Wanawake acheni Kupiga Kikatili Watoto wenu kwani hamkulazimishwa Kuwazaa

Wanawake acheni Kupiga Kikatili Watoto wenu kwani hamkulazimishwa Kuwazaa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hakuna Kitu GENTAMYCINE nakipenda kama Watoto na Kucheza nao (japo ni Muoga wa Kuzaa) hivyo nikiona Wanaonewa au Wanateswa huwa Ninaumia mno na hata Mood ya Siku nzima Kuharibika.

Nimekutana na Mama Mmoja akimpiga mwanae wa Kumzaa Kofi ambalo hata Mtu mzima akipigwa lazima Vita Vitaanza kwa sababu ya Kipumbavu kabisa kuwa tokea Asubuhi hajaoga wakati hata Mimi GENTAMYCINE kwa Jicho langu Kali la Kinjagu / Kiupelelezi nimegundua hata Yeye (Mama Mtu) tokea aamke hajaoga.

Sikatai Watoto (Wanangu Kuadhibiwa) ila siyo Kikatili namna hii kwa Mihasira yako ya Mumeo Kukunyima Hela au Kukubandua vibaya au Kukosa Hela ya Marejesho ya VICOBA.

Kwa jinsi huyu Mama alivyonikera nimeshamkariri Sura na Mtaa anaokaa hivyo nitamvizia taratibu ili nione kama hiki alichokifanya leo alipitiwa tu kutokana na Hasira au ndiyo Kawaida yake ili kama ikiwa ni Kawaida yake basi Siku nikimgumia / nikimfuma anampiga kama hivi leo GENTAMYCINE nitamkata Bonge la Mtama kama ambao Juzi kati Nilimkata nao Bakari Malima (Jembe Ulaya) katika Mechi zetu za Veteran Viwanja vya Leaders Club.

Na nyie Wanaume Wenzangu wekeni tabia / Utaratibu wa Kisiri (Kimya Kimya) Kuwahoji Watoto wenu Kwani huenda kuna Wengine huwa Wanapigwa na Kuteswa vibaya kuliko hata huyu niliyemuona leo.

Inakera mno yaani Watoto mnawataka Wenyewe kwa Kutusumbua Usiku Kucha akina GENTAMYCINE tuwabandueni vyema ili muwapate na Wanamume tunahangaika na Kujipinda Kitandani Mimba iingie halafu mkiwazaa Mnatutesea Watoto Wetu.

Nachukia kuona Mtoto, Mzee, Yatima na Vilema wakiteswa, wakipigwa na wakinyanyasika na ukitaka ujue Hasira zangu Kali za Kizanaki na Kimakuwa zilivyo fanya kwa Hawa ndipo utanijua na utajua kwanini Nyoka hana Ugoko na kwanini Wimbo wa Taifa huwa hauna Kolabo.

Huyu Mama ameniharibia Siku Leo!
 
Ila Kuna mitoto mingine Ni mikorofi sijui ndo tabia za baba yao, halali Yake huyo kupigwa.
 
Maisha ya mama zetu wa kiswahili yamejaa na stress mno, hapo ana mkopo wa kukausha damu, ikifika alhamisi ana kikoba na marejesho sasa mtoto ukijichanganya kidogo tu, utaita maji mma [emoji28]
 
Back
Top Bottom