwa njaa huko kwenu kwasababu ya ushamba wenu.
Kumbe hata boxer tu ni kivutio kikubwa sana kwenu.!!

Wadada wa Dar wakamueni pesa tu hamna namna.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji87] [emoji87] [emoji87]
 
Sasa mura chachandu ya nini sisi unashikiria pilipili mkono wa kushoto afu unakua unatafunia taratibu afu ndimu ni marufuku kutumia hizo wanatumia wanaume wa dar pekee

Umenichekesha Mura, hata kwenye mahindi hamuweki ndimu kama mjini dasalam!
 
Unawezaje kuifananisha arusha na dar we ni ki.azi kweli dar hii hii au dar ya Somalia?arusha bado sana labda kidogo mwanza inakua kwa kasi sana,yaani ukiwa angani arusha ilivyo utadhani moshi tu
Point of correction, Sijafananisha na SIWEZI kufananisha "Heaven na Hell"
Atleast kiazi kuliko Bash... we ni kilaza upende kusoma uelewe ndo u-comment.
 
Heshima pesa,hata uwe unakaa vijijini ukiwa na pesa mfukoni watajireta tu.Na siku zote anayejipitisha mbele ya wanaume ili aonekane, ndo mshamba koz anaweza akajipitisha na asichaguliwe.
 
Ngoja nimalize kupata mlo nakuja!!!
2c8be3382081f1ba330bb294302377ea.jpg
Hapo patakua tarime nakiona kichuli hicho ktk kibakulli[emoji14][emoji23][emoji3]
 
Back
Top Bottom