Wanaume waliosoma seminari

Wanaume waliosoma seminari

#Bree ven kwa kweli we seminarians ni wanaume bora kabisa. Mti wa matunda daima hupigwa mawe. Kama umempata mseminaristi mshike kama lulu iyojificha shambani.
 
Sisi tuliopitia seminari lakini hatukufanikiwa Kuwa mapadri tunajulikana kama mapadri kivuli.
Mimi nilisoma bihawana Junior seminary Dodoma,
Kiukweli wengi tuliopitia seminari na kutokuwa mapadri Ni watu waaminifu sana na tunaojua kutunza siri, wote ni watu tunaomjua Mungu na kumuamini wote ni mababa bora, wanaojali Sana familia, Ila ni watu ambao hawapendi ujingaujinga, uongouongo na mambo kama hayo.
Ndio maana hata TISS wanawapa upendeleo kwenye ajira.
Wengi wetu ni wazito sana kufukuzia mademu hatunauvumilivu wa kumsikilizia demu na zilesitaki na taka.
Mimi binafsi hapa sina demu kama kuna mdada atataka Kuwa na padri kivuli kama mimi mchakarikaji na muajiriwa serikalini anakaribishwa naishi dsm
Kila la kheri Padri kivuli mwenzangu.
 
Hawapendagi ujinga.kazi tu.si unaona magufuli
Wana maadili ya dini(chrístianity) pía maadili ya jamii, wako committed kwenye kazi zao na wako serious kwenye mambo ya msingi,ni wepesi kutambua tabia ya mtu wamesomea psychology
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] hapo kwenye usinitch... yamkini ni kwa sababu shule hizo ni singo sana.
Hapana mkuu labda ni 2% ndo masnitch ila wengi wao ni watu wa kutunza sana siri na kujali hisia za wenzao na hata umfanye vip ni wagumu kuchongea wenzao. Sababu kubwa ya wao kuwa na msimamo ni pamoja na aina ya malezi na kusudio lao la kusoma kwamba wale wanasoma kwa lengo la kuwa padre na si vinginevyo na hivyo misimamo kwao ndio kigezo chao. Nina mengi kuhusu wao ila wacha niishie hapa nitaendelea kuchangia kadiri ya hoja zitakapokuwa zinatolewa.
 
Wanaume waliosoma seminary Kwanzaa ni waaminifu na watiii, huwa Wacha mungu kutokana na misingi waliokulia, pia ni wachapa kazi Sana sio watu legelege,, watu wanaopenda kumsikiliza mtu kwa umakini
 
Wana maadili ya dini(chrístianity) pía maadili ya jamii, wako committed kwenye kazi zao na wako serious kwenye mambo ya msingi,ni wepesi kutambua tabia ya mtu wamesomea psychology
psychology wanasoma wale walioenda major seminary(seminary kuu) baada ya kumaliza form 6 na kufaulu, waliopo mtaani wengi ni wale walioishia junior seminary ( kidato cha 1-6).
 
Wanaume waliosoma seminary Kwanzaa ni waaminifu na watiii, huwa Wacha mungu kutokana na misingi waliokulia, pia ni wachapa kazi Sana sio watu legelege,, watu wanaopenda kumsikiliza mtu kwa umakini

Kwenye mapenzi ni hatariii zaidi ya kobraa kila akipata kuonja mpya hurukwa na akili yaani anakimbia na kuhamia huko completely, akionya mpya tena hivyo hivyo, akiona shape, ziwa jipya yaaani zinamruka ukiwa naye jipange, akipata mpya tu kesho yake hunaye tena.
 
Nenda uendako mtu yeyote aliyesoma seminari hata awe mhuni vipi hawezi kuwa,katili wana hofu ya Mungu.
Atafanya ubaya vyovyote vile ila mwisho huomba msamaha.
Zamani waliopitia seminari waliipata kazi bila kupitia interview.
Mwanafunzi akivuka form two seminari hawezi fukuzwa kirahisi ni hatua mkubwa.
Misa masaa 24 hadi magoti yanaota sugu.
mkuu utakuwa mseminari nini mbona mulemule????
 
Back
Top Bottom