Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Wanawake wana matarajio makubwa karibu katika kila eneo linalohusu maisha yao, lakini inapokuja kwenye tendo la ndoa, mambo ni tofauti sana. Kwa nini? Ni kwa sababu, wanawake wengi ambao hawaridhishwi na tendo la ndoa kwenye uhusiano wao huwa wanafanya siri. Bila kujali liko kwao au kwa waume zao, wanawake hufanya siri kutoridhika kwao kimapenzi. Huweka siri kwa waume zao na hata madaktari.Ndio maana wateja wa wauza dawa zinazohusiana na tendo la ndoa (Mkuyati) ni wanaume.
Siyo kwamba, hakuna idadi kubwa yawanawake wenye matatizo ya udhaifu wa tendo la ndoa, hapana. Ni kwamba, kwa wanawake, matatizo yanayohusiana na tendo la ndoa huwa hayapewi kipaumbele. Kuna wakati wanaume wanaweza kuwa na ugumu wa kujua kwamba, wake au wapenzi wao hawaridhiki kimapenzi, kwani wanawake huwa hawasemi kuhusu matatizo hayo.
Kwa wanaume ni tofauti sana. Wanapokuwa na tatizo na tendo la ndoa huo unakuwa ni mgogoro halisi, kwani hupewa kipaumbele sana. Ni wepesi sana kukimbilia hospitalini au kwa wauza mitishamba ili kutafuta tiba ya tatizo hilo. Kwa wanawake hali ni tofauti, huwa hawafanyi hivyo. Wanawake ni wepesi kuomba ushauri au kuwasimulia mashoga zao kuhusu matatizo ya ndoa zao. Ni pale tu watakapochokozwa, ndipo wanapoweza kusema kwamba, maisha yao ya tendo la ndoa na waume zao hayako barabara. Hilo kwao halipewi uzito wa juu, au naweza pia kusema, hufanywa siri.
Ukiona mwanamke anatangaza sana kutoridhishwa kwake na tendo la ndoa, ujue huyo na mumewe wako kwenye uhusiano mbaya sana. Anatumia maelezo ya kutoridhika kwake, kama adhabu kwa huyo mumewe. Lakini wale walio kwenye ndoa imara, ni vigumu kusikia mwanamke akisema kuhusu kutoridhika na tendo la ndoa kwenye ndoa yake. Kushindwa huku kusema kutoridhishwa kwao kunatokana na namna jamii ilivyomfunga mwanamke kutoonesha kuhitaji tendo la ndoa.
Kwa miaka mingi jamii imemfundisha mwanamke kujifanya kwamba hahitaji jambo hilo, na pale anapoonesha kwamba, analihitaji, huitwa Malaya. Wanawake kwa hali hiyo wamekuwa wakijali na kuvipa umuhimu vile walivyosisitizwa na jamii kuwa ndivyo vinavyowahusu. Shughuli zao na familia ndicho kipaumbele chao. Lakini, bila shaka umefika wakati sasa, wanawake wanatakiwa kuwa huru kuhusu tendo la ndoa. Badala ya kuacha wawe washirikishwaji, inabidi wawe washiriki.