PreGE2025 Wanavyuo wa kampeni ya ‘mama asemewe’ wafanya matembezi, waweka maazimio uchaguzi mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Aibu sana kuwa na kizazi cha aina hii kisichokuwa na uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo! Yaani wamepewa hizo tshirts, wanaona tayari wamemaliza. Halafu baada ya kuhitimu masomo yao, wanaanza tena kulalamika hawana ajira!

Badala ya kupigania mabadiliko, wanakubali kudanganywa na hila za ccm kama walivyodanganywa wazazi/walezi wao miaka nenda kule vijijini kwa kuhongwa kanga, vitenge, vilemba, fulana, kofia, elfu 5, na vyakula ili kuichagua ccm!
 
Hawa ndio wanafanya graduate wadharauliwe sana na wanasiasa, mpaka kufikia hatua yakuambiwa wakigraduate waende VETA ilihali watoto wa hao wanasiasa wanaingizwa kwenye vitengo nyeti.

Baadala ya kuandamania huo ujinga ilipaswa kuona mnaandama kuishinikiza Serikali ionyeshe mipango madhubuti iliyoweka kwa miaka 20 ijayo juu ya future ya vijana wanaohitimu kwenye ngazi na kada mbalimbali.

Nilipaswa kuona hawa vijana wanaandamana kuishinikiza Serikali kuweka sera madhubuti kulinda ajira za wazawa.

Mambo ni mengi sana walipaswa kuandamania kwa maslahi yao na maslahi ya Taifa lao.
 
Mnaedit sana had mnaharibu
 
Wakiambiwa waende VETA wanapiga mayowe wakati hii elimu ya chuo haijawatoa ujinga kama huu upuuzi wanaofanya. Pumbavu kabisa.
 
Wanajua kama baada ya chuo wanaenda VETA? Halafu yanatia huruma
 
Sisi tupo huku veta tunawasubiri baada ya uchaguzi.
 
Wakimaliza kusoma wanarudi mtaani kutumikishwa na darasa la saba. Elimu ya Tz imeshuka kiwango sana.
 
Tunawasubiri mtaani ndio watakapoona hasara ya huo ujinga wanaoufanya leo. LISU piga spana hii mi chawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…