Wanawake hawapendi cost sharing?

Wanawake hawapendi cost sharing?

anampenda sana ndo mana HATAK AMWACHE AENDE MOTON kwa kutowajibika kulipa bili zote km maandiko yanavyosema..MWANAUME NI KICHWA....na amtunze mkewe.

Jamani mbona unaniwahi kila mara.. nakuunga mkono 100%. Nasema tena 'sipendi cost sharing'
 
Tumejigaramia sana kabla ya mtoko. Saluni, kokonko mpya, pamba ya kimtoko, nimekodi kibajaji kukufata. Bado tu unataka tushee cost wakati mwenzio hata nauli ya kurudia sina.
Hebu onesha uanaume bwana.
Mwanaume hasifiwi sura. Alaaaa!
 
mmh BB wee ni bahili unaonyesha yaani unataka hadi kiingilio cha club iwe ni cost sharing????? we ni kiboko dah...hivi siku Mungu amekujalia mihela unaweza kweli kumnunulia gari ur wife bila yeye kuchangia hata shilingi kisa tuu na yeye anafanya kazi???wanaume wa siku hizi mnabore sana mbona mnakwepa majukumu yenu??? ukiwa namsichana au mke mfanyakazi unataka kila kitu 50% jamani hamjaumbwa hivyo sasa utakuwaje kichwa cha nyumba kama kodi ya nyumba mnalipa nusu kwa nusu,ada za watoto shule mlipe nusu kwa nusu kwa nusu, huyu akilipa maji wewe umeme,bado hapo utataka mwanamke ajimaintain mwenyewe kwa mavazi na cosmetics ....aaiii sasa uanaume wako uko wapi? kwenye ku-do tuuu?????
 
Back
Top Bottom