Wanawake hawawezi kununua Mkuyati

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Wanawake wana matarajio makubwa karibu katika kila eneo linalohusu maisha yao, lakini inapokuja kwenye tendo la ndoa, mambo ni tofauti sana. Kwa nini? Ni kwa sababu, wanawake wengi ambao hawaridhishwi na tendo la ndoa kwenye uhusiano wao huwa wanafanya siri. Bila kujali liko kwao au kwa waume zao, wanawake hufanya siri kutoridhika kwao kimapenzi. Huweka siri kwa waume zao na hata madaktari.Ndio maana wateja wa wauza dawa zinazohusiana na tendo la ndoa (Mkuyati) ni wanaume.

Siyo kwamba, hakuna idadi kubwa yawanawake wenye matatizo ya udhaifu wa tendo la ndoa, hapana. Ni kwamba, kwa wanawake, matatizo yanayohusiana na tendo la ndoa huwa hayapewi kipaumbele. Kuna wakati wanaume wanaweza kuwa na ugumu wa kujua kwamba, wake au wapenzi wao hawaridhiki kimapenzi, kwani wanawake huwa hawasemi kuhusu matatizo hayo.

Kwa wanaume ni tofauti sana. Wanapokuwa na tatizo na tendo la ndoa huo unakuwa ni mgogoro halisi, kwani hupewa kipaumbele sana. Ni wepesi sana kukimbilia hospitalini au kwa wauza mitishamba ili kutafuta tiba ya tatizo hilo. Kwa wanawake hali ni tofauti, huwa hawafanyi hivyo. Wanawake ni wepesi kuomba ushauri au kuwasimulia mashoga zao kuhusu matatizo ya ndoa zao. Ni pale tu watakapochokozwa, ndipo wanapoweza kusema kwamba, maisha yao ya tendo la ndoa na waume zao hayako barabara. Hilo kwao halipewi uzito wa juu, au naweza pia kusema, hufanywa siri.

Ukiona mwanamke anatangaza sana kutoridhishwa kwake na tendo la ndoa, ujue huyo na mumewe wako kwenye uhusiano mbaya sana. Anatumia maelezo ya kutoridhika kwake, kama adhabu kwa huyo mumewe. Lakini wale walio kwenye ndoa imara, ni vigumu kusikia mwanamke akisema kuhusu kutoridhika na tendo la ndoa kwenye ndoa yake. Kushindwa huku kusema kutoridhishwa kwao kunatokana na namna jamii ilivyomfunga mwanamke kutoonesha kuhitaji tendo la ndoa.

Kwa miaka mingi jamii imemfundisha mwanamke kujifanya kwamba hahitaji jambo hilo, na pale anapoonesha kwamba, analihitaji, huitwa Malaya.
Wanawake kwa hali hiyo wamekuwa wakijali na kuvipa umuhimu vile walivyosisitizwa na jamii kuwa ndivyo vinavyowahusu. Shughuli zao na familia ndicho kipaumbele chao. Lakini, bila shaka umefika wakati sasa, wanawake wanatakiwa kuwa huru kuhusu tendo la ndoa. Badala ya kuacha wawe washirikishwaji, inabidi wawe washiriki.
 
Ah, labda wengine mwenzangu mie namwambia mumewangu kama sijatosheka au leo tubadili mtindo, usipokua muwazi utajikuta una hesabu boriti za nyumba mwenzio anakoroma.
 
Umejibu tuhuma kuwa wadada wamekupa rushwa mzee ili usimwage materio jukwwani..?
Asante kwa elimu......
 
Mtambuzi unaendeleaje na kuumwa?

Mwanangu, nilikuwa naendelea vizuri, lakini haya mawingu na hivi vyuma vilivyowekwa mkononi, ninasikia maumivu ya ajabu, hapa natumia pain killer, lakini wapi!
 
Mkuu wanaume wengine kwa kweli hawajui mapenzi,
yeye atatoka huko na ma ny e g yake,
atakuta umelala atachomeka nani yake,
hata dakika bado yeye tayari,
na mida mida huyo anakoroma,
jamani kweli nasema wanaume wengine ni noma.
 
Mwanangu, nilikuwa naendelea vizuri, lakini haya mawingu na hivi vyuma vilivyowekwa mkononi, ninasikia maumivu ya ajabu, hapa natumia pain killer, lakini wapi!

pole sana mkuu , naamini utapona maadam umeshapata matibabu ..
mkuu wanawake hawatumii mkuyati ila wao hutumia kungu kulegeza maana wakitumia mkuyati hawatafika hata robo ya safari
 
hayo mambo mbona ni ya kizamani sana, eti upige kimya huku unateseka. me namchana jamaa laivu kama hanifikishi. kuzungumza ndo kuelewana.
 
hayo mambo mbona ni ya kizamani sana, eti upige kimya huku unateseka. me namchana jamaa laivu kama hanifikishi. kuzungumza ndo kuelewana.

Miaka ya nyuma ulikuwa huwezi kumwanza mwanaume,
wewe unabana kimya tu.
 
Mwanangu, nilikuwa naendelea vizuri, lakini haya mawingu na hivi vyuma vilivyowekwa mkononi, ninasikia maumivu ya ajabu, hapa natumia pain killer, lakini wapi!

pole sana baba, nitakuja kukuona panapo majaliwa.
 
Ah, labda wengine mwenzangu mie namwambia mumewangu kama sijatosheka au leo tubadili mtindo, usipokua muwazi utajikuta una hesabu boriti za nyumba mwenzio anakoroma.

Off topic: kumbe wewe ni mwanamke? Siku zote najua dume....lol
 
ha ha ha,kutambua jinsia humu jf ni simple sana angalia tu comments za watu utawajuwa tu mzee wa katavi
Ahahahaah!! Ila kuna midume humu inajitahidi kweli kujibadili jinsia na inafanikiwa kweli.
 
Baba yake cantalisia mbona haujajibu majibu yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…