Elisha Ray
JF-Expert Member
- Mar 19, 2012
- 323
- 94
Wakuu, hii ni ya Taiwan kwamba wanataka kupitisha sheria kuwa na wanaume nao wawe wanakaa wakati wanakojoa. Kama tujuavyo wanaume wakiwa wanakojoa huwa kuna matone ya mkojo ambayo hurukia kwenye kingo za choo mpaka pale pa kukalia na most of the time hawafuti choo maana hata ukiflash bado yanakuwepo. Sasa yale matone baada ya muda hutengeneza vijidudu ambavyo vinasababisha U.T.I na magonjwa mengine ya namna hiyo kwa wanawake kwani kutokana na maumbile yao huwa rahisi kwao kushambuliwa kama nao hawasafishi/hawafuti choo kabla ya kutumia (katika public toilets au nyumba zenye wakaka wasiosafisha vyoo baada ya kutumia). Sasa na hii sitashangaa ikija bongo na mie siko tayari kukaa ili nikojoe wakati naweza kukamua nimesimama... Wajameni kwa wale wasio na tabia ya kufuta choo baada ya kukojoa badilikeni kuweni wasafi basi ili hii kadhia isije kwetu eeenh???? Tuwapende mama/dada/wake zetu basi na kwenye afya zao pia!!!! Ni rahisi tu, ukikojoa futa zile kingo then flash... Hii mambo ya kuambiwa mke/mama/dada/mtoto ana UTI haipendezi halafu kumbe wewe mume/baba/kaka ndo chanzo!!!!