Wanaume wenzangu tupunguze Chips-Viazi, tutafedheheka !

Wanaume wenzangu tupunguze Chips-Viazi, tutafedheheka !

Kwa wanaume wenza mitaa ya Jamvi,
Jana nikiwa napita maeneo katikati ya Jiji , mara hammadi , mbele yangu pakawa na vijana wawili wakiwa na makundi mawili ya wapambe.
Kwa dakika chache nilizosimama kuangalia mwenendo wa mambo katika makundi yale yaliokua yakihasimiana , kila kundi lilikua likimsapoti mmoja baina ya vijana wale wawili waliokua wakiporomosheana mitusi ya nguo.
Muda si muda ngumi zikajiri baina ya vijana wale.
Wakati ngumi zinaanza niliwasikia wapambe wa makundi wakisema "Hapa leo haamuliwi mtu, leo wapigane hadi mwisho wao ndiyo wataheshimiana mnatusumbua kila siku tumewachokeni"
Nami ama kwa umbea au kwa kila kiingiacho mjini si haramu, nikasema sibanduki hadi nione mwisho wa ndindo hizo.
Kuzingatia mijanadume ile kuonekana ni ile yenye mijifua mikubwa na mikono iliojaa marinda ya viazi, nikajua shughuli pevu itakuwepo.
Wadau ngumi zile , ndondi hazikumaliza dkk 5 !
Wanaume wale wakiwa hawajaamuliwa walikua washatepeta ile lachilachi ! Mbendembende !
Hakuwepo wa kurusha konde .
Ile hali ilinishtua na nikalazimika niifanyie utafiti iweje mibarobaro kama ile iwe vile kama mikaka poa?
Hatimae jana nikakutana na jamaa yangu ambae ni (X-Boxer)
nikampa muhtasari mzima wa lile tukio na nini sababu ya vijana kuwa wachovu kiivo.
MAJIBU
Mdogo wangu vijana wa sasa tatizo la kukosa nguvu linaanzia kwenye msosi.
Usitegemee mchana ushindie Chips , na jioni Chips then ukategemee kuwa na nguvu ! Tena si za kupigana ngumi tu hata nguvu za Para (ngono) utakua hoi tu.
Vyakula vya kwenye makopo, Kuku wanaozalishwa bila Jogoo , Mayai ya incubation, Ugali wa unga uliolowekwa ni matatizo matupu!
MWISHO WA MAJIBU.
Nami nimeshawishika kwa nia njema kabisa niitupe Mkekani, kwa kuwaokoa wanaume wenzangu hizi ChipsChips tuzipunguze kama si kuachana nazo.
Zitatupelekea fedheha kwa hawa wanawake wetu kutudharau kwa kuja kwetu kuwapa ule muziki upaswao tuwape. AIBU
A s a n t e n i
Misosi tunapiga na mazoezi tunahudhuria kama kawaida. hiyo imekaaje?
 
Mbona wataalamu wa lishe wanatuambia kuwa viazi na ugali vyote vina kazi moja vya kuupa mwili nguvu. Jamani vyote si vyakula vya wanga?
 
Lakini wanaume wa Dar nani kawaroga?? Wanaume wa mikoani tunakula ugali maharage nyie mnakula chips hadi mnaandaa matamasha ya kula chips mayai? Hivi hizi heshima kwenye ndoa zenu zitaletwa na ngumi? Jipangeni aisee.....watu wanahamasishana kula ugali wa dona,ugali wa muhogo...nyie mnatuletea vituko gani? Kuweni sirias aisee mnatutia aibu. Huku kwetu Mbeya chips mayai inatumika kama mboga wakati wa kula dona.Arusha chips mayai wanaita matunda sasa [emoji51][emoji51][emoji51]nyie mnakula na mnalalia! Halafu baada ya miaka mnaanza kukimbilia kwa DR. MWAKA. Jaman acheni hizi aibu.


Am Done!
 
Lakini wanaume wa Dar nani kawaroga?? Wanaume wa mikoani tunakula ugali maharage nyie mnakula chips hadi mnaandaa matamasha ya kula chips mayai? Hivi hizi heshima kwenye ndoa zenu zitaletwa na ngumi? Jipangeni aisee.....watu wanahamasishana kula ugali wa dona,ugali wa muhogo...nyie mnatuletea vituko gani? Kuweni sirias aisee mnatutia aibu. Huku kwetu Mbeya chips mayai inatumika kama mboga wakati wa kula dona. [emoji51][emoji51][emoji51]nyie mnakula na mnalalia! Halafu baada ya miaka mnaanza kukimbilia kwa DR. MWAKA. Jaman acheni hizi aibu.


Am Done!
 
Lakini wanaume wa Dar nani kawaroga?? Wanaume wa mikoani tunakula ugali maharage nyie mnakula chips hadi mnaandaa matamasha ya kula chips mayai? Hivi hizi heshima kwenye ndoa zenu zitaletwa na ngumi? Jipangeni aisee.....watu wanahamasishana kula ugali wa dona,ugali wa muhogo...nyie mnatuletea vituko gani? Kuweni sirias aisee mnatutia aibu. Huku kwetu Mbeya chips mayai inatumika kama mboga wakati wa kula dona. [emoji51][emoji51][emoji51]nyie mnakula na mnalalia! Halafu baada ya miaka mnaanza kukimbilia kwa DR. MWAKA. Jaman acheni hizi aibu.


Am Done!
 
Kwakweli wanaume wa Dar wametudhalilisha sana....Teh Teh...
 
Muda si mrefu tutasikia wanawake D'salaam wanaandamana kisa waume zao "hamna kitu" kabisa kunako 6X6.
 
Ngoja sass uone jinsi utakavyotukanwa japo umeongea ukweli na siku zote msema ukweli ni mpenzi wa MUNGU
 
Kweli waambie Mimi hapa ilemi nimekula ndizi za kuchoma magimbi na maparachichi nikashushia na maziwa mgando kiasili zaidi [emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Dresalaam ni jiji sio kijiji....
kuna watu wa kila aina
faida ya kuishi kwenye jiji ni uhuru wa kufanya unachokipenda bila kuhofia 'wanakijiji' watakufiikiriaje...

Sasa kama wewe inakuuma baadhi ya watu kula chips na wewe unaona sio sahihi....basi una tatizo wewe binafsi

huku jijini kuna watu mlo mmoja ,wengine miwili ,wengine mitatu na kadhalika...
wengine siku inapita tu hivyo hivyo but wote hao hawajali nani anakula nini

karibu jijini....
 
IMG-20160602-WA0046.jpg



Mtu akipata jina Dar akienda mkoa wowote anakuwa superstar
 
Back
Top Bottom