Wanaume wanaovaa cheni na hereni wanataka nini?

Wanaume wanaovaa cheni na hereni wanataka nini?

Babu zako wamevua mikufu !!!!!????
Masikio wameziba na nini au wamekunjia juu!!!????
Morani hawasuki tena??????

Sidai?????!!!!!!

Hii ni hoja dhaifu sana--huwezi kufananisha mavazi ya kitamaduni na uvaaji wa hareni na shanga (kiunoni) kwa wanaume. Wamasai na makabaila mengine ya wafugaji wamekuwa wakisuka rasta tangu zama za kale. Huwezi kutumia kigezo hicho dhaifu kuhalalisha ukengeufu wa kuvaa chachandu na hereni kwa wanaume. Mimi swali langu ninalouliza ni kwamba WANAUME HUVAA HERENI, SHANGA NA MIKUFU ILI IWEJE? Je, wasipovaa watakosa nini ambacho wanakifaidi pindi wakivaa vifaa hivi vya KIKE? Swali langu ni rahisi sana--sijui kwanini unarefusha hii mada kwa kuuzunguka mbuyu.
 
Mmh nguvu ya mwanamme bwana kumfuko sio swaga za cheni na mikufu sasa tutatofautiana kweli jamani mimi napenda mwanamme smart shati au tshirt jeans nzuri ila kaunda suit kaaa pembeni sio type yangu swaga za mavazi sio ma chain imehusu
 
Na kunawanaume wanatetea hapa kwenye huu uzi..mm nlikua nafanya kazi sekta ya afya bongo mjini posta hapo..nlikua nikiona akija mshkaji gentleman na mabrazamen..hata uelewa wa mambo ni tofauti, lkn hata aina ya shida zao ni tofauti..lkn mademu wanawafagilia sana ndo nashangaa..yaani unakuta mtu yupo na mtu anavaa vichupa chupa tu mpaka najiuliza inakuaje..ila ndo ukipita kwenye mitandao hata hapa wanawake wanalalamika wanaime hawawezi kazi na nini..ila unakuta wanadate na wavaa cheni na wavaa hereni

nawashangaa hawa wanaume wanaotetea huu upumbavu. ukiona mwanaume anafagilia hivi vitu mara nyingi anakuwa na shida flani. nishakuwa na mmoja mpenda cheni sana, mengine alikuwa hafanyi naona alikuwa anaona aibu kulingana na status yake mjini. akijitahidi saaaaana ni viwili tena baada ya kupumzika kama saa mbili hivi.
 
nikute asubuhi naenda zangu mishe,nna shati ya mikono mirefu nimeikunja mapindo mawili,mkono wa kushoto nna ORLANDO inayoelekea black afu inang'aa,suruali yangu ya heshima chini nna zara afu nanukia ambition.dah semeni tu saa siachi kuvaa.
Tyta angetuwekea picha...kwa mfano una kutana na mwanaume kavaa sa nyekundu, pink, sijui blue na wengine siku hizi akivaa saa nyekundu na nguo nyekundu... Hayo mambo ya wanawake bana acheni
 
Pokea LIKE zangu za dhati dada Mrembo by Nature. Nawashangaa sana wanaume hawa, kama vipi wafanye surgery wawekewe matiti wavae brassier na pia wachongewe viuno vya kike wakavae shanga. Eti watu wanahalalisha upumbavu kwa kisingizio cha USASA! Hata tabia za kishoga zilianza hivi na hatimaye sasa ushoga linaonekana ni jambo la KISASA hapa nchini. Wale mnaotaka usasa kwanini msiingia kwenye ushoga ili muwe wa kisasa zaidi?

kila kitu chini ya mwavuli wa usasa...hii ni kazi kweli kweli. wanawafanya wadogo zetu wanapotea kisa kuiga mitabia yao ya ajabu. kama unavaa hereni, unaweka nywele dawa, unatinda nyusi, unapaka poda, lipstick, cheni n.k kwa kigezo cha kuvutia jua kuna siku utavaa pedo kama ommy dimpo ili tuyaone maungo yako. na kifuatacho itv ........unakijua.
 
Last edited by a moderator:
nawashangaa hawa wanaume wanaotetea huu upumbavu. ukiona mwanaume anafagilia hivi vitu mara nyingi anakuwa na shida flani. nishakuwa na mmoja mpenda cheni sana, mengine alikuwa hafanyi naona alikuwa anaona aibu kulingana na status yake mjini. akijitahidi saaaaana ni viwili tena baada ya kupumzika kama saa mbili hivi.
Ni kweli Mrembo by Nature...wasichana wengi hawajui mara nyingi watu kama hawa psychologicaly wanakuwa unstable labda pia na low self esteem sasa ili kucompasate ndo inabidi mtu aongezee micheni cheni, mapete nk..na unakuta wengine hata chakula hali vzr hela kaenda kununua mkufu na mipete ya gharama(kwa mwanaume haifai)
 
Hii ni hoja dhaifu sana--huwezi kufananisha mavazi ya kitamaduni na uvaaji wa hareni na shanga (kiunoni) kwa wanaume. Wamasai na makabaila mengine ya wafugaji wamekuwa wakisuka rasta tangu zama za kale. Huwezi kutumia kigezo hicho dhaifu kuhalalisha ukengeufu wa kuvaa chachandu na hereni kwa wanaume. Mimi swali langu ninalouliza ni kwamba WANAUME HUVAA HERENI, SHANGA NA MIKUFU ILI IWEJE? Je, wasipovaa watakosa nini ambacho wanakifaidi pindi wakivaa vifaa hivi vya KIKE? Swali langu ni rahisi sana--sijui kwanini unarefusha hii mada kwa kuuzunguka mbuyu.
Ndo maana mm naona watu wanakimbia mzizi wa uzi yaani wanataka sema diamond au hemed phd akivaa hereni au mkufu au saa ya rangi ya pink kwa mfano..labda na kuweka nyele rangi na kupaka lipshin wanaendeleza utamaduni..au wanawaiga singa singa..! Basi bongo vijana tuna serious problem kwenye namna ya kuderive maono yetu ya maisha.!!!
 
Kuva pete ya dhahabu iliyochongwa herufi ya jina..ili upendeze hii ni hulka ya wanawake..mwanaume kiasili anatakiwa apendeze jinsi alivyo ikianza kuongeza vitu vilivyoo kaa kwa mlengo wa kike zaidi ni kuanza kuvuka mpaka kwenda upande wa pili..lkn pia pete ya ndoa haivaliwi ili upendeze unaivaa kama sign na ni wajbu kuivaa..hata mantiki yake ya kuivaa ni tofauti na mantiki ya kuvaa ili upendeze na km wangine walivyosema ili kuwa sexy..

Pete ni pete tu iwe ya ndoa au ya talaka zote ni symbol na hupewa maana na jamii au wahusika tu sio lazima ukisema ya ndoa ndio ionekane ya maana au useme ya rozari sijui ukienda kwa sonara utanunua pete hiyo maana utaweka wewe!!!!!!!

Tunaongelea Afrika hapa hebu nipe mfano wa kabila linalosema watu wakioana wavae pete ya ndoa!!!!!

Hayo ya kupendeza ni social constructionism ndio maana wamakonde walijichora usoni,wamasai wakatoboa masikio, wazungu na latinos wao tatoo sasa hapo unaona kupendeza ilivyo tata?????!!
Hili la kuoendeza tukijaaliwa tuliwekee uzi wake hapa litaua mada hii
 
Sasa mkuu mbona kama unasema jinsi mtoa mada alivyomaanisha..pete ya ndoa ikivaliwa kwenye jamii inajulikana ni ya ndoa na inapewa tafsiri yake..ila mwanaume akivaa mipete huku na huku kama hadija kopa..inabidi kuangalia vzr...mmasai akitoboa maskio inaeleweka kwenye jamii duniani kote...ila diamond au hemedphd akitoboa maskio na kuvaa hereni herebi ili apendeze.. chid benz alitobo na pua kabisa inabidi kuuliza maswali sio kawaida.. Hawawezi wakasema wanadumisha mila...na hapa tusipoelewana basi tena mkuu itakua dah nawasi wasi sasa
 
Hii ni hoja dhaifu sana--huwezi kufananisha mavazi ya kitamaduni na uvaaji wa hareni na shanga (kiunoni) kwa wanaume. Wamasai na makabaila mengine ya wafugaji wamekuwa wakisuka rasta tangu zama za kale. Huwezi kutumia kigezo hicho dhaifu kuhalalisha ukengeufu wa kuvaa chachandu na hereni kwa wanaume. Mimi swali langu ninalouliza ni kwamba WANAUME HUVAA HERENI, SHANGA NA MIKUFU ILI IWEJE? Je, wasipovaa watakosa nini ambacho wanakifaidi pindi wakivaa vifaa hivi vya KIKE? Swali langu ni rahisi sana--sijui kwanini unarefusha hii mada kwa kuuzunguka mbuyu.

Wanaume wanaovaa cheni na hereni wanataka nini???!!!

Hilo ndilo swali lako la msingi sasa likijibiwa kwa mapana unaona nazunguka mbuyu????!!!
La chachandu unalizua sasa ili kuleta chaos na confussion,otherwise edit heading yako!!!!
Nimekujibu ninalolijua juu ya maasai kuwa ni mila imeprescribe nikaongeza na mfano wa bangili kwa masinga wa kiume na wao maana yao ni hard working and responsible (kama nakumbuka vizuri)
Aliokwambia kuwa wakivaa wanafaidi ni nani,au wanavaa ili wafaidi ni nani na unaposema kufaidi operational definition ya kufaidi hapa ni ipi????!!!!!
Halafu nani anasema bangili na mikufu ni vya kike na je unaweza sema bangili na brecelet viko kundi moja kwa mfano?????!!!!

Ukitaka hoja ijadiliwe kama wote ni watoto wa baba mmoja,kabila moja,dini moja na tumelelewa katika context moja utakuwa unakosa a sense of cultural relativism na utakuwa unagubikwa na hila ya cultural ethnocentrism!!!!!!

Mimi kwa mfano ni nusu Maasai nusu Mnubi na ni Muislam sasa umasaini mi siulizwi lolote kama naamua kuvaa mkufu au bangel ila Uislam hauruhusu!!!!!
Unaona hiyo diversity sasa ila siwezi kuwa stigmatized kuwa haya ni marembo ya kike!!!!!

Maada yako ni ndefu sana kwa nature yake na ukitaka kulazimisha iwe fupi basi utakuwa huelewi tye logic behind your very own puzzle!!!!!
 
Sasa mkuu mbona kama unasema jinsi mtoa mada alivyomaanisha..pete ya ndoa ikivaliwa kwenye jamii inajulikana ni ya ndoa na inapewa tafsiri yake..ila mwanaume akivaa mipete huku na huku kama hadija kopa..inabidi kuangalia vzr...mmasai akitoboa maskio inaeleweka kwenye jamii duniani kote...ila diamond au hemedphd akitoboa maskio na kuvaa hereni herebi ili apendeze.. chid benz alitobo na pua kabisa inabidi kuuliza maswali sio kawaida.. Hawawezi wakasema wanadumisha mila...na hapa tusipoelewana basi tena mkuu itakua dah nawasi wasi sasa

Unajua maana ya subculture???!!!!!
Jamii gani ya watu wanavaa pete na wanavaa vidole gani, wanaweka vito,vy aina gani???!!!
Watu gani wanavaa mikufu,ya ukubwa gani na madini gani,ina vidani vya mawe au madini???!!!
Wanatoboa masikio je yote mawili au moja kama moja ni la upande gani???!!!!

Uko sawa kuwa inabidi kuuliza maswali na huu ndio ufunguo wa kuelewa sio kuja na sulihisho bila hata kujisumbua kujua maana ya hao wanaofanya hayo kwa wanavyomaanisha wao na sio ujuavyo wewe!!!

Kwani wao walisema wanadumisha mila mkuu au wewe unadhani wao tajibu hivyo??????!!!!!
Tusipoewana na ukabaki na wasi wasi ni vizuri sasa chukua wasiwasi kama changamoto usome juu ya symbolic interactionism na social constructionism halafu tuendelee na mjadala kama na wewe una refferences nipe nikaongeze maarifa
 
Niwe mkweli saa yangu mkononi saa nzuri ya 200k au 300k , cheni yangu ya silver nyembamba isiyokua na kidani na visuruali vyangu kadet na vishati vyangu vya kunienea na sio oversize na ichwani nywele zangu fupi na kwenye kidevu hakuna ndevu huku kucha za mikono zikiwa fupi na nina nukia utuli ndo hua navaa halafu leo uhamasishe niache kuvaa cheni?? Whaaaat shit is this
Sawa basi hebu vaa hivyo hivyo ukatize mitaa ya Mombasa, Malindi, Pemba na Unguja halafu uone wanaume wasipopakuwa mbolea a.k.a samadi wakikuacha ukichechemea.
 
Niwe mkweli saa yangu mkononi saa nzuri ya 200k au 300k , cheni yangu ya silver nyembamba isiyokua na kidani na visuruali vyangu kadet na vishati vyangu vya kunienea na sio oversize na ichwani nywele zangu fupi na kwenye kidevu hakuna ndevu huku kucha za mikono zikiwa fupi na nina nukia utuli ndo hua navaa halafu leo uhamasishe niache kuvaa cheni?? Whaaaat shit is this

Cheni ni pambo la kike, na amelaaniwa mwanaume mwenye kuvaa mavazi/mapambo ya wanawake.kula ujana mkuu, Tuacheni sie tule uzee.
 
Ndo maana mm naona watu wanakimbia mzizi wa uzi yaani wanataka sema diamond au hemed phd akivaa hereni au mkufu au saa ya rangi ya pink kwa mfano..labda na kuweka nyele rangi na kupaka lipshin wanaendeleza utamaduni..au wanawaiga singa singa..! Basi bongo vijana tuna serious problem kwenye namna ya kuderive maono yetu ya maisha.!!!

No way hapo sasa unatoka mazima kwenye hoja! !!!!!!!

Narudia tena hayo yote ni symbolic na kila atumiaye ana maana yake na inawezekana kwa cluster yao wanaelewana sasa badala ya kuweka assumption zetu ni bora kufanya enquiry ili kupata the inner meaning from actors "verstehen"!!!!!

Anaweza kukuambia ndio anadumisha mila ya kundi fulani hapa duniani ambayo yeye anaona iko sawa kama wewe ulivyo na dini kutoka nje huko naye kaamua kuingia katika kundi ambalo kutoboa sikio yaweza kuwa sawa na maana ya kuvaa rozari au kushika tasbihi!!!!!!!

Suala la rangi pia ni mapokeo ya jamii husika mimi sina shuka nyekundu wala damu ya mzee nyumbani kwangu kwa ajili ya kitanda ila ninayo ya kimasai navaa nikiwa huko kwetu au hata mjini nikiwa na shughuli za mila yangu rangi ni mapokeo tu sio valid and reliable truth mkuu!!!!!

Lakini kama unakubali pink ni rangi ya kike mbona hutaki kugeuza shingo kuwa hao wanaosema hayo ndio wavaaji wakubwa wa mikufu na hereni????!!!!!

Nakubaliana na wewe problem ya maono ipo sana tena iko heavily loaded na stigma,rigidity,conservatism,blindness and even blanket treatments,actually suffocating from judgemental tendencies!!!!!!
 
..ila mwanaume akivaa mipete huku na huku kama hadija kopa..
rais wa Tz ndivyo anavyovaa. Sina uhakika kama ni urembo, bahati, kinga au ni alama tu!

...inabidi kuangalia vzr...mmasai akitoboa maskio inaeleweka kwenye jamii duniani kote....
pengine hata hao wamasai wanavaa/ wanatoboa kama urembo (kwa sehemu kubwa).

Kwa vyovyote vile ni vigumu mno ku generalize across people, culture and time. Kila kitu, ikiwamo tamaduni, kina mwanzo.
 
Tyta angetuwekea picha...kwa mfano una kutana na mwanaume kavaa sa nyekundu, pink, sijui blue na wengine siku hizi akivaa saa nyekundu na nguo nyekundu... Hayo mambo ya wanawake bana acheni

Hapa umecategorise....mleta mada kaileta mazimaaaa..bila kuweka boundaries ni pete zipi..mikufu ipi...saa zipi...n.k...hujaona amelaani hata uvaaji wa pete za ndoa...anasuggest ziwekwe sandukuni! Hapo ndo tunasema si sawa
 
nawashangaa hawa wanaume wanaotetea huu upumbavu. ukiona mwanaume anafagilia hivi vitu mara nyingi anakuwa na shida flani. nishakuwa na mmoja mpenda cheni sana, mengine alikuwa hafanyi naona alikuwa anaona aibu kulingana na status yake mjini. akijitahidi saaaaana ni viwili tena baada ya kupumzika kama saa mbili hivi.
Mrembo by Nature hata ww kweli unaweza kutia hoja dhaifu hivi ya kurrelate performance kitandani na uvaaaji wa cheni? Hata siamini

Cc OLESAIDIMU sokwe
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom