Hilo "kujichua" nalichukia sana limeniharibia mno brand
Mwez uliooita nilipata mshtuko kwa mguu nikawa siwez hata kutembea nikapiga x ray haikua tatizo kubwa nikapewa dawa za maumivu na dawa kuchua.
Sasa last week nilikua shop jiran na home mzee wangu akawa ananijulia hali nikamwambia niko poa kuna dawa pamoja za kuchua ,akaniuliza kuna mtu wa kukuchua sasa?
nIkamwambia tangu wife asafiri najua tu nishazoea wala hakuna shida tena ya kutafuta mtu mmwingin.
Kuna mmama mtu mzima jiran yetu akadaka hio sentens ya mwisho ,nikaona jion nmekuja kutembelewa na viongoz wangu wa jumuia ,wakitaka kujua wife yuko wapi na pia kunielekeza madhara ya punyeto kiafya na kiroho , maumivu niliopata siku ile moyoni ningekua na uwezo that day hata moyo pia ningeuchua ilikua ni maumivu plus fedheha