Wanawake baadhi wana mikosi ukikutana nao nyota yako ya hela inapotea

Wanawake baadhi wana mikosi ukikutana nao nyota yako ya hela inapotea

Inaweza kutokea labda upo neutral tu huna hzo baraka wala mikosi?

Kuna namna nyingi ya kudetect hzo baraka/mikosi ukiachana na kusex?
Nope, kila mtu anazo baraka zake.
Ina tegemea na sehemu au application yake Ina fanya kazi vipi.

Yap, ukiacha sex, Kuna ile kukutana na watu asubui.
Mwingine aki kutana na Mwanamke face to face.
Basi mambo lazima yadamsh.

Sawa sawa na mwanamke akutane na mwanaume asubui.
 
Sio lazima, ila mtu ana paswa aji tathimini ili kujua.
Au Kuna Ile kitu Wana ita chemistry ehh🤣, mkikutana, kufanya kazi, au hata story mambo lazima šŸ”„šŸ”„
Mhh ngoja niendelee kusoma comments mm bado sijaona athari ya haya mambo kwangu naona ninyandue nisinyandue nikutane nisikutane mambo mengi ni mule mule
 
Naomba kushiriki ktk mjadala huu

Haya mambo yapo, ktk ukanda huu waa mipaka inayopatikana mkoani kagera haya mambo yapo Sana hasa kwa wanawake wanaotoka ktk kabila la wanyarwanda waliokimbia vita.

Wanyarwanda wengi waliojikuta maeneo ya karagwe na Uganda hasa ile jamii ya wa tutsi wamejikuta na hii kadhia ya mikosi.
nitatoa Mikasa mmoja ambao ulitokea kwa marafiki wawili waliolala na Dada mmoja mwenye sifa ya mikosi.
Ilikua hivi: Kwanza kabisa huyo Dada ni mzuri Sana kwa muonekano kuanzia sura, height na shape, hakuna mwanaume rijali anaweza muona alafu asimtamani.

Jamaa wanafika mpaka kati ya Uganda na Tanzania anapoishi huyo bi Dada hawa mbali na kua marafiki lkn pia alikua mtu na boss wake.
Boss kuna ford (zero km) amegiza, chombo imefika dar Sasa inabidi iendeshwe hadi hapo mpakani walipo ili atakapovuka upande wa pili atumie chombo mpya, na kweli chombo ikafika wadau wanakula bia chombo ikapokelewa border.
Huyu mwingine yy yaani mwenzake na boss kuna mzigo anasubiria hapo mpakani ili uvuke uingie nchini lkn wakati huo mifumo bado haiko na nguvu kwa hiyo ni mwendo wa magendo.
Tukio likaanza huyu mwamba wakusubiria mzigo akaomba atafutiwe demu mkali na kwa gharama yoyote mtoto akaletwa jamaa wote udenda unawatoka hadi machawa,,, dalali kakabidhiwa 3m kwa ajili ya demu na yy kapewa miatatu yake kama dalali.
Kumbe bhana boss anaetakiwa kuvuka nae kampenda mtoto hapa ndo kila kitu kilipoharibika.
Hotel wamefikia moja wameenda kulala huyu mwenye demu kaingia room kwake na boss nae kaingia room kwake, majira ya kumi alfajiri anamwamsha boss wake kua anawahi kuona gari maana ameambiwa kuna shida japo walikua wameshavuka.

Baada ya kutoka room na boss kujiridhizisha kua mwamba ametoka, ikabidi na yy agonge kwa mtoto ili ajilie tunda kweli mtoto hakua na makuu akakubali kufungua na mwamba nae akala tunda, walikuja kusimuliana asubuhi na hawakuamini.

Huyu bwana mzigo aliokua anasubiria ulikua ni SPIRIT kwa ajili ya kwenda kutengenezwa pombe Kali gari imekula mzinga na tayari ipo mikononi mwa TRA kwa ajili ya penalty lkn pia hasara ya mzigo wote, huyu mwamba wa kuvuka yy alikula mzinga na gari lake jipya likiharibika vibaya Sana pasipo yy kupata hata jeraha, Sasa huyu wa spirit akamuuliza au nilivyotoka na wewe ulipiga mbona hizi ajali sio za kawaida jamaa akamwambia ndugu yangu nami nilipiga ulivyochomoka, huyo Dada aliogopwa kama ukoma na kuna matukio mengi ya watu waliotembea nae kukutwa na majanga ya kufirisika na hata kupoteza kazi.


sio huyo tuu wapo wengi Sana ila kwa leo naomba niishie hapo.
 
Wana Jf..

Nakumbuka miaka ya 2012-2016 nilikua na upepo mkali sana wa hela, yani kama ni hela nilichezea sana ingali bado kijana mdogo sana na mademu nilikua na wafungia vioo ni mimi mwenyewe mwenyewe polepole tuu akili yote kwenye hela sikutaka kabisa stress za mademu japo hela nilikua nayo ya kutosha sana kuwapanga foleni ila sikutaka kabisa

Nakumbuka mademu zangu walikua ni nyagi, hela, na wine za kila aina. Nikitoka mishe napitia bar na lewa weee na kurudi gheto kuegesha fuvu, siku nisipo pita bar napita kijiwe cha kahawa nacheza draft kidogo na masela then gheto kukazia na movie na ma-game mpaka night kali sana

Sasa mwaka 2017 akajitokeza mwanamke mmoja sijui alitokea wapi nikajikuta na mtongoza akawa mpenzi wangu wakuu tokea hapo nikaanza kuumwa umwa hovyo hovyo na kulazwa pasipo kuonekana ugonjwa wowote ila ni kuswet mpaka na konda na kukonda

Nilikaza fuvu hivyo hivyo kuwa nae nikaanza kukosa madili ya hela, dili zangu za kusafirisha nguruwe kwenda dar zikagonga mwamba na kuhamia kwenye kununua dhahabu na kuuza ila nako zikawa zina sua sua, nikawa naona hapa mambo hayajakaa sawa kama na chezewa vile, baadae masela wakanambia nikachek nyota nikagoma ila tuu na waeleza na mashaka na huyu mpenzi wangu mbona kabla sijawa nae sikua hivi nikaja kumpiga chini huyu demu.

Baada ya kumpiga chini nikasema na dhahabu na piga chini biashara hii itanitoa roho, nikahamia kwenye kununua ndizi na kupeleka dar fuso kwa fuso, then na viazi na toa huko napeleka dar, huku nikaweka wakala wa mayai dodoma. Fuso ikitoka kupeleka ndizi dar inapitia dom kushusha trei za mayai za kutosha. Mimi nilikua silali ni mimi na barabara tuu , mzee wangu alikua mjeda vyeo vya juu sana ( majina kapuni) hivyo nilitembelea pia cheo chake maana alikua anajuana na wakuu wengi sana.

Ndugu nikaja okota demu mwingine 2019 yani hapa ndiyo nikaharibu kabisa kabisa..

Ndugu mpaka sasa ni mimi na wanawake ,pombe na mishe za hela naona zinasua sua sana ila nakaza hivyo hivyo japo kiukweli kuna muda na fikiria kabisa kama siyo kujiingiza kwa mademu nisinge tetereka ni mara mia ningetafuta demu mmoja nioe badala ya kupuyanga puyanga.

Nimejionea mwenyewe wanawake baadhi wanamikosi na ukikojoa ndani ndiyo una haribu kabisa kabisa.

Sasa kazeni mafuvu.

Mwanamke yeyote anayegongwa na zaidi ya mmoja automatically anakua na mikosi.
 
Mwaka 2012-15 nilikuwa vyema kiuchumi mpaka nilipolala na dada mmoja aliyekuwa akiuza uji nje ya duka langu ndipo mambo yakaharibiki kwa harakaharaka kama vile sio mimi yule wa siku zote.

Kwanza kesho yake tu nilikoswa na ajali kubwa alafu wiki ileile wakavinja dukani kwangu wakaiba kila kitu hadi panga lililokuwa nyuma ya friji.

Sio muumini wa haya mambo ila nabaki najiuliza tu au inawezekana kuna watu wenye mikosi kweli?
 
Summary:

Negativity towards women's
Inferiority complex
Depression
Fear
Paranoia
Insomnia
Mental health issues
Too much emotionality

Reference:- Trust Me Bro
Mwenzako kafanya practical kuchovya chovya kapata matokeo.

Sasa wewe unapingana naye huku umejituliza kama kasuku nyuma ya keyboard.

Emb tanga na njia uone mabalaa yatayokukumba halafu uje urejee jukwaani kutuweka sawa.

Wanaoshuhudia hayo usidhani wana mapungufu ya akili ama wana sonona.

Dunia hii baba imejaa mambo yaliyoficha kuliko yanayoonekana kwa macho ya nyama.
 
Back
Top Bottom