Wanaume waficha Wallet/pesa wakifika home.why?

Wanaume waficha Wallet/pesa wakifika home.why?

midada wana tabia ya kusachi pochi na kujitwalia vijisentsn kimya kimya ukiuliza wanadai labda umepoteza bar,kumbe wameshachakachua bora kuacha kwenye gari kama unalo
 
Mmmhh ndoa hizi, wakati mwingine sipati mzuka kabisa wakuolewa. Bora mapenzi tu ya urafiki. hao wanaue ni wachoyo na pengine wanawakuwapa huko nje
 
Tatizo wanawake hawajui kama kuna kesho wanataka kutumia pesa yote leo kwa matumizi yasiyo na tija. Tunaficha hizo pesa ili zitumike kesho. Mwanamke anaweza taka kutumia pesa zote leo na kesho akataka pesa nyingine

Kwa nini msianze na kuwapa matumizi ya wiki ili apange mwenyewe? Mimi kwa kweli hata mie sipendi biashara ya kuombana hela kila asubuhi (kama uwezo wa wiki upo). Mambo ya kukimbizana khanga zinatudondoka tunaomba hela za mboga jamani? Na kwa nini wakati mwingi muwe na mawazo kuwa akina mama wanaongeza matumizi wakiona uzito wa hizo wallet? Mimi ninavyojua wakati mwingi akina mama wanapanga matumizi kutokana na pesa uliyompa, kama umebana ukaacha elfu moja, basi ataweka maharage pekee. Lakini ukiacha elfu mbili si utakuta na mboga ya majani angalau na tunda pembeni? Mmeshawahi kurudi nyumbani mkakuta hakuna chakula kwa sababu pesa uliyoacha ni kidogo? Au utakuta chakula kutokana na pesa iliyoachwa? Na mara nyingi mnaacha pesa ya bajeti pasua kichwa, na mbishe. Kisa ukiacha nyingi atabana ya saloon. Na ya saloon je umemuachia? Jamani familia is a package!
 
wengine wana tabia zao za ubinafsi na uchoyo uliokidhir ,...kama mnakaa kama familia na kujadili mambo yenu saa ngapi utakuwa nahuo muda wa kufunika funika mifuko.....wanaume wa sampuli hii wachunguze hata matumizi ya nyumba zao kutoa ni tabu mwaka mzima hajui hata mke anaishije kama ana kipato kidogo au hana kabisa ni kuzengea za mke,huku yeye akitegea majukukumu......... no wonder ndio maana wengine wanaishia kula vya haramu katoa hela jumaaaaaaaaa ,waja jion wakuta nyama unachekelea usiku umeficha wallet shame on you badilikeni huo ubinafsi una malipo yake.
 
Kwa nini msianze na kuwapa matumizi ya wiki ili apange mwenyewe? Mimi kwa kweli hata mie sipendi biashara ya kuombana hela kila asubuhi (kama uwezo wa wiki upo). Mambo ya kukimbizana khanga zinatudondoka tunaomba hela za mboga jamani? Na kwa nini wakati mwingi muwe na mawazo kuwa akina mama wanaongeza matumizi wakiona uzito wa hizo wallet? Mimi ninavyojua wakati mwingi akina mama wanapanga matumizi kutokana na pesa uliyompa, kama umebana ukaacha elfu moja, basi ataweka maharage pekee. Lakini ukiacha elfu moja si utakuta na mboga ya majani angalau na tunda pembeni? Mmeshawahi kurudi nyumbani mkakuta hakuna chakula kwa sababu pesa uliyoacha ni kidogo? Au utakuta chakula kutokana na pesa iliyoachwa? Na mara nyingi mnaacha pesa ya bajeti pasua kichwa, na mbishe. Kisa ukiacha nyingi atabana ya saloon. Na ya saloon je umemuachia? Jamani familia is a package!

Familia ikiwa na lengo moja mambo haya hayawezi tokea. Wanawake wajione ni sehemu ya familia na wanawajibu wa kuiendeleza familia. Changamoto za ndoa zinawaumiza sana wanaume na ndio maana tunakufa mapema na kuwaacha. Jaribuni kutupunguzia presha za maisha jamani
 
Inauma sana endapo mwanaume huo ambaye hatoi pesa za kutosha kwa matumizi ya nyumbani lakini kila ukifua unakuta bill za beer na nyama choma si chini ya elfu hamsini.
 
Wanawake wengine ni wafujaji wa pesa na ndio maana wanafanyiwa hivyo.
 
Jamani wanwake hawana budget kabisa.... anaomba pesa afanyie A..B...C ukimpa hiyo pesa atafanya A then D.. E...F. Kwa kifupi plan zao zinakuja baadae baada ya kupewa hiyo cash.
 
wewe unaionekana utakuwa mjinga fulani hivi....zuzu hivi....unapoteza muda? ndio maana unakuja na thread za kishwaini asubuhi asubuhi...shame on u....
.....na mtakuwa watumwa wa wakenya na wahindi mpaka muote sugu makalioni....pambafu kabisa.....

mhh mzee mbona umechukua neno moja ume conclude kabisa na kutukana? hatari hiyo Yo Yo!!
 
Mmmhh ndoa hizi, wakati mwingine sipati mzuka kabisa wakuolewa. Bora mapenzi tu ya urafiki. hao wanaue ni wachoyo na pengine wanawakuwapa huko nje

Kweli sababu za kuwa single ni nyingi sana.., na mapungufu ya wanaume ni mengi, lakini hili sidhani kama ni tabia ya wengi..
 
Hebu pata picha hii.....
Umetoka kazini umechoka ni kati kati ya mwezi una kiasi fulani cha hela kidogo tu cha kukuwezesha kuishi mpaka utakapo pata hela ya kutosha.Huna hela nyingine na wala si kwamba una matumizi ya ulevi etc.

Unaamka asubuhi unakwenda kazini mara unaamua kununua mahitaji ya nyumbani na kucheki unakuta kuna hela ndogo sana, unadhani umeibiwa, kumpigia mama anakuambia alikuta hela amechukuwa na kuwatumia baba na mama, au ametumia tu kwa maytumizi yake yeye ambayo hakukuambia. Mara kusuka, saloon, nilichukua nguo, na mengine mengi tu...

Sasa unafikiria itakuwaje , mtaishije mpaka utakapo pata hizo hela unazotegema??

Je nani anataka pressure za namna hii....

Lakini hapa kama ungekuwa umeficha wallet yako ... ahaaa wala hizi pressure za kujitakia usigepata na usawa wenyewe huu.

Mimi naona lengo kwa kina baba wengi kufanya hivi sio baya, ni katika kuweza ku control matumizi tu!
 
Naona bibie unagusia mambo ikulu,hii ni hatari sana iwapo wapo watu wa namna hiyo. Mmeoana na kuwa mwili mmoja. I wapi dhana ya mwili mmoja ktk hali ya namna hiyo?
 
Naona bibie unagusia mambo ikulu,hii ni hatari sana iwapo wapo watu wa namna hiyo. Mmeoana na kuwa mwili mmoja. I wapi dhana ya mwili mmoja ktk hali ya namna hiyo?

Ndio hivyo watu wanaficha ficha utadhani wako na machangu
 
Hebu pata picha hii.....
Umetoka kazini umechoka ni kati kati ya mwezi una kiasi fulani cha hela kidogo tu cha kukuwezesha kuishi mpaka utakapo pata hela ya kutosha.Huna hela nyingine na wala si kwamba una matumizi ya ulevi etc.

Unaamka asubuhi unakwenda kazini mara unaamua kununua mahitaji ya nyumbani na kucheki unakuta kuna hela ndogo sana, unadhani umeibiwa, kumpigia mama anakuambia alikuta hela amechukuwa na kuwatumia baba na mama, au ametumia tu kwa maytumizi yake yeye ambayo hakukuambia. Mara kusuka, saloon, nilichukua nguo, na mengine mengi tu...

Sasa unafikiria itakuwaje , mtaishije mpaka utakapo pata hizo hela unazotegema??

Je nani anataka pressure za namna hii....

Lakini hapa kama ungekuwa umeficha wallet yako ... ahaaa wala hizi pressure za kujitakia usigepata na usawa wenyewe huu.

Mimi naona lengo kwa kina baba wengi kufanya hivi sio baya, ni katika kuweza ku control matumizi tu!

Kwa hiyo ndio unajifanya unaweka pesa kidogo kwa dressing table zingine unazisweka chini ya kapeti looo nani kakwambia! nyumba yoote huwezi kuficha kitu mwanamke asikione. Halafu mwanaume anajidanganya mkewe kalala, hakuna mwanamke analala kabla mumewe hajaingia ndani anapata mang'amung'amu tu, akisikia gari au mlango ndio anajifanya amelala
 
wewe unaionekana utakuwa mjinga fulani hivi....zuzu hivi....unapoteza muda? ndio maana unakuja na thread za kishwaini asubuhi asubuhi...shame on u....
.....na mtakuwa watumwa wa wakenya na wahindi mpaka muote sugu makalioni....pambafu kabisa.....

Yoyo samahani naona post imekugusa pole sana kwa kuficha wallet ila jifunze kubadilika uwe unapanga matumizi na mkeo sio unahangaika kuficha ficha mwishowe unasahau ulipoficha asubuhi unaanza kumwambia tena akusaidie kutafuta
 
Kuna rafiki yangu moja ana b/case kwa hiyo vitu vyote nyeti pamoja na pesa kila akirudi huwa anafifadhi pale na kufunga kwa namba.
Siku moja alisafiri safari ya wiki moja. Mama alitafuta mtaalamu wa kufungua hiyo b/case. Alipofanikiwa kuifungua alikuta pesa na barua zingine za siri zilizosababisha ndoa kuvunjika baada ya njemba kurudi.
 
kapos kama izi wanakuwa wameopoana kwenye baa ama!?
Spati picha aisee.
Wako very discent hao wadada na wana kazi zao nzuri na heshima zao sana tu kuliko unavyofikiri. Olewa dada wewe uyaone
 
Ndoa za siku hizi zina mambo sana. Wanawake wamekuwa hawatabiriki kabisa. Anafanya kazi nawe unafanya kazi ila hela yake huioni. Utasikia tu hana hela baadae unastuka kumbe anamjengea mama yake kwao na nyie hata kiwanja hamna

Anafanya kazi na anapomuomba kumbuka wanachangia sometimes, ila jamaa bado anataka kuficha za kwake akaweke heshima bar
 
Natmani nimpate mume wa kuficha pesa zake alafu, nikimchabo tu!! Imekula kwake na lazima ajute kwani mie ndio nitakua nampa kama ni ya matumizi au nauli. Au simpi kabisaaaa!!!! kwa uzembe wake.Ila nitamuambia nimeokota wallet so usinipe pesa ya matumizi mpaka nitakapo kuambia.:clap2:

Avatar yako inanitisha!!!
 
Hebu pata picha hii.....
Umetoka kazini umechoka ni kati kati ya mwezi una kiasi fulani cha hela kidogo tu cha kukuwezesha kuishi mpaka utakapo pata hela ya kutosha.Huna hela nyingine na wala si kwamba una matumizi ya ulevi etc.

Unaamka asubuhi unakwenda kazini mara unaamua kununua mahitaji ya nyumbani na kucheki unakuta kuna hela ndogo sana, unadhani umeibiwa, kumpigia mama anakuambia alikuta hela amechukuwa na kuwatumia baba na mama, au ametumia tu kwa maytumizi yake yeye ambayo hakukuambia. Mara kusuka, saloon, nilichukua nguo, na mengine mengi tu...

Sasa unafikiria itakuwaje , mtaishije mpaka utakapo pata hizo hela unazotegema??

Je nani anataka pressure za namna hii....

Lakini hapa kama ungekuwa umeficha wallet yako ... ahaaa wala hizi pressure za kujitakia usigepata na usawa wenyewe huu.

Mimi naona lengo kwa kina baba wengi kufanya hivi sio baya, ni katika kuweza ku control matumizi tu!

Nakubaliana nawe. La pili ni kwamba takribani wanawake wengi wanatumia vizuri hela zao lakini siyo za wengine/waume zao. Kwa wale waliooa wanaweza kulibaini hilo. Mwanamke anatamani sana kutumia hela za mume wake badala ya kutumia hela za kwake. Hata ukisoma posts kama 3 humu utaona ....oh kesho nitamwomba mume matumizi...., nitamwambia nunua hiki...n.k. Hii yote ni mfumo dume ambao umetawala ndani ya jamii na familia kwa ujumla. Wanawake wanajikuta wakitumia opportunity ya kuwa mke kudai kila kitu kutoka kwa mume na hapa ndipo weakness yao inaonekana.

In this case, wanaume wakigundua hilo, na ili waweze kubana matumizi ya fedha yake, analazimika kuficha ili apange matumizi vizuri lakini haina maana (haijasemwa) kwamba anamnyima matumizi mkewe. Na kwa kuwa Mtoa mada ameongeza kuwa madada hao wana kazi zao, utagundua kuwa kuna tatizo la dada husika kutoshiriki kutoa fedha za matumizi hapo nyumbani.
 
Back
Top Bottom