Kumbe imepitishwa kuwa mabeki tatu wengi wanapendeza kuwa mazombie
Mkuu imenenwa mwanamke mwerevu hujenga nyumba yake mwenyewe na mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake mwenyewe (nisamehe kama sijaweka vizuri kauli yenyewe) lakini kifupi ni kwamba mwanamke atakuwa ni mjinga akikubali kuwa na housegirl aliyemzidi uzuri, au aliyemzidi hekima au aliyemzidi busara-ni muhimu mama mwenye nyumba akawa mbele tena kwa mbali kwa kila kitu dhidi ya housegirl
Utakuta mkeo kawaagiza mashosti na ndugu zake anatafuta binti wa kazi wa ndani wakiletwa zaidi ya mmoja anachagua asiye na mvuto kuliko wengine eti ili asije akamuibia mumewe.Yaan hawa viumbe hawajiamini kabisa hii nimeona kwa dada yangu alipoletewa wasaidiz zaidi ya watatu
@Mbu anaendeleaje?Huu usemi wa mwanamke mwerevu sijui mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe nadhani unaapply na kwa wanaume pia! Kwani nyumba haijengwi na mwanamke peke yake.
Usemi huu mie nauchukuliaga kama ukandamizaji kwa wanawake! Yaani kumtaka awe mvumilivu tuuuu no matter what kisha asiivunje nyumba na kuitwa mpumbavu!!