Nilibahatika kusikiliza mazungumzo ya wadada fulani wakisema ati wanaume wazuri ni wale waliopata malezi ya karibu ya mama zao.
Wakatoa mifano ya ni vipi waliliona hilo:
Wanaume hao wanajua kupika, kulea watoto, wana huruma zaidi, wanaheshimu wanawake, wana upendo, wanajali, etc.
Hili likanifanya nifikirie na kwa kiasi nikaona lina ukweli.Nimeliona hilo kwa ndugu zangu wa kiume waliolelewa na mama zao bila kuwepo baba, au wale waliokuwa na baba lakini wakatii sana mafundisho ya mama zao.Wako independent zaidi, hawanaga makeke sana kwa wake zao, nk...
Hebu tupate mawazo zaidi kwa wale wenye uzoefu.
TM,
Tabia ya mtu hujengwa na malezi na mazingira.Mazingira ni pamoja na mila, desturi, imani za dini etc.
Mama ni mwalimu wa kwanza wa mtoto na mwalimu mzuri atafundisha vizuri somo litaeleweka kwa wanafunzi
wenye kufundishika.Mwalimu mwenye wito naye ni tofauti na yule asiye na wito.Hapa nataka kutofautisha malezi
ya mama mwenye wito wa kuwa mama, na malezi ya mama mwenye kulea mradi twende.Mama mwenye wito
atalea watoto watakaokuwa mama/mke au baba/mume mzuri huko mbeleni.
Baada ya kusema hayo, nitajaribu kujibu swali kama ni kweli malezi ya karibu ya mama yanasababisha
mwanaume awe mzuri ( kitabia) na kuwa kivutio kwa mke/wanawake.Kijana anapokuwa karibu na mama yake,
na mama akampatia mafunzo sahihi yenye kumjenga kama mwanaume kwa maana kutambua uanaume wake,
lakini hapohapo kujifunza stadi mbalimbali, basi kuna uwezekano mkubwa kwa kijana/mwanaume huyu kuja kuwa mume bora zaidi ya yule asiyepokea mafunzo.Nasema asiy
Aidha kuna akina baba nao huchangia kuharibu mwitikio, kwa kuwakataza vijana wao wasiingie
kufanya yale yanayodhaniwa ni ya wanawake.Vijana kama hawa huweza kujikuta wakiigiza yale waliyoyaona kwa baba
zao ( hasa yale yasiyo mazuri sana kama kutokupenda kuwajibika, ulevi etc) na kuwa mzigo kwa familia zao katika
huu ulimwengu uendao kasi wenye kuhitaji ushirikiano baina ya mume na mke.
Tukija upende mwingine, malezi ya mama nayo yaweza kuchangia kumharibu kijana kama mama atasahau
kukomelea ( re-enforce) yale yanayomfanya mwanaume ajenge kujiamini kama mwanaume.Hapa kijana
anaweza kuelemea zaidi zile tabia za kujirudisha nyuma au kujiweka chini ya himaya ya mtu mwingine
kama alizoea kumsikiliza mama atoe kauli ya mwisho, au kusubiri mama amfanyie kila kitu.
nyumbani kisa ni watoto wa kiume.Vijana kama hawa ni tofauti na wale vijana waliolelewa kwa kufunzwa,
wakiwa na nyumba zao basi ni mzigo mkubwa sana kwa wake zao kwa sababu hawafanyi kitu
bila kumuuliza mama.Si ajabu hata mke wakatafutiwa na mama.
Hitimisho langu naweza kusema kuwa kuna ukweli - ikiwa wamepewa malezi/mafunzo "sahihi".