Wanaume wa siku hizi hawawezi kuongea

Wanaume wa siku hizi hawawezi kuongea

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Nilikuwa nasikia zamani wakati ndo tunakua,tunanukia umri wa kuanza kumjua mwanaume,wasichana wanatusimulia wanavyokuwa wanasafiri kwenye mabasi wanakaa sit moja na wakaka wanapiga stori za hapa na pale hadi mwisho wa safari,muda mwingine safari inaishia na matumaini mapya ya mahusiano,yaani unaingia nyumbani unafarijika na zile stories za mkaka yule na cha ajabu ndo mara ya kwanza kukutana ndani ya hilo basi

Siku hizi unaingia ndani ya basi, unabahatika unakaa na mkaka sit moja,safari inaanza,kituo cha kwanza,hamna kitu,cha pili,hamna kitu,cha tatu unajifanya kumuulizia sehemu fulani basi linafikapo SAA ngapi,anajibu tu bado SAA moja
Halafu anarudisha earphone masikioni,anacheza games

Mnakuwa mabubu mpaka mwisho wa safari

Huwa hamtutendei haki kwa kweli

Mkiwa kwenye usafiri hasa mrefu msijifanye bize sana,huwa tunapenda tupige story mbili tatu

Ubize wetu kwenye mabasi huwa ni kupretend tu ,anza mazungumzo uone kama hutajibiwa
 
Pole sana unakaa na walevi wa smartphone. Katika safari mimi huwa napiga sana story hata mtaani nikitokea maeneo ya watu wa rika langu lazima nikaribishwe nipige story mbili tatu.
Wewe ni mtam safarini aisee,unafika mwisho bila kujua
 
Kama itatokeaa Tena safarii usisite kunijuzaaa awamu hiii sitakuwaa mzembe pichaa linaanzaa naacha smart phone nimwendo wa story tu hakuna hata kipengele Cha wadhamini aseeee
 
Sasa mtu sikujui huni jui sasa tutapiga story za aina gani wakati sijui Karia yako na yangu bora ni ongeze sauti kwenye earphones zangu sitaki story za uwongo na mtu
Note Bene : nikiwa kwenye basi huwa nafanya hivyo ila sio kitaa
 
Pole sana kwa yaliyokukuta... Umeongea kwa uchungu sana... Huenda na wewe ulijifanya uko bize sana
 
Niliwahi safir na mdada from dm to mwanza yule dada ni mwanachuo SAut ila kashamaliza nahis maana ni muda tangu 2015, mi si muongeaji sana kama nitakutan na bubu mwenzangu labda niwe nimeshatia mavituz,kama kawaida kanuni ya kuanza maongezi ni salamu tu nikamsalimia ile morning pre-safari nilimuona huyu bila kumchangamkia tutafika mwanza hatujaongea hata maneno kumi maana muda mwing namuona anachati mara wasap mara sms mara insta ila sikubahatika kumuona akiingia jf nahis alikua mshamba haijui,

nikamchangamkia nikamletea story nying yani story inazaa story mpka tukazoena,nikawa namchomekea maneno nikamuona hana maneno,akawa na usingiz safari imenza kumchosha nikachukua shuka langu la kimasai nikamtandikia corridon ya basi akalala maana alikua anahitaj kujinyoosha

Watu nahis walijua kama tunajuana kumbe no akawa ameachana na simu katia kwenye mkoba tukazidsha story ,nilikua na begi flan portable nimelipakata akalalia pale, niliwaza nimletee pigo za mapenzi zaid nikakumbuka nina wangu nikakausha
 
Sasa mtu sikujui huni jui sasa tutapiga story za aina gani wakati sijui Karia yako na yangu bora ni ongeze sauti kwenye earphones zangu sitaki story za uwongo na mtu
Note Bene : nikiwa kwenye basi huwa nafanya hivyo ila sio kitaa
Kujuana na mtu mpka iweje kwan au mpka umpelkee barua ya maombi ya urafiki?,ukishasalimiana na mtu ndo mshajuana kwa kanuni zetu wanadamu, au uanataka mpka umvue nguo ndo umjue, we juana nae kibinadamu piga nae story za kawaida atajua mwenyewe kama ye ni wazir,polisi,jambazi ,maana ukijua ivo kabla unaweza usizoeane na mtu hat kidogo,
 
Nilikuwa nasikia zamani wakati ndo tunakua,tunanukia umri wa kuanza kumjua mwanaume,wasichana wanatusimulia wanavyokuwa wanasafiri kwenye mabasi wanakaa sit moja na wakaka wanapiga stori za hapa na pale hadi mwisho wa safari,muda mwingine safari inaishia na matumaini mapya ya mahusiano,yaani unaingia nyumbani unafarijika na zile stories za mkaka yule na cha ajabu ndo mara ya kwanza kukutana ndani ya hilo basi

Siku hizi unaingia ndani ya basi, unabahatika unakaa na mkaka sit moja,safari inaanza,kituo cha kwanza,hamna kitu,cha pili,hamna kitu,cha tatu unajifanya kumuulizia sehemu fulani basi linafikapo SAA ngapi,anajibu tu bado SAA moja
Halafu anarudisha earphone masikioni,anacheza games

Mnakuwa mabubu mpaka mwisho wa safari

Huwa hamtutendei haki kwa kweli

Mkiwa kwenye usafiri hasa mrefu msijifanye bize sana,huwa tunapenda tupige story mbili tatu

Ubize wetu kwenye mabasi huwa ni kupretend tu ,anza mazungumzo uone kama hutajibiwa
Wadada wa zamani awakuwa na njaa kama nyinyi mkisalimiwa tu mnapiga mzinga mnazani mmepata buzi na wakaka wa zamani hawakuwa na Pesa hivyo walitegemea mdomo
 
Mwisho wa siku mnatupa maneno ya shombo kama haya.

Screenshot_20190819-212018.jpeg
 
Back
Top Bottom