Jackal
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 9,971
- 13,608
Mimi na mke tumekuja kipindi hiki huku kijijini Arusha.Nyumba yetu ya huku kijijini bahati nzuri umeme wa REA umepita karibu,ule wa elfu 27 tukawa tumevuta.Nilipoenda Tanesco nilijiandikisha kama mtumiaji mdogo ,Tariff 4,Yaani matumizi yangu hayazidi 9,500/- kwa mwezi napata unit 75,sitakiwi kuzidisha.Sasa nimekuwa conscious kwenye matumizi kuhakikisha vitu vinavyowashwa km Jiko la umeme,fridge,pasi n.k havipitilizi hayo matumizi ya umememe unit 75,kwa mwezi.Katika kudhibiti matumizi ya umeme,nimetafuta vyanzo vingine vya nishati km Solar,Jiko la gas,jiko la mafuta ya taa,jiko la mkaa,jiko la maranda ya mbao,Jiko la kuni n.k
Mke wangu hajapenda jinsi ninavyodhibiti matumizi ya umeme,sasa amuamua kila kitu anakibandika kwenye kuni,hata kama hicho kitu ni rahisi kuiva na hakitumii umeme mwingi.Mfano Leo asubuhi kanipashia ndizi na kupika chai kwenye jiko la kuni,yaani vinanuka moshi.
Mimi nilishamfafanulia kwamba kama kitu hakili umeme sana,basi tumia tu jiko la umeme ,jiko la gas au jiko la mafuta,kuokoa muda.Vitu vyenye kula umeme mwingi ,kama maharage au makande,ndio tumia kuni,mkaa au maranda ya mbao.
Wadau wengine mliooa hapa JF na nini mnashuhudia vitimbi vya wake zenu?
πππ
Nawatakia Eid El Adha,Kwenu Mullars na Ayotollars wote