Wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao, kweli?

Na kingine nilichojifunza, mwanaume akiwa karibu na mama yake na kumpenda mama yake anakuwa na respect kwa wamama wote including mkewe. Nina mifano mingi sanaaa. I love mama's boys.
 

nilifundishwa kwamba mwalimu mkubwa wa mwanaume ni dunia, na pia ndoa nyingi zinateseka iwapo kijana anakua karibu sana na mama kwani mama huingilia ndoa ya mwanae.... pia nikasikia kwamba watoto wa mama wanadeka hadi kwenye ndoa

MY ADVICE: WANAUME WAZURI NI WALE WANAOFUATA MAADILI NA WALIONUFAIKA NA MALEZI BORA YAWE YA MAMA, BABA AU WAZAZI/WALEZI WOTE WAWILI
 
Naunga mkono hoja..sitopenda kusifia sana coz nitakuwa najisifia coz hata mimi nimelelewa na mama.Nilijifunza mambo mengi kwani mimi ndiye niliyekuwa nawatunza wadogo zangu kuwapikia kuwaogesha...kuwabembeleza walale mchana huku maza akiwa kazini ...


Mhhhhhh! Congrats Mkuu! Mi nawapenda sana watu kama wewe. Hakuna ubaya wa kujifagilia 🙂🙂
 

AMINA!
Ila hapo kwenye bold....ukumbuke siyo kila mtoto ana bahatika kulelewa na baba na mama kwa sababu mbalimbali.
Kuna wanaozaliwa na mama akiwa mzazi-peke, kuna wanaokataliwa na baba zao, kuna wanaojikuta wazazi wameachana, kuna wanaofiwa na baba zao.Mradi kuna kila sababu.Yote ni majaaliwa ya mola.
 
Nilikuwa sijalisoma vizuri hili li sredi asee:

Kulaaaaleki!

Hiyo red......... Mungu apitishie mbali. Heri tulelewe na baba zetu bana
Nahisi kampeni ya kuingiza mswada wa Cameroon kwenye katiba ya MMU! Na hili halikubaliki!

Halafu kuhangaika na kuosha masufuria ndo kitu gani tena?
 
Afu watu wengi wana conclude kuwa wanaume wanaodeka ni wabaya. Si kweli kikubwa apate partner anayejua kudekeza; kuwe na balance. Si wanawake wote wanadeka. Kama mimi ninapenda sana mwanamme anayedeka kwani napenda kudekeza. Mume wangu anadeka but I like it.
 
F'COZ DC.
Hakuna la kawaida lisilo na exceptions, na pia huwezi kujumuisha watu wote kwenye kila situation.


Hapo sasa tunaanza kuelewana,

Pamoja na kuwa kuna ukweli fulani...Lakini sina hakika kama sample size yetu inatupa uhakika wa kusema hayo tunayotaka kuyasema! Na hapa kuna watu wametoa upende mwingine kabisa ingawa inaonekana hoja zao umezitupa kapuni...

Ni ukweli usiopingika kuwa kuna mama wengine wanaharibu sana watoto kwa malezi ya kizembe zembe na kudekeza dekeza!!

Kwangu mimi, nasimama kwenye ideal situation ambayo naamini ndiyo yalikuwa malengo ya Mungu, kwamba ni bora watoto wakalelewa na wazazi wote...Ila kama imeshindikana, basi mama (kama yuko responsible) anaweza kuwa mlezi mzuri!

Disclaimer: This is from a man's perspective!!
 
Asikwambie mtu mwanaume anayejua kupika anakuwa more romantic kuliko asojua. Kuna wakati anakwambia darling tulia leo mi ndo sterling hapa jikoni. Mungu akupe nini donda ndugu???

I knew from the start, kwamba hicho kitu wanawake wanakipenda sana....Naenda jikoni kama kuna sababu ya msingi aisee!!
 

Kweli kabisa....Angalia sana usije kuharibu watoto wako???

Sipate picha dume linalodeka linakuwaje....

No, no please....Mwanaume wa kweli sharti awe kidume 24/7...!!!
 
Baba's boys utawajua tu

Kuna mtoto wa kiume wa dada yangu anapenda sana kazi za jikoni. Basi ikifika likizo kila mtu anamgombania. He is so loving. Yani akija kwako yeye muda wote mtashinda nae jikoni. What a good husband to be for the lucky lady.

Kweli kabisa....Angalia sana usije kuharibu watoto wako???

Sipate picha dume linalodeka linakuwaje....

No, no please....Mwanaume wa kweli sharti awe kidume 24/7...!!!
 
Kweli kabisa....Angalia sana usije kuharibu watoto wako???

Sipate picha dume linalodeka linakuwaje....

No, no please....Mwanaume wa kweli sharti awe kidume 24/7...!!!

Kudeka anakozungumzia NK ni kudeka kwa kiutu uzima bana!
Kudeka huko siyo kule kwa kumfanya hata hajui kubadilisha bulb au kuunganisha waya zilizokuwa loose.La hasha!
Kudeka huku ni kule kwa kimahaba zaidi.Mwanaume haoni vibaya kuchukua khanga ya mkewe akajifunga wakakaa wote jikoni,haoni vibaya kukumbatiwa, haoni soo kulishwa chakula...
Siyo tena jianadume limengangamara utadhani mnara wa babeli! Halidekezwi wala halibembelezeki!Limeshupaa mwanzo mwisho! Mara nyingi midume kama hii ngumi mkononi! Ni ubayaubaya tu!

 

NK,
Wewe nami tuko ukurasa mmoja!
 
Kudeka hakukufanyi usiwe mwanaume. Kuna watu wanawalea watoto wao wa kiume kuwa wakatili bila kujua. Mfano utasikia "unalia wewe mwanamke" what a statement?! Cry my boy cry! Alosema wanaume hawana haki ya kuonyesha feelings zao nani?

 

Msaidieni huyo mtoto....Hapo alipo hali yake ni mbaya sana. Labda kama mna mpango wa kumgawa kwa mzungu!!

Nina hakika binti zangu hawatamtaka huyo...

Kuna dada mmoja alikuwa anasema kwamba kama mume wake aking'ang'ania kushinda nyumbani (siyo jikoni) lazima atengeneze ajali amuunguze na maji ya moto!!

Sasa huyo anayeshinda na wanawake jikoni atapata wapi muda wa kujadili mambo ya kiume na wanaume wenzake!!

Big no to my boys!!
 
Ndo nasikia leo. AU sizitaki mbichi hizi. Kweli kuna mwanamke anayependa mumewe ashinde kijiweni au bar???


 

Please Tausi,

Mbona package nyingine zina utata??? Sasa huyo ni mwanamume au shoga yako???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…