Wanaume wenzangu tupunguze aibu ndogo ndogo

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Kwenye maisha huwezi kufanya kila kitu, na huwezi kujua kila kitu , japo kuna vitu vidogo vidogo si mbaya kuvijua na kama huvijui jaribu kukaa kimya ili kuepuka na aibu.

Mimi napenda sana michezo kama mpira wa miguu na nimeucheza miaka hiyo.lakini pia ni mfuatiliaji mzuri wa mipira na klabu za ulaya,nikiwa ni Real Madrid fan kwa upande wa Spain,lakini ni shabiki wa Arsenal the Gunners kwa upande wa England.na Yanga kwa hapa Nyumbani

Basi kwa mantiki hiyo nafuatilia sana huu mchezo kwa kiasi fulani Mimi naingia vibanda umiza na kwenye mabaa kwani napenda sana makelele,kitu kilichonishinda ni kwenda uwanjani,hata nikienda huwa nalazimishwa tu kwakuwa ni sehemu ya mtu nafahamika na wadau hivyo huwa sina pa kukwepea napenda jinsi Tv inavyorudia matukio

Kilichonisukuma niandike huu uzi ni watu kushindwa kujua ni kinaendelea kwenye Dunia ya soka.

Kuna siku msimu huu 2024/2025 kulikuwa na mechi kati ya Valencia na Barcelona,ile mechi Barcelona alianza kwa kufungwa, basi tukiwa kwenye ile pub,akainuka mjuba mmoja tena anaonekana ni mjanja tu masikini akauliza kwani Messi Yuko wapi mbona hamuoni?
Watu tukakaa kimya tukijua labda anafurahisha watu, asalaaalee kumbe mchizi hajui chochote,akainuka na kuondoka kwa aibu huku akizomewa.

Kubwa zaidi Jana nilikuwa maeneo fulani tunaicheki TAIFA STARS timu ambaye ikikujaa kifuani huenda ukafariki kwa presha kutokana na mwenendo wake mbaya ikiwa na odds 1.9 nikaipa Direct win kwa pesa ya mke wangu kilichotokea wanamichezo tumeona tumesikia.

Kilichonishangaza ni wanaume watu wazima wanaoonekana wana ushawishi ni watu wa mjini na wengine nawafahamu , kuanza kuwaulizia Aziz ki na Chama,hakika nilicheka sana nimezoea kusikia habari hizi toka kwa wanawake hata mke wangu anaweza kukaa kwenye TV mpo wote lakini asijue nini kinaendelea,hata baada ya Mamelodi Sundown kutudhulumu goli kidogo hamu ya kula ilipotea huku wife akinicheka akidai yanini nijiumize na vitu si vya msingi

japo Kuna wanawake kibao wanafatilia mchezo huu vizuri.

Huenda wajuba walikuwa sahihi maana Mzize,Job na wengine walikuwa first Eleven huku Mwamnyeto na Mudathir wakiwa Sub,aibu niliona mimi tena wajuba wakawa wanalaumu kabisa kwanini Key master hajaanza😂😂😂 aibu niliona

Tatizo sio kutokujua,tatizo ni ule wajihi ,majamaa wanaonekana mafuta sana halafu ..... Dah

Jamani kitu hukijui uliza,au nyamaza itasaidia kukulindia heshima yako .
 
Wewe jamaa nimekushangaa sana. Unafikiri ulimwengu wa interest zako ndio ulimwengu wa kila mtu?

Nina friend wangu from Newcastle england. I was supprised aliponiambia hamjui Wala hajawahi kumfatilia Allan Shearer, u can imagine. Kwake yeye mastaa wa michezo anaowajua ni wanacheza mchezo wa ice hockey. Wewe unaijua ice hockey?
 
Umeongea sahihi..kuna vitu vya msingi hata kama huvifuatilii lazima kama mwanaume/Baba uvifahamu
 
Wewe jamaa nihangaa sana. Unafikiri ulimwengu wa interest zako ndio ulimwengu wa kila mtu?

Nina friend wangu from Newcastle england. I was supprised aliponiambia hamjui Wala hajawahi kumfatilia Allan Shearer, u can imagine. Kwake yeye mastaa wa michezo anaowajua ni wanacheza mchezo wa ice hockey. Wewe unaijua ice hockey?
Nasema hivi ,usiropoke kitu usichokijua
 
point ya Jack Daniels ni kwamba. Kama unajua hujui kuwa mpole usilete ujuaji kwenye mambo ambayo uyajui utajiletea fedhea bure.

Punguzeni ujiaji kwenye mambo msiyoyajua. Kama wewe doctor kapeleke ujuaji wako kwa wangojwa ukifika kwenye mpira na hujui kitu wewe na udoctor wako unakaa kimyaa au unauliza kwa utulivu usilolifahamu kuhusu mpira.
 
Kwenye maisha huwezi kufanya kila kitu, na huwezi kujua kila kitu , japo kuna vitu vidogo vidogo si mbaya kuvijua na kama huvijui jaribu kukaa kimya ili kuepuka na aibu.

Mimi napenda sana michezo kama mpira wa miguu na nimeucheza miaka hiyo.lakini pia ni mfuatiliaji mzuri wa mipira na klabu za ulaya,nikiwa ni Real Madrid fan kwa upande wa Spain,lakini ni shabiki wa Arsenal the Gunners kwa upande wa England.na Yanga kwa hapa Nyumbani

Basi kwa mantiki hiyo nafuatilia sana huu mchezo kwa kiasi fulani Mimi naingia vibanda umiza na kwenye mabaa kwani napenda sana makelele,kitu kilichonishinda ni kwenda uwanjani,hata nikienda huwa nalazimishwa tu kwakuwa ni sehemu ya mtu nafahamika na wadau hivyo huwa sina pa kukwepea napenda jinsi Tv inavyorudia matukio

Kilichonisukuma niandike huu uzi ni watu kushindwa kujua ni kinaendelea kwenye Dunia ya soka.

Kuna siku msimu huu 2024/2025 kulikuwa na mechi kati ya Valencia na Barcelona,ile mechi Barcelona alianza kwa kufungwa, basi tukiwa kwenye ile pub,akainuka mjuba mmoja tena anaonekana ni mjanja tu masikini akauliza kwani Messi Yuko wapi mbona hamuoni?
Watu tukakaa kimya tukijua labda anafurahisha watu, asalaaalee kumbe mchizi hajui chochote,akainuka na kuondoka kwa aibu huku akizomewa.

Kubwa zaidi Jana nilikuwa maeneo fulani tunaicheki TAIFA STARS timu ambaye ikikujaa kifuani huenda ukafariki kwa presha kutokana na mwenendo wake mbaya ikiwa na odds 1.9 nikaipa Direct win kwa pesa ya mke wangu kilichotokea wanamichezo tumeona tumesikia.

Kilichonishangaza ni wanaume watu wazima wanaoonekana wana ushawishi ni watu wa mjini na wengine nawafahamu , kuanza kuwaulizia Aziz ki na Chama,hakika nilicheka sana nimezoea kusikia habari hizi toka kwa wanawake hata mke wangu anaweza kukaa kwenye TV mpo wote lakini asijue nini kinaendelea,hata baada ya Mamelodi Sundown kutudhulumu goli kidogo hamu ya kula ilipotea huku wife akinicheka akidai yanini nijiumize na vitu si vya msingi

japo Kuna wanawake kibao wanafatilia mchezo huu vizuri.

Huenda wajuba walikuwa sahihi maana Mzize,Job na wengine walikuwa first Eleven huku Mwamnyeto na Mudathir wakiwa Sub,aibu niliona mimi tena wajuba wakawa wanalaumu kabisa kwanini Key master hajaanza😂😂😂 aibu niliona

Tatizo sio kutokujua,tatizo ni ule wajihi ,majamaa wanaonekana mafuta sana halafu ..... Dah

Jamani kitu hukijui uliza,au nyamaza itasaidia kukulindia heshima yako .
Hao walidai mbona Aziz Ki na Chama hawapo,yamkini msemo wa "Timu ya wananchi" umewaharibu akili,walijua labda ni Yanga🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom