Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii mkoani Mtwara la Faidika Wote Pamoja (FAWOPA), Baltazar Komba amewataka wanaume kuelewa juhudi zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali za kuwawezesha wanawake kupata nafasi za kugombea uongozi.
Akizungumza na Safari Redio kuhusu kufahamu namna ambavyo wamejiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024 hususani wanawake,Mkurugenzi huyo amesema uchaguzi wa mwaka huu wanawake wengi wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo uenyekiti na nafasi nyingine.
Hata hivyo wanawake wengi ni wake za watu hivyo wanaume wanalo jukumu la kuhakikisha wanawaunga mkono wanawake ili kufikia malengo na kuunga juhudi za serikali na wadau mbalimbali zilizofanywa kwa muda mrefu.
Aidha katika kipindi hiki cha kampeni za kuelekea uchaguzi huo wanaume wanayo nafasi ya kuwaunga mkono wanawake na kuwapa nafasi ya kushiriki kufanya kampeni.
"Sisi kama wanaume lazima tuelewe kuwa wake zetu wameingia kwenye uchaguzi na sasa wapo kwenye kipindi cha kampeni,kipindi ambacho kinachukua muda wao mwingi sana unaoweza ukawa unavuruga majukumu yao ya familia,kwahiyo kama wanaume sehemu yetu ya kuunga mkono ni kuhakikisha tunawapa nafasi ya wao kwenda kufanya kampeni na sehemu ambayo itahitajika kufanya majukumu ya kifamilia tuwasaidie."amesema Komba
Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Shadida Ndile ametoa wito kwa wanaume hao kuwaamini na kuwaunga mkono wanawake ili kusimamia maendeleo ya Tanzania.
"Mwanamke ni kiongozi tangu ngazi ya familia na tunaamini ukimuwezesha mwanamke basi umewezesha jamii nzima kwasababu mipango mingi ya ndani baba anamuamini mama katika kupanga maendeleo na majukumu mengi ya kifamilia mwanamke ndie ambae anasimamia kwahiyo ukimpa uongozi atakuwa na mapana ya kusimamia jamii kwa ujumla."amesema Ndile