tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Siku hizi ni kawaida kumkuta mwanaume amevaa cheni shingoni au hereni masikioni. Tena utamkuta mwanaume mwenye akili zilizotimia (achilia mbali mateja) amevaa hereni na cheni kubwa huku akijiona mjanja! Huu ni ujanja au ni dalili za kukengeuka?
Tangu dunia hii ilipoumbwa, inajulikana kwamba urembo ni kwa ajili ya wanawake. Mwanaume hata ukiwa rafu ni pouwa tu--hakuna mtu atakayekushangaa, tofauti na ilivyo kwa wanawake. Mwanamke ni kiumbe anayejisikia kuonekana nadhifu na mrembo nyakati zote. Hivyo hupenda kuvaa vifaa vya urembo kama vile hereni, mikufu, pete, vidani, bangili, nk. Sasa wale wanaume wanaovaa vifaa hivi vya KIKE tuwaweke fungu gani? Si wavae na sketi kabisa ili tujue moja?
Kwa kweli wanaume wenzangu wanaovaa pete, hereni na mikufu wananiudhi sana. Mimi siwezi hata kuvaa saa kwa kuwa inanifanya nijihisi nimevaa bangili! Sasa iweje wanaume na ndevu zao watamani kuvaa urembo wa kike?
Naomba tujadiliane BILA JAZBA hadi jibu lipatikane. Samahani sana, najua hata humu JF wavaa hereni wamo.