Wanavyuo vikuu tusaidiane ni kweli kuna akili ndogo na akili kubwa?

Wanavyuo vikuu tusaidiane ni kweli kuna akili ndogo na akili kubwa?

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
192
Reaction score
23
Jana katika moja ya mijadala hapa mtaani Kinondoni Shamba, Jijini Dar, kulitokea mada iliyozua utata miongoni mwetu pale ambapo mtoa mada ndugu Jackson Joseph alizungumza kwamba kuna AKILI KUBWA na AKILI NDOGO. Akifafanua mada hiyo alianza kwa kutafasiri maana ya akili, harafu akaelezea vitu vinavyohusiana na akili, na mwisho akamalizia kwa kusema vitu hivyo ambavyo ni UJUZI, MAARIFA, na ELIMU ndiyo vinapima ukubwa na udogo wa akili ya mtu.

Alitafasiri AKILI kuwa ni uwezo wa mtu kufikiri na kutafakari kisha kupata njia au jibu la kutatua tatizo fulani au kumudu mazingira fulani. Alisisitiza kuwa watu watofautishe UBONGO na AKILI akasema ubongo unaweza kuukamata na kuuona lakini akili haikamatiki wala haionekani ila ni matokeo ya kazi ya UBONGO. Alifafanua kuwa ubongo wa mwanadamu awe mrefu au mfupi, mzungu ua muafrika, mwarabu au muasia, mweupe au mweusi unalingana.

Aliendelea kujenga hoja kwamba ubongo una sehemu zake kuu TATU fore brain (ubongo wa mbele), middle brain (ubongo wa Kati) na rear brain - medula oblangata (ubongo wa nyuma) ambavyo vyote kwa pamoja mtu huzaliwa navyo akiwa na uwezo wa kufikiria namna ya kumudu mazingira. Kadhalika alisema akili hiyo ya kuzaliwa nayo kila mtu inapopata ujuzi,maarifa, na elimu (formal or informal) zaidi kutoka kwa wenye navyo na kuweza kufikia ujuzi, maarifa elimu kwa kifupi uwezo wa kufikiria na kutafakari na kutatua matatizo kumudu mazingira kwa kiwango cha juu hapo mtu anaitwa ana akili kubwa.

Alitolea mifano kuwa hata hiyo akili ya kuzaliwa nayo kuna utofauti fulani ambao unapelekea mtu kubaki na akili ndogo mwingine kuwa na akili kubwa. Mtu anakuwa na uwezo mdogo wa uelewa (poor understanding ability) mwingine uwezo wa kati wa uelewa ( intemrmidiate understanding ability) na uwezo wa juu wa uelewa ( high or big understanding ability). Huyu mtu wa poor understanding ability mtoa elimu anatumia nguvu nyingi sana kumpatia elimu ya maarifa na ujuzi mbalimbali ili kumudu mzaingira,kitamaduni, kiuchumi kiafya,kisiasa nk mwisho wa siku uwezo wake wa kuyashika unakuwa na kikomo hata ufanye vipi hasongi anaishia kuwa na akili ya kawaida (ndogo)

Huyu wa intermmidiate(kati) unatumia nguvu kubwa kidogo si sana kama yule wa kwanza ananasa haraka na kuipokea ile elimu anakua na ujuzi, maarifa na elimu kubwa (kiutendaji achilia mbali vyeti). Na huyu ya kundi la mwisho Big understanding ability ndiyo miongoni mwao wanapatikana watu maarufu kwa jina la Genius - exceptional intellectual or creative power or other natural ability. Hapa mwalimu au mhadhiri hatumii nguvu kubwa kufundisha ni kugusa tu kitu kimelipuka. Kundi hili ndilo hupatikana maprofesa na madaktari wengi wenye uwezo mkubwa.

Hizi akili kubwa nazo zimegawanyika kuna mtu ana uprofesa wa mambo ya uchumi na mwingine ni udaktari wa mifugo, hapa hakuna ubishi wote wana akili kubwa japo kuwa kila mmoja wao hawezi fanya kazi ya mwingine. Pia mtu aweza kuwa injinia wa madaraja makubwa na barabara na mwingine ana uinjinia wa majengo au miundombinu ya maji hao wote wana akili kubwa hali kadhalika hakuna awezaye kuifanya kazi ya mwenzie aliyoisomea kumshinda yeye mwenye wa taaluma yake. Kundi hili mtu wa poor understanding capacity, panga pangua hawezi kufikia kiwango hicho cha taaluma na akili yake itabaki kuwa ndogo ukilinganisha na watu hao.

Na ukija kwa madaktari, mainjinia, maprofesa nk, mchumi kama Lipumba anaweza kuwa na uwezo mdogo wa kufikiria, kitabibu juu ya njia za kuokoa maisha ya ng'ombe ambaye anajifungua mtoto akiwa anatoka ndivyo sivyo kwa maana ya kwamba profesa Lipumba ana akili ndogo kulinganisha ya Daktari aliyesomea mifugo. Hali kadhalika daktari wa mifugo ana akili ndogo kwa mambo ya kiuchumi ukilinganisha na Profesa Lipumba.

kuna kundi fulani la majiniasi wachache upasuaji anaweza, ualimu anaweza, urubani wa ndege anaweza, meli anaongoza, gari anateneza na kuendesha nk. Panga pangua hawa wana akili kubwa sana huwezi pinga. Katika jamii tuliyonayo kuna watu ambao ni wengi asilimia 75 hawajui kitu wana akili ndogo sana hata kazi hawafanyi ni majungu kwenda mbele hivyo akili zao ni ndogo na ndiyo maana Tanzania tuko nyuma kimaendeleo.

Hata ukichukulia mfano kwa wanyama mbwa ana akili kubwa kuliko ya nguruwe lakini nyoka ana akili kubwa kuliko wanyama hao wote. (Akili ya mnyama wataalamu wanaiita SILIKA) Hivyo basi naomba ieleweke kuna AKILI KUBWA na AKILI NDOGO ndivyo alivyomalizia Bw. Jacksoni Joseph. Wadau naomba mchango wenu ni kweli kuna akili kubwa na akili ndogo?
 
me nipo wapi sijui.!But nachoelewa niko njiani kuelekea uprofessor so may be miaka mitano mbele ntakuwa na akili kubwa ......hope by this fact, it sounds well
 
ndiyo, kuna akili kubwa na ndogo na ndiyo maana ktk mitihani kuna wanaopata div one na wengine wanapata sifuri ili hali wanafundishwa na walimu wanaofanana
 
ndiyo, kuna akili kubwa na ndogo na ndiyo maana ktk mitihani kuna wanaopata div one na wengine wanapata sifuri ili hali wanafundishwa na walimu wanaofanana
ikiri

Asante kwa jibu lako zuri, Bw Luyungu unafikiria ni kwa nini wengine wana akili ndogo na wengine wana akili kubwa?
 
me nipo wapi sijui.!But nachoelewa niko njiani kuelekea uprofessor so may be miaka mitano mbele ntakuwa na akili kubwa ......hope by this fact, it sounds well

Ok then, Honorable Darius although it sounds well, na in five years to come utakuwa professor tusaidie kujua nini kinasababisha naturally watu kuwa na akili ndogo na wengine kuwa na akili kubwa?
 
me nipo wapi sijui.!But nachoelewa niko njiani kuelekea uprofessor so may be miaka mitano mbele ntakuwa na akili kubwa ......hope by this fact, it sounds well

Ok then, Honorable Darius although it sounds well, na in five years to come utakuwa professor tusaidie kujua nini kinasababisha naturally watu kuwa na akili ndogo na wengine kuwa na akili kubwa?
 
Nipo UDSM mleta mada Mr Jackson Joseph kama alifanyia utafiti, basi alifanikiwa kupata vitu muhimu ambavyo ni kweli kama alivyovielezea kwa kiwango kikubwa ni visababishi na uwazi kuwa kuna akili KUBWA na akili NDOGO. Hapa UDSM hilo liko wazi na lilipata mashiko zaidi pale ambapo Mchungaji Msigwa Mbunge wa CHADEMA aliposimama bungeni na kusisitiza kuwa kumekuwa na mwenendo mbaya kiuongozi wa nchi hii kutokana na akili ndogo ya viongozi wa serikali na CCM kuitawala akili kubwa watanzania wasio serikalini na viongozi wa upinzani hususani chadema walio na akili kubwa.
 
Ni kweli kuna akili ndogo na akili kubwa. Kuna wavumbuzi wa mambo ya kisayansi na fomula zao zinatumika mpaka leo mfano ni Galileo galilei, Newton, Achimedes, nk ambao ni mifano dhahiri walikuwa na akili kubwa! Leo hii tunaona akina Profesa Ibrahim Lipumba, Profesa Julius Mkomel, Dr David Mosafale wanakaa meza moja na wazungu kuchunguza na kupata solution za changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kiuchumi, kiafya nk.

Ni KWELI kuna akili KUBWA na akili NDOGO ni lazima tulikubali hilo. Angalizo, Mr Jackson endeleza kuwaelimisha kitaani KINO nchi hii tunahitaji akili kubwa vijana ndilo taifa la sasa. Wenzetu Kenya wamepitisha sheria Mbunge au gavana lazima awe na Degree ya vyuo vinavyotambulika (akili kubwa) wamefuta ile ya anaweza kuwa hata fomu four.
 
Back
Top Bottom