Wanaume woooote ni ...........mdada usimwache laazizi wako kwa hili

kosa langu halifanyi kosa lako lionekane sawa/right
 
hapana nakataa
wanaume malaya ndio wengi zaidi sema utakuta mwanamkee mmoja anacheza na wanaume wanne so uwiano ni 1:4 wanaume na wanawake respectively

Huo uwiano wa 1:4 umeupata wapi? Usitumie hisia, tofauti ya wanaume na wanawake ni ndogo mno, si uwiano wa 1:4 (kama kweli unajua maana ya uwiano). Halafu unasema eti mwanamke mmoja anacheza na wanaume 4, huo ni uongo wazi. Wanawake wenye uwezo huo (wa kuwa na mabwana wanne kwa wakati mmoja ni wachache mno kama wapo). Ukweli ni kuwa mwanaume mmoja malaya amepitia wanawake lukuki na kwa msingi huo, waweza kusema wanawake ndo malaya zaidi.

Huo uwiano uliousema mara nyingi ni kinyume chake! Yaani mwanaume mmoja malaya, wanawake wanne malaya. Na kwa uwiano kama huu, wanawake malaya ni mara nne zaidi ya wanaume!!
 
nimegundua wewe unaibiwa mumeo kila mara na bila chenga (yaan anachukuliwa mbele yako) ndio maana unanijia juu kiasi hiki.

Sikujii juu ibali nakushangaa, umeshaniona nalalamika juu ya wanaume humu? Mungu kanifunda na nimefundika najua jinsi ya kuishi na mume wewe, kama anachukuliwa mbele yangu na mimi sijui kama anachukuliwa nina hasara gani mwanakwetu..niache kufurahia ndoa yangu eti nahisi mume wangu anaibiwa.....! No no sikuolewa kufanya hiyo kazi ya uchunguzi.......
 
Ni tangu lini umenijua wewe mtoto? acha uongo bhana...! Mimi ni mwaminifu sana.....! Yaani ukiniachia siendi kusema...!
kwa nini unatumia avatar ya radi/moto??????????
 


Thanx God,thanks button's back. Nakugongea mkuu,you deserve it.
 
hah.....hah.......hah
umenifurahisha sana
Mwanaume ukishamkubali usimfanyie uchunguzi manake atakutapisha ila kuwa wakati kwa coincidence unajikuta umejua na hapo watu wa roho kama zako watajifanya kumwacha mara vikao visivyo na maana kumbe wengine tumeshazoea
 
Mwe jamani kumbe wewe sio mzee, mi saa zote najua ni mzee, mbona sasa umekata tamaa mapema hivi?
sio kwamba nimekata tamaa ila nimeukubali ukweli mapema...waache wanaotafuta mwanaume wa kuwa wao peke yao
 

Mimi sina roho ya kuachana wewe mbona hunielewi? Nimeshakwambia toka mwanzo kwamba haachwi mtu Mungu hapendi jamani......
 
Wakuu natafuta dawa ya 'mshipa' wa kike. Anayejua inakopatikana anielekeze, kuna jinsia humu imezidi uchokozi, jamani!
 
Mimi sina roho ya kuachana wewe mbona hunielewi? Nimeshakwambia toka mwanzo kwamba haachwi mtu Mungu hapendi jamani......
kumbe tunafanana
hata mimi nimeapa simuachi kwa namna yeyote
 
"for every action, there is an equal and opposite reaction'. Kwa wanaojua fizikia, wanajua nnachomaanisha hapa
 
sio kwamba nimekata tamaa ila nimeukubali ukweli mapema...waache wanaotafuta mwanaume wa kuwa wao peke yao

Marytina nikuambie tu kuwa ukweli ni kuwa suala la mtu kufanya mapenzi ni la kibayolojia zaidi. Ni kweli kuwa kila wanaume wengi waliooa kuna wakati wanatamani kufanya mapenzi na mwanamke asiye mke wake... Hii inamtokea mwanaume (hata wanawake), mara moja, mara 2, mara 3,.... mara 100, na mara zote hizo kuna nguvu inamwambia usifanye hivyo maana unamkosea mungu, unamkosea mkeo, unahatarisha afya yako... Roho inataka lakini mwili ni dhaifu, kuna siku moja au mbili au tatu... au kumi kati ya hizo mia uzalendo unamshinda anajikuta kafanya. Ila usikatae kuwa kati ya wanaume kumi, kuna wawili, watatu, au hata saba watakaoweza kushinda hivovishawishi vya kusaliti ndoa zao... usikatae, lakini usiamini kuwa kila mwanaume anayesema humu kuwa yeye mwaminifu, basi ndiye mwaminifu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…