Wanawake Bhana!

Wanawake Bhana!

Jackal

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
9,971
Reaction score
13,608
Mimi na mke tumekuja kipindi hiki huku kijijini Arusha.Nyumba yetu ya huku kijijini bahati nzuri umeme wa REA umepita karibu,ule wa elfu 27 tukawa tumevuta.Nilipoenda Tanesco nilijiandikisha kama mtumiaji mdogo ,Tariff 4,Yaani matumizi yangu hayazidi 9,500/- kwa mwezi napata unit 75,sitakiwi kuzidisha.Sasa nimekuwa conscious kwenye matumizi kuhakikisha vitu vinavyowashwa km Jiko la umeme,fridge,pasi n.k havipitilizi hayo matumizi ya umememe unit 75,kwa mwezi.Katika kudhibiti matumizi ya umeme,nimetafuta vyanzo vingine vya nishati km Solar,Jiko la gas,jiko la mafuta ya taa,jiko la mkaa,jiko la maranda ya mbao,Jiko la kuni n.k

Mke wangu hajapenda jinsi ninavyodhibiti matumizi ya umeme,sasa amuamua kila kitu anakibandika kwenye kuni,hata kama hicho kitu ni rahisi kuiva na hakitumii umeme mwingi.Mfano Leo asubuhi kanipashia ndizi na kupika chai kwenye jiko la kuni,yaani vinanuka moshi.

Mimi nilishamfafanulia kwamba kama kitu hakili umeme sana,basi tumia tu jiko la umeme ,jiko la gas au jiko la mafuta,kuokoa muda.Vitu vyenye kula umeme mwingi ,kama maharage au makande,ndio tumia kuni,mkaa au maranda ya mbao.

Wadau wengine mliooa hapa JF na nini mnashuhudia vitimbi vya wake zenu?
😀😀😀
Nawatakia Eid El Adha,Kwenu Mullars na Ayotollars wote
 
Wanawake wanachangamoto sana...ukipata mwanamke ambaye sio muelewa waswahili husemwa wa Nongwa ni shida hataki kuelekezwa..
Mpe kitimoto tena huo ndio ubavu wako...
Ukiwapa wanadamu wakushauri utampoteza mkeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hapa mkuu nimekunywa chai vizuri kama hakuna tatizo,na hatuna kinyongo Ila ndio yaliyotokea mkuu TZLEO!
 
Ndizi zimeletwa mezani zinanuka Moshi mm nasusa kula!!!!
Dawa ya moto sio moto Bali ni maji.Nilichokiangalia ni gharama IPI kubwa ,kati ya kususa ili tuanzishe vurugu au kula ili amani itawala asubuhi hii ili niendelee na shughuli zangu kwa amani,mkuu Lwasu.
 
Mkuu Baba S labda na Mimi nianze huo mchakato wa kujipikia,manake amri zangu naona zinawakwaza watu[emoji23][emoji23][emoji23]
Unakosea unaposema "Amri Zangu"....

Huwezi kumpa Mke Amri , mpe maagizo, taarifa, mwelekeze kwa Upendo.

Hata Mimi ningekufanyia makusudi iwapo utakuwa unani Amrisha vitu.

Hamishia gharama za nishati nyingine uongezee kwenye Umeme na Gas, hayo mazagazaga mengine yatumike wakati wa emergency tu.

Ni mawazo yangu tu.[emoji4][emoji4]
 
Dawa ya moto sio moto Bali ni maji.Nilichokiangalia ni gharama IPI kubwa ,kati ya kususa ili tuanzishe vurugu au kula ili amani itawala asubuhi hii ili niendelee na shughuli zangu kwa amani,mkuu Lwasu.
Sasa mtu anakuletea ndizi zinazonuka Moshi kesho akikuletea ugali usioiva je utaendeleza amani ndani ya nyumba??
 
Kwani gesi imeisha jamani,maana kupikia jiko la umeme gharama kweli na mkiishi pamoja mnahitaji kuwa na bajeti nzuri sio kukomoana,mueleze ukweli aelewe maana kama anakukomoa au gesi hakuna na mkaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes mama Sabrina, gas imeisha toka juzi,kwa hiyo nilimwambia apikie jiko la umeme km vitu vyepesi na jiko la mkaa au maranda kama kuna vitu vigumu vya kuiva.Jiko la maranda lina moto mkali kama wa gas na gharama yake ni rahisi sana.Gunia zima la maranda,kiwandani nanunua 1000 tu,na linatumika mwezi mzima,na halina Moshi kama jiko la kuni.Yeye hizo ndizi na chai angetumia umeme wala kusingekuwa na shida,manake haizidi dakika 10 kutayarisha!
 
Inaonekana una bajeti kali sana unamuambia kila saa sasa nadhani hapendi,jaribu kuwa unaongea mara moja tu na usifatilie sana mambo ya jikoni unamkwaza ,we uliweka jiko la umeme la nini humo ndani [emoji23][emoji23],unaonekana mpanga bajeti sana na mkeo mbishiii [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mtu anakuletea ndizi zinazonuka Moshi kesho akikuletea ugali usioiva je utaendeleza amani ndani ya nyumba??
Mimi mindset yangu,nilishavuka kwenye kukwazika kwenye mambo madogo km chakula.Ningekuta kapinga amri yangu kubandika chakula kigumu kwenye umeme hapo tungekorofisha.Hizo ndizi nilizokula na chai sio issue.Soon nitaelekea mnadani kwenye nyamachoma😂😂😂
 
Back
Top Bottom