Wanaume wenzangu tusifanye hivi

Umeongea point mkuu
 
Mahitaji ndio tatizo...unakuta binti ameshika mimba na hana kipato cha kutosha inamiwia vigumu kutimiza mahitaji ya mtoto , hivyo anabaki anajilaumu na kuhuzunika mwisho anapata msongo wa mawazo
 
Kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa ndiyo mwanzo wa matatizo yote haya - utoaji mimba, kuwa na single parents, mauaji, n.k. Kama jamii tunapaswa kubadilika.
Vipi na wale waliooana na bado wanachomana moto kwa magunia ya mkaa??
 
Pisi kali kama hii imekuwaje tena imeamua kukwama. Shida ni ulaya, ingekuwa bongo, huyu mchumba anawekwa ndani anaishi kama mwali bila kutoa mia, na watoto analelewa bila shida.
 
Shauri yake. Kwani alipoamua kuzaa bila mpangilio alitegemea nini?
 
Inasikitisha ila hapa kuna fundisho mara mbili. (1) Unaweza kukuta mdada anaamua kuzaa tu na kibaka wa kitaa sababu ya tamaa ya kumiliki IPhone 13 au Samsung S21 wakati jamaa hana mpango naye, yeye anataka shoo tu kisha asepe zake. Huyu kibaka hata umsingizie kuwa mimba ni yake hana mpango nawe, utaishia kushinda kwa waganga tu kumrudisha akili akuwaze wewe.

(2) Hii ninaweza sema kidogo inaweza linagana na point namba moja maana unakuta wanawake wengi wanapenda kujiingiza mahala pasipo na pendo ili tu apate kutunzwa na mwanamme. Atajitahidi kujipendekeza hata kama hatakiwi, anaweza kujuwa jamaa ni kicheche ana mademu kila kona ila yeye atajipendekeza tu kwa jamaa kisa ana gari, hela, nyumba nzuri, kazi nzuri, mwisho wa siku anashika mimba ya jamaa bila matarajio, java anamtimua.

HAKUNA mwanamme anayependa kushitukizwa na ujauzito labda apange yeye mwenyewe. Ujinga huu wanao sana mademu wa kibongo haswa hawa macelebrity uchwara wetu.
 
Haya matukio japo yanasikitisha lkn yakawe funzo kwao
 
Yamenikuta hayo hayo au wewe ni mimi?
 
Yamenikuta hayo hayo au wewe ni mimi?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Acha kabisa!! Unawekwa kwenye majaribu magumu ya kufanya maamuzi--

--huku unajua mahusiano yenu yalishashindwa, huku unajua kuna mtoto anakuja na hautaki mtoto alelewe pasipo baba na mama pamoja!!

Wanaume na wanawake tuna 50% shares kwenye changamoto ya ongezeko la single mothers!
 
Hujaulizwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…