WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
mie nimelelewa na dingi na ma bro
najua kupika ile mbaya
nina penda sana kumpa mpenzi wangu "double love', as 4 mum and her, coz mum alivuta nkiwa mdogo sana
ila ni mbabe wa kutupwa demu anapoleta mapozi ya nyau
Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali, etc.
Hili likanifanya nifikirie na kwa kiasi nikaona lina ukweli.Nimeliona hilo kwa ndugu zangu wa kiume waliolelewa na mama zao bila kuwepo baba, au wale waliokuwa na baba lakini wakatii sana mafundisho ya mama zao.Wako independent zaidi, hawanaga makeke sana kwa wake zao, nk...
Hebu tupate mawazo zaidi kwa wale wenye uzoefu.
TM,
Tabia ya mtu hujengwa na malezi na mazingira.Mazingira ni pamoja na mila, desturi, imani za dini etc.
Mama ni mwalimu wa kwanza wa mtoto na mwalimu mzuri atafundisha vizuri somo litaeleweka kwa wanafunzi
wenye kufundishika.Mwalimu mwenye wito naye ni tofauti na yule asiye na wito.Hapa nataka kutofautisha malezi
ya mama mwenye wito wa kuwa mama, na malezi ya mama mwenye kulea mradi twende.Mama mwenye wito
atalea watoto watakaokuwa mama/mke au baba/mume mzuri huko mbeleni.
Baada ya kusema hayo, nitajaribu kujibu swali kama ni kweli malezi ya karibu ya mama yanasababisha
mwanaume awe mzuri ( kitabia) na kuwa kivutio kwa mke/wanawake.Kijana anapokuwa karibu na mama yake,
na mama akampatia mafunzo sahihi yenye kumjenga kama mwanaume kwa maana kutambua uanaume wake,
lakini hapohapo kujifunza stadi mbalimbali, basi kuna uwezekano mkubwa kwa kijana/mwanaume huyu kuja kuwa mume bora zaidi ya yule asiyepokea mafunzo.Nasema asiy
Aidha kuna akina baba nao huchangia kuharibu mwitikio, kwa kuwakataza vijana wao wasiingie
kufanya yale yanayodhaniwa ni ya wanawake.Vijana kama hawa huweza kujikuta wakiigiza yale waliyoyaona kwa baba
zao ( hasa yale yasiyo mazuri sana kama kutokupenda kuwajibika, ulevi etc) na kuwa mzigo kwa familia zao katika
huu ulimwengu uendao kasi wenye kuhitaji ushirikiano baina ya mume na mke.
Tukija upende mwingine, malezi ya mama nayo yaweza kuchangia kumharibu kijana kama mama atasahau
kukomelea ( re-enforce) yale yanayomfanya mwanaume ajenge kujiamini kama mwanaume.Hapa kijana
anaweza kuelemea zaidi zile tabia za kujirudisha nyuma au kujiweka chini ya himaya ya mtu mwingine
kama alizoea kumsikiliza mama atoe kauli ya mwisho, au kusubiri mama amfanyie kila kitu.
nyumbani kisa ni watoto wa kiume.Vijana kama hawa ni tofauti na wale vijana waliolelewa kwa kufunzwa,
wakiwa na nyumba zao basi ni mzigo mkubwa sana kwa wake zao kwa sababu hawafanyi kitu
bila kumuuliza mama.Si ajabu hata mke wakatafutiwa na mama.
Hitimisho langu naweza kusema kuwa kuna ukweli - ikiwa wamepewa malezi/mafunzo "sahihi".
Nimependa mchango wako. Ila hapo uliposema mwanaume anatakiwa kujengwa kama mwanaume na kutokuwa chini ya himaya ya mtu nimepata shaka kidogo. Nikichukulia malezi nilopewa, hakuna cha ubaguzi wa huyu mwanamke wala mwanaume we were all treated equally na nadhani mwanamke pia anatakiwa kutokujishusha wala kuwa chini ya himaya ya mtu, otherwise atakuwa chini ya kila mwanaume forever.... Yes kuna vya ku give and take kwenye relationship but that goes both ways na si kwa kuwa mimi mwanamke niwe wa ku give tuuuuu.
Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali, etc.
Hili likanifanya nifikirie na kwa kiasi nikaona lina ukweli.Nimeliona hilo kwa ndugu zangu wa kiume waliolelewa na mama zao bila kuwepo baba, au wale waliokuwa na baba lakini wakatii sana mafundisho ya mama zao.Wako independent zaidi, hawanaga makeke sana kwa wake zao, nk...
Hebu tupate mawazo zaidi kwa wale wenye uzoefu.
Ni kweli kwa kiasi kikubwa, ila kwa wanawake waliolelewa na mama pekee au wale ambao mama yao amemtawala baba, ni kinyume kabisa cha hao wa kiume. sijui ni kwanini kwani wengi wa wanawake walioishi na single parent ambaye ni mama ni 'social problem' completely
Asante,
Nimeyapokea maoni yako.Nitasema kitu kimoja.
Niliposema 'kutokuwa chini ya himaya' nilimaanisha mwanaume awe na "independent mind".
Sikumaanisha malezi yenye ubaguzi hasa wa kijinsia japo wa kijinsi ni muhimu ku shape mtu "me" awe "me" na syo "ke".
Nimeona kuna walioleta hoja ya wanaume wanaokuja kuwa "gays" kwa vile waliachwa zaidi katika kujitambulisha na
utambulisho wa "ke".
Kwa kuweka mambo sawa napenda niseme kwamba,hata wanawake wenye kupenda wanaume walio na
vigezo tunavyovijadili hapa, wanataka mwanaume awe na "added value" inayoleta tofauti ya kuwa "me' na "ke".
Mkiwa wote "mnafanana', sijui hiyo nyumba itakuwaje.Binafsi ninapenda mwanaume atakayenifanya
nijiskie kuwa niko na mwanaume na siyo mwanamke mwenzangu.Katika mahusiano, kinacholeta ladha
ni utofauti.Mkiwa "wote sawa" sijui inakuwaje.
Ni mtizamo wangu tu.

vipi bi dada nikimrudisha huyu mke wangu nije kwako?Nalog offMi nataka mwanaume anizidi nguvu tu za kutwangana ili tukitoka awe mlinzi. Lol. Ila asithubutu kuinua mkono wake kunitia hata kofi. Vingine not necessary. Na suala la mwanaume kuwa na nguvu halina kozi ni nature. Kama ni pesa akinizidi sawa, nikimzidi sawa vile vile kwani kwa elimu nilonayo si hajabu kuwa na kipato zaidi ya hubby au yeye akawa nacho zaidi yangu inategemea nani ana bahati zaidi.
Duh, napenda mwanamme mkali, akiingia ndani wote tunakaa mguu sawa. Hagusi kazi za nyumbani labda nyumba nzima tunaumwa lakini awe anatimiza majukumu yake ya kibaba, pure mwanamme wa kiafrika.
Hata kama namzidi mshahara naweza mpya kadi na password kwa ajili ya kupanga matumizi ya familia, mimi napenda niwe mshauri na yeye awe decision maker.
A man should be a CEO wa familia, hawa wa kupika na kupakua ?????
mwanaume anajilizaliza bila sababu! tia chaka mwanaume wa style hii,nichague mimi.Nalog off
Mie mawenge, wewe mawenge, haitakuwa familia hiyo, lazima nipate kichwa kilichotulia
Maelezo yametulia haya.. looh!....kijana/mwanaume bora ni yule aliyepata malezi bora ya baba na mama(yenye uchaji Mungu)..hakumwona mzazi mmoja akitenda kinyume...suala la kujua kupika,kufua nk. halihusiani kabisa na tabia/ubora wa mtu...Asante,
Nimeyapokea maoni yako.Nitasema kitu kimoja.
Niliposema 'kutokuwa chini ya himaya' nilimaanisha mwanaume awe na "independent mind".
Sikumaanisha malezi yenye ubaguzi hasa wa kijinsia japo wa kijinsi ni muhimu ku shape mtu "me" awe "me" na syo "ke".
Nimeona kuna walioleta hoja ya wanaume wanaokuja kuwa "gays" kwa vile waliachwa zaidi katika kujitambulisha na
utambulisho wa "ke".
Kwa kuweka mambo sawa napenda niseme kwamba,hata wanawake wenye kupenda wanaume walio na
vigezo tunavyovijadili hapa, wanataka mwanaume awe na "added value" inayoleta tofauti ya kuwa "me' na "ke".
Mkiwa wote "mnafanana', sijui hiyo nyumba itakuwaje.Binafsi ninapenda mwanaume atakayenifanya
nijiskie kuwa niko na mwanaume na siyo mwanamke mwenzangu.Katika mahusiano, kinacholeta ladha
ni utofauti.Mkiwa "wote sawa" sijui inakuwaje.
Ni mtizamo wangu tu.
Nadhani somo hapa liko wazi - waume wazuri na wake wazuri huanza kuandaliwa nyumbani. Na siyo tu kwa uzuri wa maisha ya ndoa lakini generally character inajengwa nyumbani kwa kupata malezi sahihi, ya wakati na ya kina. Nje ya hapo tunakuwa kama kulazimisha maji yachanganyike na mafuta! Mtoto akiwa mtu mzima hajijui kama yeye ni maji, au mafuta au matope!