Wanawake huwa mnajisikiaje katika hili?

Wanawake huwa mnajisikiaje katika hili?

Sheffer95

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2020
Posts
211
Reaction score
515
Kwanza nianze kwa kuwapongeza kwaajili ya siku ya Akina mama wote, pili niwashukuru wanawake wote kwa mioyo yenu ya upendo, uvumilivu, kujali na kila kitu. Ninyi ni mama, dada,wadogo pamoja na wake zetu

Ni hivi huwa mnajisikiaje pale tunapokuwa tumewadanganya na majanga yakatukuta na ikabidi nyinyi mje kutuuguza labda. Mfano unakuta nimekudanganya naenda safari ya kikazi mkoa labda Dodoma, then napata labda ajali labda Arusha au nimefumaniwa huko na kupigwa vibaya na niko katika hali mbaya na unakuja kuchukua simu yangu unakutana na mambo mengi ya kufedhehesha

Hivi ukiwa unaniuguza huwa mioyo mwenu mnajisikiaje au huwa mnatuwazia nini?

Ningependa kufahamu kuhusu hilo tu ahsante🙏🤲
 
Unajua nini mkuu umeuliza swali la msingi sana Daah ningependa kusikia hoja zao ngoja tuwasikilize

Kuna siku niliandaliwa ambush guest huko mkoani huko kwa hawa wasukuma nilikuwa na mwanafunzi , baba mtu akiwa na wadogo zake wawili wa kiume walitaka wavunje mlango watu walijazana nje sema walizuiwa polisi ndio walikuja kunitoa kuepusha ugomvi pale kipindi hicho naishi na huyu mwanamke sogeza tuishi ila alichangia pia ktk juhudi za mimi kutoka plus kuniletea msosi lock up Ila nashukuru Mungu ⁦⁩[emoji119] lile tatizo sijui liliishaje ndani ya siku tatu nilitoka japo mfuko ulitoboka nilikuwa nawaza pale nikivaa sare za njano na upara sijui itakuwaje

Sasa pamoja na kosa langu huyu mwanamke alisimama na mimi sijui kwenye kichwa chake aliwaza nini
 
Kama hamjali mnauguza ya nin sasa?
Kwa kawaida mwanamke anapenda kudanganywa yan uongo unaofanania ukwel kabsa...ukijifanya mzee wa kunyoksha maelezo atakuchoka mapema anaona mwanamme hauna jipya.

Hawa viumbe wanapenda mtu anaewarusha roho wapate kitu cha kufikiria kichwan mwao
Huwa hatujali wala nini, ila mioyo inakua imekufa
 
Unajua nini mkuu umeuliza swali la msingi sana Daah ningependa kusikia hoja zao ngoja tuwasikilize


kuna siku niliandaliwa ambush guest huko mkoani huko kwa hawa wasukuma nilikuwa na mwanafunzi , baba mtu akiwa na wadogo zake wawili wa kiume walitaka wavunje mlango watu walijazana nje sema walizuiwa polisi ndio walikuja kunitoa kuepusha ugomvi pale kipindi hicho naishi na huyu mwanamke sogeza tuishi ila alichangia pia ktk juhudi za mimi kutoka plus kuniletea msosi lock up Ila nashukuru Mungu ⁦⁩[emoji119] lile tatizo sijui liliishaje ndani ya siku tatu nilitoka japo mfuko ulitoboka nilikuwa nawaza pale nikivaa sare za njano na upara sijui itakuwaje

Sasa pamoja na kosa langu huyu mwanamke alisimama na mimi sijui kwenye kichwa chake aliwaza nini
Hujawahi muuliza
 
Back
Top Bottom