Wanawake baada ya nywele tukumbuke na miguu pia

Wanawake baada ya nywele tukumbuke na miguu pia

Wanawake ni kundi lenye majukumu lukuki katika siku, pamoja na majukumu hayo usafi na urembo ni jambo muhimu pia.

Wanawake wengi wamekuwa wakizingatia zaidi nywele na uso huku wakiacha miguu na kucha zake vikibaki kwenye hali taaban,

Unakutana na mdada kasuka knotless kachora wanja wa lulu ila ukimtizama kucha za miguu zina weusi wa uchafu, kwa kweli inaharibu picha nzima ya urembo wake.

Wanawake tujitahidi kuikumbuka miguu yetu na kucha zake,tupake mafuta na kuiweka katika hali ya usafi hii inakamilisha maana nzima ya usafi na urembo.

Tips za kuweka miguu safi,

muda 30mnts
vifaa
beseni
maji ya vuguvugu
sabuni ya maji(shampoo)
nail cutter
nail file
msasa
kibrush cha kucha
chumvi ya mawe au asprin
mafuta ya maji

maandalizi
weka kwenye maji,aspirini au chumvi ya mawe na sabuni

kata kucha zako na kuzifile

loweka miguu yako kiasi 6-10mnts sugua kwenye visigino kwa kutumia msasa na kwenye kucha kwa kutumia brush

tumia nailfile kuondoa uchafu pembezoni mwa kucha .

ukiwa tayari kausha miguu yako na upake mafuta.

kwa wasiopenda rangi waweza kutia henna na kucha zako zikabakia na urembo wa asili.

View attachment 1739344

karibuni kuongezea tips mbalimbali za utunzaji wa miguu..

.View attachment 1739345View attachment 1739346View attachment 1739346
Hii nzuri [emoji120]
 
Acheni mkorogo jamani. Aliyetupa rangi yetu hakukosea. Hii rangi inasaidia kwetu sisi tunaokao sehemu zenye jua kali. Ona hii miguu sasa - ni binadamu huyu kweli?

1625123664749.png
 
si tulikubaliana ni unywele na kauso tu au? sasa uko miguuni uyo mtu atakuwa anatafuta nn
 
Back
Top Bottom