Wanavyuo, kwanini huwa mnaona noma kutaja majumbani kwenu?

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Good morning....
Enzi hizo naanza chuo nlikua nashangaa kila mwana chuo anasema kwao dar, mtu anaongea lafudhi yani kisukuma cha ndani kabisa huko mwamashimba ila ukimuuliza kwao anasema dar tena anajitahidi na kumix kidogo lafudhi ya dar mi naiita kuvunja nazi..... Hiyo mixer ya kisukuma plus kuvunja nazi sasa mweh!!!

Juzi nlikutana na masista duu wa chuo, tunafamiana wakawa wananiaga wanaenda likizo, wa kwanza nikamuuliza home wapi, akajibu naenda dar af kesho kutwa narudi, nikamuuliza kwanini unarudi soon akasema narudi afu ndo naenda home Arusha. Dar kunani huko nami nije? Mtu anaona noma kusema arusha kisa dar?

Wa pili sasa lol nae nikamtel safari njema home wapi, akajibu napita dar kwanza nisipoenda itakua lawama, Ha ha nkauliza tena so home wapi nkaona sura yake imenyong'onyea, imejaa wasiwasi, kwa sauti ya chini akajibu nikitoka dar naenda kigoma kwa mama nilijizuia tu kucheka ila kweli ilinichekesha sana.

Jamani dar kuna nini huko? Wahenga walisema mkataa kwao mtumwa. Wasomi tabia mbaya hiyo kwani ukisema kwenu mwamashimba kuna ubaya gani?
wanavyuo nawatakia likizo njema, BILA SHAKA WOTE MPO NDANI YA SHABIBY KWENDA DAR HAKUNA ALIEPANDA SARATOGA YA KIGOMA LOL
 
Ha ha ha kweli "education makes people more stupid"
watu wakifika chuo..wanaanza kubafilika na kutaka kufanana na kina mwajeii wa darslaam...hata km hana pesa anataka avaeeee...ajichubueee...anukieeee....aonekane wa tofauti..likizo naenda dar!..akienda bariad..wk tu akirud kachokaaaa...mweusii..mmmh kweli dar skuliiii
 
Yaeda ni kwa mama au kwenu 😀

Kote kuwili.....
Ila napenda zile frozen yoghurt za Smooch......na lobster wa Karambezi........
Wacha nikaandae shamba.......Dar nitakuja tu hakuna namna nyingine.........
 
Kote kuwili.....
Ila napenda zile frozen yoghurt za Smooch......na lobster wa Karambezi........
Wacha nikaandae shamba.......Dar nitakuja tu hakuna namna nyingine.........
Poa karibu, mie home dar, maeneo ya ngaramtoni unapanda gari za sakina
 
Sura ya sista duu wa kigoma haiondoki yani nacheka ka chizi lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…