GE2025 Wanawake 231 wamechukua fomu ya ubunge kupitia CCM. Ile kampeni ya kuwainua wanawake ndo imeanza kuzaa matunda?

GE2025 Wanawake 231 wamechukua fomu ya ubunge kupitia CCM. Ile kampeni ya kuwainua wanawake ndo imeanza kuzaa matunda?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wakuu
====
wanawake wengi wamejitokeza kuchukua fomu katika nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 idadi hii ni kubwa

Je? ni kweli ile kampeni ya kuwainua wanawake imeanza kufanya kazi au ni wanafuata mkumbo.

Maoni yangu

Tuangalie majimbo ambayo yalikuwa yanaongozwa na wanawake kimaendeleo yapoje? kuna utofauti na yale yaliyokuwa yakiongozwa na wanaume kama kutakuwa na utofauti basi wanawake wapewe nafasi na wajumbe ili kupunguza zile nafasi za viti maalum wanawake wapewe majimbo zaidi.

Wanawake hawataki tena kusikika tu, bali kuwakilisha, Wanawake wengi sasa wanatambua kuwa mabadiliko ya kweli yanahitaji ushiriki wa moja kwa moja katika vyombo vya maamuzi.

Au kwa sababu Rais wa nchi ni Female amefanya kuwashawishi kuwa Mwanamke anaweza kufanya zaidi ya mwanaume?

Idadi ya wanawake waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi za ubunge katika majimbo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefikia 231 hadi sasa, ikiwa imesalia siku moja kabla ya kufungwa kwa mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa makada hao.
1751439891593.png

chanzo: AzamTv​
 
Mwanamke chake ni kuzaa na kulea familia.

Haya mengine tunalazimisha tu.
 
Samia ameprove kama mwanamke failure kwenye uongozi so amewahamasisha failures wenzake kaziii kwelikweli
 
Naona ingependeza kama ungetujuza pia idadi ya wanawake waliochukua fomu za kugombea ubunge wa majimboni na wale wa viti maalum.
 
Back
Top Bottom