Wanawake huko GOMA, washindwa kurejea makwao wakihofia kubakwa

Wanawake huko GOMA, washindwa kurejea makwao wakihofia kubakwa

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Baada ya mji wa Goma,mashariki mwa Jamhuri ya kidemokalasia ya Congo, wakimbizi waliokuwa katika maeneo ya jirani na Goma, walihamasishwa kurudi majumbani kwao, na kuhakikishiwa usalama wao.

Waliotoa taarifa, wamesema mpaka sasa wana usalama wa kutosha,japo hawana imani kama hali hiyo itaendelea. Mjini Goma, wanasema hakuna tena vibaka, wanajeshi waliokuwa wakiwapora raia mali zao na vitu vya thamani hawapo, kwa ujumla hakuna alie na hafu na jeshi la M23 mjini humo.

Lakini, baada ya kambi zao kusafishwa na makazi ya wakimbizi hao kuondolewa, wamekuwa wakionekana wanawake hasa wajane, wanaokaa maeneo ya makanisani au majengo mabovu. Wakiongea na vyombo vya habari, walisema matukio ya mara kwa mara waliyokuwa wakiyaona, baada ya M23 kufika Goma, hayapo tena.

Lakini wamesema bado hawawezi kuwa na uhakika wa usalama wao, na kwamba huenda hata M23 ikawa na tabia ya ubakaji kama ilivyokuwa kwa jeshi la seriakali.

Umoja wa mataifa, katika ripoti yake inayohusu mapigano makali yaliyopelekea mji wa Goma kuangukia mikononi mwa M23, umetuhumu pande zote kuhusika na ukiukwaji haki za kibinadamu. Jeshi la Congo pia limehusishwa na vitendo vya ubakaji, ambapo ripoti hiyo imesema iliweza kupata wanawake 50 waliobakwa na wanajeshi hao wa FARDC.
 
Back
Top Bottom