Wanawake acheni kuzaa na waume za watu ilihali waume zenu wapo

Wanawake acheni kuzaa na waume za watu ilihali waume zenu wapo

Hapo namba 1 nimekupata vizuri sana. Na shida nadhani ni umasikini.

Kuna siku nilienda mkoani hapo nikakuta kesi ya dada kutembea na mchungaji na kisha mumewe akajua mwanamke akawa mkali na mchungaji akisema kuna maono huyo mwanamke inabidi akakae kanisani ili kufukuza shetani anayeingia katika hiyo ndoa.

Ila sababu ni umasikini mchungaji anatumia sadaka na maombi feki kumhadaa mke wa mtu. Wanafamilia nao pande mbili zote wamekuwa kama misukule walirogwa.

Wanaona kabisa mwanaume anakosewa adabu na mkewe na anafanya umalaya na uhasi ila wanatoa macho na kutochangia chochote zaidi ya kumtazama yule mwanaume kwa macho ya huyu ni mchungaji usigombane nae sio vizuri.

Sasa yule mwanaume ukiomuona maisikini hadi anatia huruma. Ni wale vijana wa kijijini anaependa familia yake masikini na anapambana ili maisha yawe mazuri ila mkewe anamuangusha kupitia maswala ya imani na wana watoto wadogo.

Nikasema huyu kijana apate tu ujasiri tu achukue watoto awapeleke kwa bibi yao. Aondoke akatafute maisha mengine kimya kimya.
Duuh
 
Starehe ya maskini ni ngono na umasikini ukithiri huko vijijini
Hili ni fact, is why jamii ambazo hazijaendelea or maeneo ambayo umaskini umekubuhu, ngono na pombe ndio starehe kuu
 
Back
Top Bottom