PreGE2025 Wanavyuo washiriki Kampeini ya Mama Asemewe; Tutaona mengi kuelekea GE2025

PreGE2025 Wanavyuo washiriki Kampeini ya Mama Asemewe; Tutaona mengi kuelekea GE2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Joined
Jun 26, 2024
Posts
41
Reaction score
57
Maelfu ya wanavyuo kutoka vyuo mbalimbali mkoani Dodoma wamefanya matembezi maalum kwa ajili ya kuweka maazimio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

1743314515720.png

Matembezi hayo yamefanyika chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama asemewe ya Ndg. Geofrey Kiliba, yakihusisha wanachama wa kampeni hiyo wanaounga mkono juhudi za maendeleo za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan .

Akizungumza baada ya matembezi hayo, Ndg. Geofrey Kiliba amesema kuwa lengo ni kuonyesha mshikamano wa wanavyuo katika kuchagiza maendeleo ya taifa na kuandaa mikakati ya kuhakikisha vijana wasomi wanashiriki kikamilifu kwenye uchaguzi ujao.

“Tunatambua mchango wa vijana katika ustawi wa nchi yetu, na kupitia Kampeni ya Mama Asemewe tunajipanga kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga Tanzania yenye maendeleo endelevu chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” alisema Kiliba.

Katika maazimio yao, wanavyuo wameeleza dhamira ya kushiriki kwa wingi katika mchakato wa uchaguzi, kuhakikisha ushiriki wa vijana unakuwa na nguvu, na kuendelea kueneza uelewa kuhusu sera na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita.
 
Hili Taifa linaweza kuja kukombolewa na wasio soma.


Walio soma wengi huishia kuwa machawa na walamba miguu ya wanasiasa...

No reform no Darby
 
Back
Top Bottom