Wanaume wanaovaa cheni na hereni wanataka nini?

Wanaume wanaovaa cheni na hereni wanataka nini?

Babashopu unaenda huendi, au hata saluni basi unaendaga? Ukifika huko bila shaka huwa unamwambia huyo kinyozi wako jinsi gani akunyoe sio, ni kwa nini basi unachagua mtindo wakati wewe mwanaume... kwa nini usitenge tu hilo bichwa lako kama kifuu... lol.

mkuu, mimi sijakuzuia kuvaa hereni, mkufu na vikuku. ukipenda hata SHANGA vaa tu.

kufananisha kukata nywele na mavazi ni vitu viwili tofauti. na kama unadhani kunyoa nywele ni fasheni kama kuvaa hereni, mbona hujawahi kusuka nywele zako au kupaka wanja? kwani kusuka na kupaka wanja sio fasheni?
 
ni upungufu wa kisaikolojia hivyo hutaka kufidia na vitu kama hivyo. utanashati kwa mwanaume ni muhimu lakini isiwe too much! unamkuta mtu kavaa cheap jewerls kibao, cheap perfumes mpaka anakera na vikolombwezo kibao
 
Kweli kabisa hereni na kata K tuwasubiri wengine watasemaje hapo maana sie zetu ni cheni za kiume tu tena kama mimi silver tu

mkuu, usitake kuhalalisha ujinga kwa kusema CHENI ZA KIUME. mbona hakuna sketi na shanga za kiume? ina maana urembo au vazi lolote likiitwa la kiume hata kama uasili wake hauko hivyo wewe unashobokea tu? basi waambieni watengeneza urembo wakutengenezee SHANGA ZA KIUME ukavae kiunoni.
 
hawa bongo (fleva+muvi) mwanaume mzima na ndevu zake anapaka poda mpaka na rangi ya midomo inang'aa.
tutaona mengi "hata mbuyu uliaza kama mchicha"
 
mleta mada sijui unaishi wapi dunia hii ya sasa,kuvaa cheni unaona dhambi?bora hata hereni cheni!enzi hizi za insta na fcbk we bado uko enzi za ujima aisee,yaani kwakweli nyie ndio watu ambao mnatakiwa kurudishwa kwenu huko vijijini mlikotoroka mkaendelea kulima viazi.
maana kwa mtu kama wewe huna faida ya kuishi mjini kama sio duniani kabisa.kha
 
mleta mada sijui unaishi wapi dunia hii ya sasa,kuvaa cheni unaona dhambi?bora hata hereni cheni!enzi hizi za insta na fcbk we bado uko enzi za ujima aisee,yaani kwakweli nyie ndio watu ambao mnatakiwa kurudishwa kwenu huko vijijini mlikotoroka mkaendelea kulima viazi.
maana kwa mtu kama wewe huna faida ya kuishi mjini kama sio duniani kabisa.kha

bado hujajibu hoja. kuna umuhimu au maana gani wanaume kuvaa mikufu na hereni? ni ili waonekane wa KISASA? ili iweje?
 
Dah! Hata saa mkuu tpaul?

Hereni nakuelewa! Ila saa na mkufu naona umecomplicate sana.
 
Last edited by a moderator:
Sidhan kama cheni ina shida..mkuu labda huna hela ya kununua silver useme!!
 
kwenye cheni sikubaliani na mtoa uzi hata kidogo!tuache ushamba!
 
Niwe mkweli saa yangu mkononi saa nzuri ya 200k au 300k , cheni yangu ya silver nyembamba isiyokua na kidani na visuruali vyangu kadet na vishati vyangu vya kunienea na sio oversize na ichwani nywele zangu fupi na kwenye kidevu hakuna ndevu huku kucha za mikono zikiwa fupi na nina nukia utuli ndo hua navaa halafu leo uhamasishe niache kuvaa cheni?? Whaaaat shit is this

It seems that ua always shinning,Big Up mkuu,huyu jamaa labda angeongelea tu hereni lkn hata cheni na pete?
 
Siku hizi ni kawaida kumkuta mwanaume amevaa cheni shingoni au hereni masikioni. Tena utamkuta mwanaume mwenye akili zilizotimia (achilia mbali mateja) amevaa hereni na cheni kubwa huku akijiona mjanja! Huu ni ujanja au ni dalili za kukengeuka?

Tangu dunia hii ilipoumbwa, inajulikana kwamba urembo ni kwa ajili ya wanawake. Mwanaume hata ukiwa rafu ni pouwa tu--hakuna mtu atakayekushangaa, tofauti na ilivyo kwa wanawake. Mwanamke ni kiumbe anayejisikia kuonekana nadhifu na mrembo nyakati zote. Hivyo hupenda kuvaa vifaa vya urembo kama vile hereni, mikufu, pete, vidani, bangili, nk. Sasa wale wanaume wanaovaa vifaa hivi vya KIKE tuwaweke fungu gani? Si wavae na sketi kabisa ili tujue moja?

Kwa kweli wanaume wenzangu wanaovaa pete, hereni na mikufu wananiudhi sana. Mimi siwezi hata kuvaa saa kwa kuwa inanifanya nijihisi nimevaa bangili! Sasa iweje wanaume na ndevu zao watamani kuvaa urembo wa kike?

Naomba tujadiliane BILA JAZBA hadi jibu lipatikane. Samahani sana, najua hata humu JF wavaa hereni wamo.

Mh,kwenye hereni sawa ila hata cheni? Na pete? Je zile za harusi na engagement ring? We umezidi ubandidu mkuu...TOKELEZEA...
 
Back
Top Bottom